Ali Mufuruki on ITV: Kilimo kwanza kiliishia wapi? Viwanda vya Saruji kupata hasara si ishara nzuri

Wivu wa kike unakisumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa Anaongea fact Sana ushauri wake ukifuatwa tutapiga hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
Pamoja na kuwa Franchisee wa Woolworth Tanzania na Uganda, pia ni mwanzilishi na CEO wa Infotech Investment Group. Miezi michache iliyopita Tume ya Ushindani ilitoa tangazo lifuatalo:


Mafuruki alikuwa na mpango wa kununua 50% za Wananchi... ukichanganya na ile yake 1% ambayo bila shaka aliipata kwa kuitumikia Wananchi kama Mwenyekiti, hapo ni kwamba atakuwa ba 51% na kuwa largest shareholder.

Moja ya biashara zinazofanywa na Wananchi Group ni pamoja na ZUKU Satelite TV pamoja na ZUKU Fibre wanaotoa huduma za internet na mawasiliano.
 
Very funny!

Yaani mtu ambae yupo kwenye private sector for almost 30 years bado ni lazima asome Google kufahamu mazingira ya biashara ya Tanzania na nini kinahitajika?!

Ameshawahi kuwa mwenyekiti au bado Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania!

Hapo kabla au hadi sasa amepata kuwa board member wa Mwananchi Communication, Nation Group (KE) pamoja na Stanbic Tanzania pamoja na ATC!

Nadhani hadi sasa bado ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wananchi Group inayomiliki ZUKU tv & ZUKU Fibre!

Yaani kwa akili yako mtu kama huyo atashindwa kufahamu nini kinahitajika Tanzania when it comes to business?!
 
nlikuwa najua swala la viwanda ni bongo muvi jana nlimsikiliza huyo mtaalam nimeona ni zaidi ya komedi
 
Ni mmoja kati ya wachache walioifilisi CRDB orijino Kabla haijachukuliwa na akila Kimei. Baadaye aliunda kikampuni kikiitwa infosys ambacho kilitajwa kwenye mambo ya Lugumi na Polisi wao. Kikampuni kikawa uchochoro wa kupitishia pesa nzito za mirahi krk awamu za upigaji. Mtu huyu hafai hata kusikilizwa.

Tatizo pia ni hao waandishi wa habari, Wanatafuta mtu wa kuzungumzia mambo muhimu ya kitaifa bila hata kuangalia historia yake na bila kumuuliza mambo yake ya nyuma. Anapoachiwa kubwabwaja, baadaye anawekwa kwenye kundi la wenye influence. Baadhi yetu wenye ufahamu wa mtaani tunamuona bonge la mtaalamu! Anatakiwa asipewe muda wa 'kuelimisha' umma, badala yake aitwe kuulizwa mambo yake ya hovyo hovyo.
 
nlikuwa najua swala la viwanda ni bongo muvi jana nlimsikiliza huyo mtaalam nimeona ni zaidi ya komedi
Soma msg hizi ili baadaye ujue uliyemsikiliza siyo mtaalamu, ni Bonge la Tapeli.
 
I missed it! Sikujua kama kutakuwa na madini, nikatazama mechi.
Media za Bongo hazishawishi kuziamini.
 
Ha ha ha, mkuu hata wewe ukiamua kusoma taarifa husika kwa ajili ya presentation inawezekana, na tunaweza kudhani unajua sana kwenye hiyo sekta.

Applicability ndo changamoto, ni sawa na Mwl Kashasha anavyochambua mpira, mpe ukocha uone.
hakuna mfanyabiashara kwa kiwango cha mufuruki halafu awe bogasi kichwani
 
hakuna mfanyabiashara kwa kiwango cha mufuruki halafu awe bogasi kichwani

Mkuu point yangu ni kwamba mtu ukijipa homework ya kutafuta info kwa ajili ya presentation, unapitia madesa kadhaa na unapata mifano, ukienda kufanya presentation unaweza kuonekana kichwa.

Changamoto inakuja pale unapotakiwa kufanya practice ya hicho unachokielezea.

Nikatolea mfano hawa wachambuzi wa mpira ukiwapa ukocha hawawezi kitu ila kuongea mpira wanaweza.
 
Upande wa giza wa wafanyabiashara wengi wa Tanzania unatisha sana na kutukatisha tamaa sana sisi wengine tunaopambana na kuwa na doto ya kuwa matajiri wakubwa maana kila tajiri akitajwa humu watu wanafunguka vyanzo vyake vilivyopatikana kiasi cha wengine kuogopa na kuwa na mashaka kama kweli tutafanikiwa kwa michongo hii halali bila haramu..

Inaonekana Tanzania huwezi kutoboa bila haramu, maana sijasikia bado tajiri mkubwa mtanzania mweusi ambaye ameanzia chini mpaka kufikia level za utajiri wengi utasikia walikuwa wafanyakazi wa umma tena wenye vyeo wakatumia mianya na nafasi zao kupiga hela na kuja kuwekeza kwenye biashara halafu leo wanakuja kutuinspire mara ooooh mimi nilipambana nilianza vile nikafanya hivi mara ooooh na blah blah nyingi kumbe kuna dark side ndio chanzo cha utajiri mhusika hasemi.. VIJANA TUNA KAZI SANA KWENYE MAPAMBANO YETU..
 
hakuna mfanyabiashara kwa kiwango cha mufuruki halafu awe bogasi kichwani
Naona ni mmoja wa wale ambao hawana elimu. Unaweza usiwe bogasi (bogus), uwe smart lakini morally dead na ukafanikiwa. Tusipende kushabikia bila kuhusisha vichwa kikamilifu.
 
Nilimsikia huyu mtu ana exposure kubwa ya biashara
Aaaah! kila mtu ana exposure ya kazi yake. Mkulima wa mtama pale Dodoma ana exposure kubwa ya kilimo chake.

Hawa wengine ni trick stars of tricksters. Wanaandika hata vitabu juu ya maisha yao na mafanikio ya biashara zao. Hata siku moja huwasikii wakisema walichokwapua serikalini na kuumiza wa-TZ wenzao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…