Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Nampenda sana Ali Saleh Kiba kutokana na mziki wake mzuri,sauti yake na hasa utunzi wake makini katika tungo zake mbalimbali mfano mzuri ni huu wimbo wake wa mwana unaotamba kwa sasa.
Video yake aliyoiachia jana ni nzuri sana,nimeipenda.
Ushauri wangu kwa Kiba,yeye ni msanii mkubwa sana,anatakiwa abadilike afanye mambo makubwa kama lilivyo jina lake.Asifanye mziki kwa mazoea kisa ana kipaji kikubwa.Aijue thamani yake sasa maana nakumbuka aliwahi kusema kua amekua surprised kwa mashabiki wake kumuulizia hadi walitaka kufanya maandamano japo alikaa kimya kwa zaidi ya miaka miwili!
Pia Kiba fans wenzangu huu ndio wakati wa kumsapoti Kiba,yeye kaonesha juhudi na sisi hatuna budi kumsapoti katika mziki wake ili naye apate mafanikio kulingana na kipaji chake kikubwa ambacho kiukweli hakiendani na mafanikio yake kimuziki.
Haswaa! Umeshusha maoni kama vile ulikuwa kichwani mwangu. Nice.
Ova

