ushauri utasaidia nini na nyimbo nzuri zote keshaimba na kamaliza!..sasa anatumia nguvu tuu. ningekua karibu nae ningemwambia asihangaike kurekodi rekodi sasa upepo unavuma tandale na si dhani kama anaweza kuhit kiasi cha kumpita yule -----. kiba. a relax sasa hivi ajipange taratibu aki panick atajikuta anatoa nyimbo kumi halafu zote hazihiti, anaweza kuchanganyikiwa na kupotea kabisa. ajipange taratibu kipaji anacho asilazimishe kupaa kipindi hiki ambacho domo yuko juu atayumba sana.
kalagabaho Franklin speaking wewe ndio shabiki wa kiba wa kweli, shabiki damuu, this is my first time nimemnotes shabiki wa kweli wa kiba toka nijiunge na jf, and no doupt wewe ni miongoni wa wale team kiba ya watu watano ambao mwenyewe alikiri kuwatambua.
umeongea facts tupuuu ambazo hakuna hata mmoja anayejiita team kiba alishawahi kusema haya,wamekalia tu kumsifia kinafki, kelele nyingi eti kiba ndio anayekimbiza wengine watangoja sana, hivi kweli kama wewe ujiitae team kiba unampenda kiba toka moyoni unaweza kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kiasi hiki??? kiba anakimbiza wapi na anamkimbiza nani???
kwani ukimwambia ukweli kuwa hafanyi vizuri kwa sasa kwenye mziki, na ukampa ushauri nini cha kufanya ili arudishe heshima yake huoni kuwa hayo ndio yatakuwa mapenzi ya dhati kwake??? acheni kumlinganisha mondi na kiba tafadhali.
kiukweli mimi ni mmoja ya watu ambao huwa namponda kiba sana, na simpondi kwa vile eti simkubali au sitambui kipaji chake, namponda kwa sababu moja kubwa, kiba hakitendei haki kipaji chake, na tatizo kubwa la kiba anasubiri kipaji kimfanyie kazi badala ya yeye kukifanyia kipaji chake kazi, matokeo yake sasa asiyekuwa hata na kipaji kama yeye lakini anakifanyia kazi kipaji kidogo alichonacho mpaka kinaonekana kwa kutumia juhudi na maarifa ndio anaekubalika zaidi, sasa yeye badala ajiongeze nae aongeze juhudi zaidi kwenye kipaji chake analazimisha kuitwa mfalme, na kutaka kumzima daimond ziii kama mshumaa na wakati moto wa mondi umeshakolea na kila siku anauongezea petrol ili uzidi kuwaka na mashabiki tunaweka mafuta ya taa.
ushauri wangu kwa kiba, hizo nguvu anazotumia kutaka kuuzima moto wa mondi, azitumie kuwasha moto wake na sisi mashabiki tutaumwagia petrol.