Ali Kiba Fans' Special Thread...

Ali Kiba Fans' Special Thread...

Morning people,nasikitika kutangaza kifo cha member mwenzetu kwa I'd ya NkyaH!Inasikitisha sana,sikujua kama kijiba cha roho kinaua!RIP
 
Last edited by a moderator:
Morning people,nasikitika kutangaza kifo cha member mwenzetu kwa I'd ya NkyaH!Inasikitisha sana,sikujua kama kijiba cha roho kinaua!RIP

Dimondi ndomo alifikisha hizo ndani ya masaa 10 tu... Vipi zitafika laki 5 kweli??
 
Last edited by a moderator:
View attachment 212894
Hii inafundisha kwamba unaweza kufanya muziki mzuri na watu wakaupenda bila kusaka scandal za kila kukicha.
Pia, hii inafundisha kwamba unaweza usiimbe mapenzi, wala video yako isijae matukio ya mapenzi na bado watu wakaipenda.
Ukiamua kuishi kwa ajili ya muziki, basi fanya muziki kwa kufuata misingi yake na kuboresha muziki wako ili mashabiki waupende bila sababu ya ziada inayohusu maisha yako biafasi.
King Kiba kwa hili umekuwa mwalimu mzuri kwa vijana waliowasaidia kuwatoa kimuziki. Hongera sana. S/o
Ova

Huyu jamaa atachukua BET asee.. Anatisha sana ahahaha lazima awe shortlisted kwenye matuzo kibaoo
 
Mleta uzi una elimu ya upagaji picha na uongozaji picha mtembeo, mpaka utoe "hukumu" kwa video ya Mwana?

nimeitazama video hiyo zaidi ya mara tatu na hivi ndio nivyoviona;

1. abstract story - katika sanaa kuna kitu kinaitwa "abstract" ambapo huoni maana au ujumbe moja kwa moja mfano kama unatembelea maonesho ya sanaa za uchoraji, ukitazama abstract paint kama huna elimu ya sanaa hiyo huwezi jua maana.
nirudi kwenye "video ya Mwana abstract meaning"... hadithi ni juu ya maisha ya kila siku ya guru/mfalme wa jukwaa/mwanamuziki ambaye kila akiamka huongea na "the man on mirror" kama sehemu ya kujiuliza alipotoka na anapokwenda. Philosophy inatu-encourage tujiulize maswali kila siku kama sehemu ya kufahamu muelekeo wetu sahihi juu ya yale yanayotukabili. kuongea peke yako katika kioo ni moja ya semhemu ya kujipa "confidence".

mfalme/guru huyu mbali na umaarufu wake anatembea kwa miguu na yuko "free from stresses" anajiamini kile anachofanya na wala hajali nani atasema nini juu yake "anacheza muziki barabarani"

Anajua kazi yake viivyo na anaongoza kwa mifano "anakuta dancers wanabishana anawafundisha kucheza hiyo choreography vizuri na wanafurahi kuelekezwa". Mfalme/guru huvishwa na hilo tunaona mrembo akimvisha Kiba.
scene za mwisho mostly ni kuonesha au kutoa hitimisho kuwa huyu mtu ni mfalme au guru wa wawapi? tunaona performance na audience wakimshangilia kwa kile anachefanya sahihi, inaonekana huyu ni mtu maarufu hapa na anafanya kazi yake vyema.
Cutaways za kiti ni ishara ya utukufu/mafanikio/where he belongs. kusimama juu ya kitu kirefu inamaanisha "he is on top of the World" he is above everything in his sphere/World/career/game.

2. KISS (Keep it Simple and Short) Writers, Directors, DoP, n.k katika industry ya film wanaamini kuwa unapofanya sanaa simple and short watu wengi wanaelewa na inapendwa. mfano, kwa nini filamu ya 12 years a slave ilfanya vizuri katika tuzo za Oscar kuliko Wolf of Wall Street? mwaka huu Maleficent ya Angelina Jolie na A Milion Ways to Die in the West hazipo hata kwenye orodha ya tuzo za Golden Globe zitakazofanyika January 2015 na hizi ni block buster films hadithi ya kawaida kabisa katika film kama Selma au Grand Budapest Hotel zinafanya poa. siri ni moja tu hadithi nzuri ambayo kila mtu anaielewa ndio hadithi inayofanya vizuri. Video ya mwana Hadithi yake imekaa vizuri kwa kua ni rahisi kueleweka na ni maisha ya kila siku.

3 Kwa nini haonekani huyo mwana aliyeimbwa? swali linaloumiza akili za wengi, jibu ni rahisi kuwa Ali Kiba ametaka kuonesha umahiri wake, kuwa yeye ni nani kwenye muziki hivyo ameamua kuonesha zaidi kuwa "mfalme amerudi" pale anapotakiwa kurudi ndio sababu kuu ya kutumia "abstract" meaning zaidi. so, relaxxx filming imepiga hatua sio neno kwa picha ila ni beauty/aesthetics na meaning!!!

4. binafsi nimeridhika na upigaji picha, matumizi ya taa, lenses na hata filters. DoP amefanya kazi yake, Director amefanya majukumu yake, wadrobe dept + Hair & make-up dept wamefanya majukumu yao.

video inanifanya mimi kama mtazamaji nivutiwe kuiangalia mara kwa mara, kwa kuwa hadithi yake ni maisha yangu ya kila siku hata kama sijui kinachoimbwa.

Akhsante kwa leo, ila Director wa video za Diamond Platnumz ni mzuri pia na anajua anachofanya. kabla ya ku-judge ni vyema tukajifunza taaluma zenyewe.

REFERENCES:
Cinematography Theory and Practice (SECOND EDITION) - Blain Brown; Focal Press (2012)
Filming the Fantastic - Mark Sawick; Elsevier Inc. (2007)
Hii ilikuwa ni elimu nzuri sana ya bure, nikategemea wabishi wangetaka kujifunza na kuuliza maswali kwa huyu jamaa, lakini ajabu walikaa kimya kwa sababu ya ubishi tu.
Hebu badilika iruhusu akili yako ikubali kwamba JF ni sehemu ya kujifunza coz watu wenye Uwezo mbalimbali wa kitaalamu wa mambo tofauti. Binafsi imenisaidia kujifunza mambo mengi.
Ova
 
Dimondi ndomo alifikisha hizo ndani ya masaa 10 tu... Vipi zitafika laki 5 kweli??


Wakati huo alikuwa keshatuonyesha picha alizopiga na zali airport,analalamika kaachwa na wema,tukaambiwa pia hata gari alilopewa zawadi lilitoka kwa jamaa mwingine.tehh tehh tehh.
Chezea kick wewe.

Acha watu waonyeshe uwezo pure.
 
Unasifu video ya alikiba imepata views zaidi ya laki kwa cku tatu akati video ya diamond ya ntampata wapi ilipata views zaidi ya laki ndani ya masaa 22......tatizo niushabiki wa mwanamziki badala kua na ushabiki wa mziki.....mwenye akili kanielewa
 
Unasifu video ya alikiba imepata views zaidi ya laki kwa cku tatu akati video ya diamond ya ntampata wapi ilipata views zaidi ya laki ndani ya masaa 22......tatizo niushabiki wa mwanamziki badala kua na ushabiki wa mziki.....mwenye akili kanielewa


Kama huna mahaba na diamond kwanini umeshangaa jamaa kutaja views za kiba,na badala yake ukalinganisha na alizopata diamond!!!?
 
Back
Top Bottom