Ali Mufuruki on ITV: Kilimo kwanza kiliishia wapi? Viwanda vya Saruji kupata hasara si ishara nzuri

Ali Mufuruki on ITV: Kilimo kwanza kiliishia wapi? Viwanda vya Saruji kupata hasara si ishara nzuri

Ali Mfuruki hakika ulikua unatiririka vizuri kwenye kipindi kuhusu uchumi Wa nchi.Kwa Bahati mbaya huku Moro w
amekata Umeme ili tusisikie Nondo wapi tumejikwaa na tufanye nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameulizwa swala la Kenya kuwa ndio exporter namba 1 wa parachichi wakati sisi tuna ardhi kubwa kuliko kenya.

Akajibu changamoto iliyoko tanzania ni kutokuwepo kwa commercial farming na kutokuwepo kwa agri proccesing industry..
Ametoa mfano bukoba ( kimondo bay sina hakika na usahihi wa hili jina) kilimo cha parachichi kinafanyika lakini

1. hakuna kiwanda cha kuongeza thamani ya parachichi

2. Gharama za usafirishaji kuzipeleka mwanza ni kubwa sana hali inayopelekea bei ya mwisho kwa mlaji kutokuwa nzuri sana.
 
Mfuruki ni mjanja mjanja tu wa hapa mjini. Fobes wanasema Jamaa yupo top 10 kwa matajiri Tanzania, wakati jamaa hatujui kabisa bussness zake zaidi ya maduka ya Wolwoth sidhani kama ana kiwanda or tangible investmen

Nakubaliana na wewe kuwa huyu ALi MFURUKI NI MJANJA MJANJA MMOJA HAPA MJINI. Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri mtakumbuka kuwa huyu bwana aliwahi kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa board ya ATC [shirika letu la ndege ] na akiwa na wadhifa huo ndio akatuingiza ubia na shirika la ndege la Afrika ya Kusini [SAA]. Ubia kati ya mashirika haya mawili ulikuwa kwa faida zaidi ya wenzetu kuliko shirika letu kiasi kwamba ATC ilibambikizwa madeni hewa under Mfuruki's watch kumbe huku yeye alikuwa anavuta mkwanja kwa njia za kiwizi!!

Hata hiva sasa bado shirika na ndege la Africa Kusini linadai ATC Fedha nyingi ambazo huko mbele zinaweza kusababisha ndege zetu mara zikitua huko zikakamatwa kwasababu ya ufisadi wa huyu bwana na genge lake!! Ni mnafiki anyejifanya kuwa ni mzalendo kumbe ni muongo anayeishi kwa Ujanja Ujanja tu wa TAX AVOIDANCE/ EVASION!!!
 
Nakubaliana na wewe kuwa huyu ALi MFURUKI NI MJANJA MJANJA MMOJA HAPA MJINI. Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri mtakumbuka kuwa huyu bwana aliwahi kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa board ya ATC [shirika letu la ndege ] na akita na wadhifa huo ndio akatuingiza ubia na shirika la ndege ya Afrika ya Kusini [SAA]. Ubia kati ya mashirika haya mawili ulikuwa kwa faida zaidi ya wenzetu kuliko shirika letu kiasi kwamba ATC ilibambikizwa madeni hewa under Mfuruki's watch kumbe huku yeye alikuwa anavuta mkwanja kwa njia za kiwizi!!

Hata hiva sasa bado shirika na ndege la Africa Kusini linadai ATC Fedha nyingi ambazo huko mbele zinaweza kusababisha ndege zetu mara zikitua huko zikakamatwa kwasababu ya ufisadi wa huyu bwana na genge lake!! Ni mnafiki anyejifanya kuwa ni mzalendo kumbe ni mou anayeishi kwa Ujanja Ujanja tu wa TAX AVOIDANCE/ EVASION!!!
Na kipindi hicho ndo akaimarisha hiyo W-stores..si mbaya kama amekuwa mzalendo siku hizi..ahhhaaahh.
 
Kwa hivyo anashauri nini kuhusu uwekezaji wa viwanda?
Tuache sababu ya muda au tuendelee?

Watanzania kwa kutaka njia ya mkato na matokeo makubwa sasa ndio maana tulichotwa akili
"Kasi mpya hari mpya"
Mara tunasikia
"Big result now (BRN)"
 
Kwa hivyo anashauri nini kuhusu uwekezaji wa viwanda?
Tuache sababu ya muda au tuendelee?

Watanzania kwa kutaka njia ya mkato na matokeo makubwa sasa ndio maana tulichotwa akili
"Kasi mpya hari mpya"
Mara tunasikia
"Big result now (BRN)"
Na sasa eti hapa kazi tuuuu!! Hakuna kitu!!
 
Hebu tupeni Cv ya Ally Mufuruki wakuu.

Huyu jamaa atakuwa hajasoma UDSM aisee hii ni Havard Bussiness School (HBS) or Massachusetts Insititute Of Technology (MIT) maana kwenye masuala ya viwanda jamaa yuko well informed.

Over
 
Sisi serikali itafanya kila kitu.
Wasihofu kuhusu uwekezaji, serikali yetu itawekeza kwenye kila kitu.

Tunajenga viwanda, jenga reli, jenga mabwawa ya maji kuzalisha umeme, kujenga barabara na fly overs, tutanunua madawa, tunasomesha watoto bure, tunaajiri.
 
Nimemsikiliza, ana mambo mazuri sana na uelewa mkubwa wa masuala ya uwekezaji na mitaji.

Alitolea mfano Singapore, wanapotafuta mwekezaji, wanakuwa wamefanya utafiti wa kutosha juu ya uwezo was Hugo mwekezaji wanayemtaka, na wao kama nchi wanakuwa pia wamekwisha Fanya utafiti wao na kuweka mazingira rafiki, pamoja na kumhakikishia faida atakayopata.

Pia wanamhakikishia Sera zisizobadilika badilika kwenye uwekezaji. Nimemfurahia sana, na watendaji wetu has a TIC na Waziri wa viwanda na biashara, wana kitu cha kujifunza.

Amedai, huwezi kusema tunataka kuwa nchi ya viwanda bila kuainisha aina ya viwanda, mkakati wa kupata wataalamu, mkakati wa kupata malighafi na masoko pia. Akatoa mfano, Tz kwa mwaka wahitimu mainjinia ni 1,200 nchi yenye watu milioni 50 wakati Singapore watu mil 30 inawahitimu zaidi ya laki moja kwa mwaka.
Hii inawezekana pale ambapo idara za usalama zinafanya kazi kwa maslahi ya taifa na siyo ya serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu tupeni Cv ya Ally Mufuruki wakuu.

Huyu jamaa atakuwa hajasoma UDSM aisee hii ni Havard Bussiness School (HBS) or Massachusetts Insititute Of Technology (MIT) maana kwenye masuala ya viwanda jamaa yuko well informed.

Over

Ha ha ha, mkuu hata wewe ukiamua kusoma taarifa husika kwa ajili ya presentation inawezekana, na tunaweza kudhani unajua sana kwenye hiyo sekta.

Applicability ndo changamoto, ni sawa na Mwl Kashasha anavyochambua mpira, mpe ukocha uone.
 
Back
Top Bottom