Ali Kiba aizungumzia Wasafi Bet, asema yeye hana mpango wa kufungua kampuni ya betting kwa sababu dini yake hairuhusu, hajajua kuhusu dini ya Diamond

Ali Kiba aizungumzia Wasafi Bet, asema yeye hana mpango wa kufungua kampuni ya betting kwa sababu dini yake hairuhusu, hajajua kuhusu dini ya Diamond

Tuwekee Aya ya Quran hapa inayokataza...
"Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi(miziki),ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua ,na wanachukulia masikhara .Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha.(Qur'an 31:6) . Aya hiyo mkuu wafasiri wengi na maswahaba wa Mtume Muhammad (SwalaAllahu'alayhiWasalam) wamesema hayo maneno ya upuuzi yaliyotajwa hapo ni mziki mfno kibongo bongo mara nyegez ,kufumua mitaro,kupiga chapuo bia ,kudanga na ushenzi mwingine na watu haswa vijana wengi wanapotea Ktk njia ya Mwenyezi Mungu wanasikiliza na kupandisha stimu za kufanya maasi
 
Kama Umesoma dini sana utajua vyote havikuwahi kuruhusiwa wala kuwahi kutumika na Mtume ni watu wamejiibulia
Samahani Mkuu kwani miaka hiyo ya mtume kulikuwa na betting company kam ni Yes naomba uthibitisho Mkuu
#Asante sana
 
Hya ndo mambo yanafanya nisimpende ali hayuko kibiashara kabisaa hata kidogo hajui kuwa yy ni brand kubwa sana watu wanaitamani brand yake wapige Mahera ila lenyewe limelala yoooo
 
Mara nyingi huwa naheshimu maamuzi ya mtu, kwasababu huwa anaona mbali sana. Kwa Ali Kiba kuwa na maamuzi ya kukataa kufungua biashara ya betting ni jambo jema kwake kwani
1. Kweli tunamkosea Mungu lakini kuna hatua usitake kuzidisha zaidi
2. Sio kila analofanya mwingine nawe uige
3. Ulipofika sema sasa basi, ikiwezekana baki hapo hapo na baadae uache
 
Safi kabisa sio kila dhambi unashiriki utawachanganya malaika siku ya mwisho wasijue wanakupiga kwa rungu gani, [emoji16]

Long live the King.
Hish!! [emoji2305][emoji2305][emoji2305]
 
N aya gani katika Qur'an imekataza mziki?

Qaswida dufu sio mziki ule?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kwa taarifa yako hata qaswida hairuhusiw kidini, nyimbo yoyte yenye mapigo ya kimziki ni haramu labda zile wanazoimba na dufu tu sio hizi qaswida za kizanzibar ni haram...
 
Akiwa anaandaa hiyo aya basi na mimi naomba niandaliwe aya inayokataza kubeti
( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ )

المائدة (90) Al-Maaida

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
 
Kwa taarifa yako hata qaswida hairuhusiw kidini, nyimbo yoyte yenye mapigo ya kimziki ni haramu labda zile wanazoimba na dufu tu sio hizi qaswida za kizanzibar ni haram...
 
( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ )

المائدة (90) Al-Maaida

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
 
Kwa taarifa yako hata qaswida hairuhusiw kidini, nyimbo yoyte yenye mapigo ya kimziki ni haramu labda zile wanazoimba na dufu tu sio hizi qaswida za kizanzibar ni haram...
Hatutaki nye nye nyee!! Leta KIFUNGU..
 
Akuna dini imekataza mziki ila dini zote zinapinga miziki ya kidunia unasingizia dini wakat kwenye muziki wako kuna mabint wamevaa bikini mnashikana shikana kimahaba

Ila kla mtu anauhuru wa kuongea na kutoa maoni yake kulingana na katiba ya Tanzania inavyohusu japo alikua kenya pind anajibu
 
Tuwekee Aya ya Quran hapa inayokataza...
Soma katika Surat Luqman aya ya 6 na ya 7. Kisha usome maswahaba wamefasili vipi aya hizo. Rejea katika Tafsiri ya Ibn Kathir kwa maelezo zaidi.

Kadhalika katika hadithi za mtume jambo hili liko wazi kwa uchache hapa nakuwekea hadithi moja ila ziko zaidi ya moja.

Nanukuu :

Amehadithia Abuu ‘Aamir au Abuu Maalik kwamba kamsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na muziki. Baadhi ya watu watakuwa pembeni mwa mlima na mchungaji wao atawajia jioni na kuwaomba haja [fulani]. Watasema: "Rudi kesho". Allaah Atawaangamiza usiku, Atawaangushia milima kisha Atawabadilisha waliobakia wawe nyani na nguruwe na watabakia hivyo hadi siku ya Qiyaamah)) [Al-Bukhaariy].

Lakini vile vile katika dini yetu ya Kiislamu mambo ya kuimba imba ni katika kazi au shughuli za kina mama tena wakiwa wenyewe katika adha katika harusi au mfano wake.

Imamu Abuu Hanifa (Allah amrehemu) alipata kusema ya kuwa mwanaume anaye imba ni "KHANITHI" au kama alivyosema.
 
Back
Top Bottom