Kuna kitu tunashindwa kuelewana na wengine kutokana na Kiba' Fans tunavyotazama au kuchukulia maisha ya muziki. Kabla hujasema chochote jiulizeni kwanza maswali yafuatayo.
Kupata mafanikio katika muziki ni nini? Kuwa na nyimbo nyingi redioni na kwenye TV's Stations? Kuwa na wanawake wengi? Kuripotiwa sana kwenye media kwa habari zisizohusu muziki?
Tumia akili yako binafsi kutafakari yafuatayo, hivi kufanikiwa kimuziki sio kutambulika kama mwanamuziki mkali na kujijenga kiuchumi kupitia muziki? Kuripotiwa na media kwa habari za muziki wako zaidi kuliko upuuzi wako mwingine? Kuwa na wimbo unaotamba?
Kwa kifupi hakuna ambaye hajakiri kama Kiba ni mwanamuziki mkali, kwani hajawahi kutoa wimbo mbaya, na hii ndio sababu ya yeye kujiamini na kuamua kupumzika kwa miaka mitatu na nusu na kutoa fursa kwa wengine kutamba.
Kiba amejijenga vizuri sana kiuchumi kwa sababu hata nyumba yake binafsi ya kuishi alimaliza kuijenga tangu 2007. Na zaidi na miradi ambayo ilimfanya amudu kuishi bila muziki kwa miaka mitatu na nusu mfululizo.
Kiba amekuwa ni mwanamuziki anayeripotiwa zaidi kuhusu muziki wake na ndio maana mpaka leo hakuna maisha yake binafsi yaliyo wazi, zaidi ya kujulikana ana watoto watatu aliozaa na akina mama tofauti.
Kwa kukazia ni kwamba, hakuna kitu katika maisha unaweza kufanya na kufanikiwa bila ya kujiwekea ratiba na ukaiheshimu ratiba yako. Sio kupelekeshwa na matukio yanayozuka kabla ya wakati wa ratiba uliyojipangia.
Kiba alijipa muda wa kupumzika, akaheshimu hilo, kisha akasema natoa wimbo mpya July, akautoa Mwana ambao aliurekodi 2012, so kama asingeheshimu ratiba yake angeutoa siku nyingi na kuvunja mapumziko yake.
Pia, baada ya kutoa Mwana (audio) alisema video atashoot November, na ndivyo alivyofanya, ni utaratibu wa kufuata ratiba uliyojiwekea katika kazi zako, sioni kile kinachoitwa uzembe au kulaza damu.
Upangaji huu wa ratiba ndefu ndefu za kutoa wimbo mpya hufanywa na wanamuziki wenye uwezo mkubwa tu, ndio maana Mwana inaendelea kufanya vizuri kwenye chart licha ya kukaribia miezi mitano sasa tangu itoke, nadhani video ikitoka nayo itakuwa na miezi mitano ya kutamba.
Kutoa nyimbo nyingi ndani ya kipindi kifupi ni kama kujimaliza mwenyewe wakati mwingine, ona Nassib alitoa Bum Bum, baada ya mwezi akatoa Mdogomdogo na moja kwa moja akaiua Bum Bum na sasa mimi binafsi naona kama kaiua Mdogomdogo kwa wimbo wa sasa ambao mapokezi yake si mazuri sana kwani ina video nzuri lakini audio ni ya kawaida sana (kwa maoni yangu).
Kabla Kiba hakuwa na management nzuri na hilo alikiri wakati akihojiwa na Clouds FM mwezi August kama sikosei na ndio maana akaamua kupumzika ili kujisahihisha, ila sasa ametimia karibu kila idara.
Mwacheni aheshimu ratiba yake, coz mpaka sasa bado hajaharibu popote kufuatana na ratiba yake.
Ova