Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Nimekumbuka kitu,kuna comment nimeona Mdakuzi kasema Kiba hajamshirikisha Fally Ipupa kwenye remix ya mwana...please nieleweshe vizuri sijaelewa hapo
Wakati Mwana inaanza harakati za kurekodiwa, ilipangwa Fally Ipupa ashirikishwe ili apige verse moja na Kiba apige mbili. Hivyo akasikilizishwa beat na kupewa maudhui ya wimbo wenyewe, mwisho wakakubaliana kwamba Kiba aimbe sehemu yake kisha Fally angekuja kumalizia kutokana na ratiba yake.
Sasa baada ya Kiba kuingiza vocal kwenye sehemu yake ikaonekana kwamba wimbo umesimama sana bila hata Fally Ipupa kuingiza vocal, kwa hiyo ikaonekana kwamba kulazimisha Fally aingize inaweza kuharibu wimbo endapo itatokea bahati mbaya.
Hivyo, Kiba akaamua kufuta mpango wa Fally kuingiza vocal kwenye Mwana na badala yake akatayarisha wimbo mwingine na kumjulisha Fally Ipupa ambaye bila kinyongo akakubali, na moja kwa moja wakashirikiana kwenye wimbo mwingine ambao tayari umesharekodiwa na umetoka mkali ile kinoma.
Ukiisikiliza Mwana ikifika kwenye dakika 2 na sekunde kama 16 hivi, utaona kama kulikuwa na mtu anasubiriwa aingize, drums zinagongwa kwa pamoja na kinanda, kisha Kiba akamtaja Man Water, ambaye akaingiza ile vocal nzito nzito hivi ya 'Umeleta Lawama', sasa sehemu hiyo alikuwa anakaa mtu mzima Fally.
Kwa hiyo huo wimbo ni mwingine kabisa, wala sio Remix ya Mwana, ni wimbo mzuri sana. Fally katenda haki na Kiba ndio usiseme. Beat ni ya Man Water kama kawaida.
Ova