Ali Kiba ni msanii anayekuzwa kuliko uwezo wake (Overrated)

Sikiliza "Aje" Ali Kiba ft M.I. Halafu tuijadili kuanzia beat, melody, harmony, creativity, lyrics, wordplay, punchlines, imagery etc.

Kama unafahamu vitu hivyo ni nini.
Hizo mbwembwe zote hazina maana mkuu.. Mtu anaposikiliza nyimbo anataka aburudike au aelimike au awe elevated spiritually! Kama nyimbo ililenga kuburudisha lakini lengo hilo halijatimia haijalishi sijui umetumia ujuzi gani wa kitaalamu hiyo nyimbo still ni failure..

Ni sawa sawa na kipindi kile imetoka video ya lupela na majority ya watu wakatoa maoni yao kuwa video ni mbovu.. Akajitokeza 'mtaalamu' Adam Juma wa Visual lab akaitetea kitaalamu kwa kutoa hoja kibao za 'kitaalamu'. kitu ambacho anasahau ni kuwa mtu wa kawaida hawana mda na hayo mambo ya kitaalamu, anapokaa sebuleni kwake anaangalia TV anataka video inayochezwa mbele yake iburudishe macho yake kama haibirudishi macho yake haijalishi ina mbwembwe gani za kitaalamu (kama alivyoeleza yeye na unazojaribu kueleza wewe) hiyo video bado inakuwa imefeli!
 
Usingecoment hii thread ningeshangaa sana... cc @k4real
 
Nifah kuna uhuru wa kutoa maoni.... hayo ni maoni yake... mbona amekuudhi tu kuexpress maoni yake
 
Ofcoz ye ndo mfalme wa Bongo fleva kama unajua nin maana ya Bongo fleva
Hao wengine walishaipoteza ile taste halisi Bongo fleva
Kina Dully sykea wajiitaje sasa
 
Nifah kuna uhuru wa kutoa maoni.... hayo ni maoni yake... mbona amekuudhi tu kuexpress maoni yake
Hayo sio maoni ni mtazamo.
Ingetosha kama angekaa kimya na mtazamo wake, lakini kauweka katika jukwaa maana yake tuchangie/tupingane au hata kumkosoa.
Na ndicho nilichokifanya...
Period
 
Dully Sykes anaimba nini na wewe?
Si bora hata ungesema Q-Chillah?
Jinga kabisa.
Dully ndo King wa Hits za Bongo fleva.... anaybishana nae wapande stage moja halafu waanze kupiga ngoma moja moja tu ile toa kitu nitoe... halaf uone
 
Dully ndo King wa Hits za Bongo fleva.... anaybishana nae wapande stage moja halafu waanze kupiga ngoma moja moja tu ile toa kitu nitoe... halaf uone
Kwa hits zipi jamani?
Hizi habari za vijiweni unataka kuleta huku sasa.
Mambo ya Salome sijui Handsome utamletea nani kwa sasa?
Yani sasa hivi hata unipigie Dhahabu ambayo kwangu mimi ndio track kali zaidi ya Dully sishtuki.
 
Wabongo tuache unafiki jamani, kipaji cha muziki cha kiba hakihitaji akili nyingi kukiona. Ukiangalia vigezo vya mwanamuziki, ikiwepo vocal Ali kiba anayo na mashairi anajua kutunga. Sikiliza vizuri ngoma kama AJE utajua jamaa anajua haswa mziki, na vocal yake sio ya kawaida. Binafsi kitu pekee nnachoona Mond anamshinda Kiba ni ujanja ujanja tu wa hapa na pale, na vimbinu flan flan tu, pengine na management inahusika kwa namna moja au nyingine. Ila kiba mziki anaujua, na ana-meet vigezo vingi sana vya muziki kuliko Mond ambae ana bifu na live perfomance jukwaani. Binafsi naona kwa mfano ukimchukua mtu anaejua haswa mziki na asiewajua kabisa hawa watu wawili na asiejua chochote kuhusu hizi team zao, akaskiliza ngoma zao na akaulizwa nani hasa anajua mziki atasema Kiba. Mi sio mshabiki wa Kiba kivile ila jamaa mziki anaujua, huo ndo ukweli.
 
Kwa hits zipi jamani?
Hizi habari za vijiweni unataka kuleta huku sasa.
Mambo ya Salome sijui Handsome utamletea nani kwa sasa?
Yani sasa hivi hata unipigie Dhahabu ambayo kwangu mimi ndio track kali zaidi ya Dully sishtuki.
Ila ukipigiwa mwana unashtuka... sio hizo tuu....

HI,baby candy, bijou, Bongo Fleva,hunifahamu,utamu... still counting
 
Ila ukipigiwa mwana unashtuka... sio hizo tuu....

HI,baby candy, bijou, Bongo Fleva,hunifahamu,utamu... still counting

Mfalme wa hits za zamani bora ungesema Nature, huyo Dully hafurukuti mbele ya kiroboto.
Anyways, baki na unalo amini...
Let's call it a day.
 
Sikiliza "Aje" Ali Kiba ft M.I. Halafu tuijadili kuanzia beat, melody, harmony, creativity, lyrics, wordplay, punchlines, imagery etc.

Kama unafahamu vitu hivyo ni nini.
Kiba hamna kitu cku izi embu kasikilize mapenzi yana run dunia au dushelele halafu uone hata km iyo aje ina fit sehemu
 
kiba alikuwa maarufu kabla ya mond sasa anakwezaje kuliko uhalisia...fikir kabla ya kuandika
 
Kinachonisikitisha ni jinsi wanavyomjaza kichwa matokeo yake anabaki palepale, yanakuja madogo kama Harmonize yanampita huku fursa anaziona, so sad, tatizo wabongo hatupendi kuambizana ukweli

Teh teh teh!
Hapa pana ka ukweli fulani japo Ali Kiba kwenye utunzi na uimbaji atabaki kuwa yuko juu.
Sema sasa ukitoa AJE, jamaa hana video ya maana kiukweli.
 
Nahisi kuna watu huwa wanatafuta "comments" si bure...Hivi unadhani kila msanii anapendwa/anawafurahisha watu wote!? Kuna styles tofautitofauti kama ilivyo "taste". Hushangai kwa nini pamoja na wewe kumuona hivyo bado ana washabiki wengi...!!!!!
 
Kiba hamna kitu cku izi embu kasikilize mapenzi yana run dunia au dushelele halafu uone hata km iyo aje ina fit sehemu

Kaka ujuzi huwa hauozi sema tuna kujisahau sana Watanzania!
Ali kiba akutuliza kicha vizuri atarudi kuwa yuleyule wa 2007 wa nakshi nakshi!
Ukumbuke hata Jay Z kuna kipindi ilimwia sana vigumu kurid kwenye muziki, lakini akatulia management yake ikakaa vizuri akaja kutoka na Blue Print 3 na Watch the Throne.
Kila kitu ni mahesabu tu ndugu yangu!
 
Kiba hamna kitu cku izi embu kasikilize mapenzi yana run dunia au dushelele halafu uone hata km iyo aje ina fit sehemu
Muziki ni kitu subjective. Huwezi kuupima kwa kilo wala mita.

Nimetaja vigezo vya kuangalia hapo juu.
Ali Kiba anatoa nyimbo melodic. Granted sio zote zitakuwa the best, lakini hata "Thriller" ina nyimbo zilizozidiana.

Kwangu mimi, mtu ambaye nafuatilia muziki mpaka nikaitwa kwenye talent competition kuwa jaji wa mashindano ya muziki, Ali Kiba anatupa muziki murua kabisa. Asichoweza ni promotion na the business side ya kumfanya aonekane yupo juu.

Wengine wanaiweza promition kuliko muziki wanainekana wako juu.

Lamini hilo ni kwa sababu watu wengi wanaangalia promotion, hawasikilizi muziki kwa sikio la Phillip Glass.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…