Sitanii
nitah sio siri kwa ngoma alizonazo Kiba ingekuwa hawa wasanii wapenda sifa asingekubali kukaa nazo tu ndani na kutotoa wimbo wowote kwa miaka mitatu. Kila niliyokuwa nikisikiliza nikawa naiona kali kuliko nyingine, yaani wanaosubiri akosee watasubiri sana coz ana akiba ya madini ya maana.
Huwezi kumfananisha Kiba na Diamond ambaye alishirikishwa kwenye wimbo wa Naumia wa Dayna akaona binti kamfunika, matokeo yake verse yake aliyoiimba kwenye huo wimbo wa Naumia akaifanya kuwa wimbo wa My Number One na ndio maana unaona umekuwa mfupi sana.
Nilifanikiwa kuusikia wimbo wa Naumia huku Diamond akiwa ameingiza verse yake (ambao ndio umekuwa wimbo wa My Number 1), ulikuwa ni wimbo mkali sana na kwa kiasi kikubwa Dayna alimpoteza Diamond na matokeo yake akaamua kuiba beat moja kwa moja na kurekodi wimbo wake haraka haraka.
Fanya hivi, sikiliza verse za Dayna kwenye demo ya Naumia kama unayo, halafu sikiliza verse ya My Number 1, utaona Diamond anajibu verse za Dayna, mfano NAUMIA: 'Moyo umependa sikuwaza ingekuwa donda'. MY NUMBER 1: 'Kidonda chako kwangu maradhi.'
Wimbo ulihusu wapenzi walioachana, lakini mwanamke analalamika kuwa bado anampenda sana mpenzi wake na anaomba amhesabu kama mpenzi wake, ndio maana katika verse ya Diamond anaeleza 'Tumetoka mbali, matatizo ni changamoto'. Kama nikiipata tena ile demo, nitashukuru sana.
Nikirudi TZ nataka tushikie bango suala la Kiba kushiriki kwenye huu uzi, ili tukate ngebe za hawa wenye wenge la zomeo la Fiesta.
Ova