Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,717
Hizo mbwembwe zote hazina maana mkuu.. Mtu anaposikiliza nyimbo anataka aburudike au aelimike au awe elevated spiritually! Kama nyimbo ililenga kuburudisha lakini lengo hilo halijatimia haijalishi sijui umetumia ujuzi gani wa kitaalamu hiyo nyimbo still ni failure..Sikiliza "Aje" Ali Kiba ft M.I. Halafu tuijadili kuanzia beat, melody, harmony, creativity, lyrics, wordplay, punchlines, imagery etc.
Kama unafahamu vitu hivyo ni nini.
Ni sawa sawa na kipindi kile imetoka video ya lupela na majority ya watu wakatoa maoni yao kuwa video ni mbovu.. Akajitokeza 'mtaalamu' Adam Juma wa Visual lab akaitetea kitaalamu kwa kutoa hoja kibao za 'kitaalamu'. kitu ambacho anasahau ni kuwa mtu wa kawaida hawana mda na hayo mambo ya kitaalamu, anapokaa sebuleni kwake anaangalia TV anataka video inayochezwa mbele yake iburudishe macho yake kama haibirudishi macho yake haijalishi ina mbwembwe gani za kitaalamu (kama alivyoeleza yeye na unazojaribu kueleza wewe) hiyo video bado inakuwa imefeli!