Nimemsikiliza, ana mambo mazuri sana na uelewa mkubwa wa masuala ya uwekezaji na mitaji.
Alitolea mfano Singapore, wanapotafuta mwekezaji, wanakuwa wamefanya utafiti wa kutosha juu ya uwezo was Hugo mwekezaji wanayemtaka, na wao kama nchi wanakuwa pia wamekwisha Fanya utafiti wao na kuweka mazingira rafiki, pamoja na kumhakikishia faida atakayopata.
Pia wanamhakikishia Sera zisizobadilika badilika kwenye uwekezaji. Nimemfurahia sana, na watendaji wetu has a TIC na Waziri wa viwanda na biashara, wana kitu cha kujifunza.
Amedai, huwezi kusema tunataka kuwa nchi ya viwanda bila kuainisha aina ya viwanda, mkakati wa kupata wataalamu, mkakati wa kupata malighafi na masoko pia. Akatoa mfano, Tz kwa mwaka wahitimu mainjinia ni 1,200 nchi yenye watu milioni 50 wakati Singapore watu mil 30 inawahitimu zaidi ya laki moja kwa mwaka.