Kama kusingekuwa na vilaza walioanza kuujua muziki wa Bongo Flava juzi juzi tu hapa, baada ya jirani yao wa Tandale kuanza kusikika, basi kusingekuwa na kelele za kipuuzi za baadhi yao. Ni wazi kumfananisha Kiba na mwanamuziki mwingine wa Bongo Flava ni sawa na kufananisha Mlima Kilimanjaro na fungu la korosho.
King Kiba aliongoza kwenye wimbo wa Hands Across The World, sio kwa kujichagua tu aongoze, ila kwa uamuzi wa mtunzi wa wimbo R Kelly, licha ya kuwako pamoja na mastaa wakubwa wa Afrika, R Kelly alisema Kiba ana sauti nzuri na ya kipekee, hivyo anapaswa kuongoza wimbo huo. Na ikawa hivyo.
Kama unafahamu Bongo Flava kitambo, utakuwa unajua kama wimbo wa Hands Across The World uliingia kwenye chart kubwa sana ya muziki ulimwenguni ya Billboards, ikiwa ni kwa mara kwanza mwanamuziki wa Tanzania kuwa na wimbo kwenye hiyo chart.
Mbali na hayo pia kundi la One8 na King Kiba na wenzake lilipata tuzo ya kuwa kundi bora la muziki la mwaka. Isitoshe kwa mara kwanza mwanamuziki wa Tanzania Ali Kiba, habari zake zililiripotiwa kwenye jarida la Billboard la Jan 8 - Mar 26, 2011, kwenye ukurasa wa 21.
Humo King Kiba ameelezewa kuwa mmoja wanamuziki wakali wa barani Afrika wa karne ya ishirini na moja, ambapo habari yenyewe iliandikwa na mwandishi wa Billboard mwenye ufahamu mkubwa muziki na vipaji vya muziki, aitwaye Diane Coetzer.
Bila shaka wakati utazungumza, tunaojua muziki na wanamuziki kitambo tutajulikana, na hata wale wenzangu na mimi wa fuata mkumbo baada ya jirani yao kuanza kuimba watajulikana. Haya sasa video ya Mwana iko njiani, sidhani kama Ijumaa itaisha bila kila mtu kuiona.
Naukumbuka huu msemo: Jiwe lisilo na shukrani huanguka - David Adeleke (Davido) Dec 10, 2014
Ova