Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Kwani kutokuwekwa kwa mabango kulianza lini?ukipitia post nyingi unaona jinsi gani watu wasivojua mikataba inakuaje! Hivi unapoambiwa mkataba haujakamilika unaelewaje?
unaambiwa walitia saini gsm na tff kuwe na mabango uwanjani, tff hawakuweka, wewe unataka gsm walipe miezi mitatu, hivi hujui ukikiuka kipengele cha mkataba hauwi halali, gsm walikuwa wanawasubiri tff warekebishe dosari hizo, hebu tuone wansheria watakavochuana
Kama mabango hayakuwekwa na simba basi hapo kumbe Simba ndo walitakiwa wawajibishwe kwa kunyimwa hizo pesa za udhamini na sio kuhusisha Club zingine zilizotii sheria
Unaposema ukikiuka kipengele cha mkataba hauwi halali unatakiwa ujue kuwa sheria yeyote iliyowekwa kama muongozo wa utaratibu fulani inapaswa kufuatwa kama ilivyoandikwa
Sasa kuna sheria ya 16 ya udhamini inasisitiza kua
Nembo ya mdhamini mkuu wa ligi kuu itawekwa kwa rangi zake halisi katika mkono wa kulia kwenye sare (jezi) za timu za kuchezea na timu zitalazimika kufanya hivyo kwa michezo yake yote ya Ligi Kuu.
1.7 Klabu inawajibika kuheshimu masharti ya udhamini wa ligi kuu kimkataba kwenye michezo yake kama navyoelekezwa na TFF/TPLB, timu itakayokiuka itatozwa faini ya shiingi milioni tatu (3,000,000/) kwa kila mchezo itakaokiuka na inaweza kuchukuliwa
hatua zaidi ikiwemo kushushwa daraja na/au kufungiwa.
Kwa maelezo hayo we unaona Yanga kavunja sheria au hajavunja sheria?