Ali Kiba hatendewi haki, Watanzania tuache ukatili

Ali Kiba hatendewi haki, Watanzania tuache ukatili

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Sio mpenzi sana wa kutoa maoni yangu kwa mambo madogo madogo hasa yasiyo ya lazima kama mambo ya muziki na filamu. Ila leo nimeona sio vibaya kusema kitu kwa huu uonevu unaondelea kwa komredi Ali Kiba. Mimi ni mpenda haki kwahiyo nimeona sio sawa kukaa kimya mtu anapoonewa.

Kwa muda mrefu kijana Ali Kiba amekuwa hatendewi haki na watanzania wenzake kwa maana ya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwa akitwishwa mzigo mzito usiomstahili. Hii sio sawa. Kitendo cha wananchi walio wengi kumpambanisha kimuziki komredi Ali Kiba dhidi ya komredi Diamond Platnumz Simba, sio sawa na ni uvunjifu wa haki za binadamu.

Hii ni sawa na bondia wa uzito wa chini kumpambanisha na Twaha Kiduku. Komredi Simba kwenye tasnia yake ni kama nyangumi baharini. Ni mkubwa sana. Ni mwanamuziki mwenye tuzo nyingi zaidi za kimataifa hapa nchini. Ana rekodi ambazo ni ngumu komredi Ali Kiba kuzikaribia huko YouTube na maeneo mengine. Isitoshe kiuchumi komredi Simba ni mkubwa mno kufananishwa na King Kiba. Namna pekee ya komredi Kiba kumpita Simba kiuchumi ni kuwahi kulala ili ampite akiwa ndotoni. Kimsingi Ali Kiba hatendewi haki. Hii itasababisha komredi Kiba kupata msongo wa mawazo na kuanza kulipua kazi kwasababu ya presha za wananchi wanaotaka awe zaidi ya Simba.

Komredi Ali Kiba anamzidi Komredi Simba mambo machache sana kama vile sauti nzuri na utunzi wa mashairi yanayodumu. Ila kwa matokeo ya jumla Simba yuko mbali mno. Nadhani kwa sasa watanzania tuache huu ukatili. Ingependeza Komredi Ali Kiba apambanishwe na wanamuziki walio kwenye level moja kama Bill Nas, Meja Kunta, Nuh Mziwanda, Queen Darlin, Shishi Baby, Ben Paulo, na huyu Official Nai. Simba tumwache atuwakilishe level za dunia.
 
Kwani likizo hii umeenda kwa Bibi, umebaki nyumbani kupambana tuition, upo uswahilini kwenye kamari ya bonanza, upo mtaani na waimbaji wa Singeli, au upo toilet!!!
 
Back
Top Bottom