Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Nimejaribu kuhusisha hotuba ya baba askofu na alicho kiandika huyu mzee, sijaona muunganiko wowote wallah; maandishi marefu lakini hayahusiani hata kidogo na hotuba ya baba askofu ya siku ya pasaka, unless mtu mmoja anielekeze hili, binafsi nimetoka bilabila
 





 
Mkwizi...
Watu wanaghitilafiana sana katika kuelewa.
Kuna watu wengi historia hii imeasisimua kwa kwa kuwa wameielewa.

Dunia ndivyo ilivyo.
Wako wanaoelewa na wako pia wanaoshindwa kuelewa.

Angalia alama za mtihani.
Juu wanaopasi sana wanakuwa wachache.

Hawa ni wale walioelewa somo vizuri.

Chini kunakuwa na mkururo wa watu wengi hawa hawakukamata kama
wale wa juu.

Uki- plot unapata Pyramid.
 
Tuanze hapo chini kisha tutaendelea:


View: https://youtu.be/ja_cL5te4Lw
 
Point KUU hii historia inahusiana vipi na tamko la askofu?!
 
Huwa sina haja ya kufungua na kusikilizamabandiko ya hizo 'clips' humu JF kwa sababu zangu maalum. Kwa hiyo usitegemee nivunje utaratibu huo leo. Mimi nasoma tu yaliyo andikwa.
Hapana neno wanaotaka kujua wataifungua clip.
 
Ulicho kiandika mimi nimekielewa vizuri sana though sio lazima nikubaliane na wewe kwenye maandishi yako kwasababu ya chumvi za kidini ambazo huaha unaweka kwenye mapishi yako. Swali langu bado lile lile tu; uhusiano wa historia hiyo ulioileta kuhusu Cathedral lile na hotuba ya baba askofu vikoje? Vinakutania wapi? Sijaona. Kwa mtazamo wangu, uzi wako ulitakiwa tu kua mpya usio na uhusiano na hotuba ya baba askofu
 
Nisamehe kijana wako Mzee wangu kwa kutumia lugha ya kuuzi hili jambo halitajirudia,japo mitizamo yako kwa kiasi kikubwa inaonekana kuegemea upande mmoja na kuwaona wa upande usio wako si kitu jambo ambalo linawakera watu wasio wa imani yako
 
Makwizi,
Mimi Kanisa Katoliki, Lindi limenikumbusha safari ya Julius Nyerere
Southern Province na yale aliyokutananayo huko.

Hili la kanisani ni moja.
Yapo mengi nitakutajia lingine.

Hili ni kisomo yaani dua aliyofanyiwa Nyerere na Sheikh Yusuf Badi.
baba askofu
Makwizi,
Mimi Kanisa Katoliki, Lindi limenikumbusha safari ya Julius Nyerere
Southern Province na yale aliyokutananayo huko.

Hili la kanisani ni moja.
Yapo mengi nitakutajia mawili.

Hili ni kisomo yaani dua aliyofanyiwa Nyerere na Sheikh Yusuf Badi.

''Lakini matukio mawili ya kumbukumbu kubwa yalikuwa katika safari
ya pili ya Nyerere alipozuru tena Jimbo la Kusini.

Kumbukumbu ya kwanza ilikuwa tawaswil aliyosomewa Nyerere na
Sheikh Yusuf Badi mwenyewe pamoja na Waislam aliowachagua yeye
sheikh mwenyewe maalum kwa hafla hiyo.

Wakachanganyika na masheikh wengine kutoka vijiji jirani na Lindi.

Kumbukumbu ya pili ni karamu iliyoandaliwa kwa heshima ya Nyerere
na Mussa Athumani Lukundu, kiongozi wa Dockworker’s Union.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
 
Naomba kufahamishwa mantiki ya andiko la ndugu Mohamed kulinganisha na alichosema Baba Askofu Wolfgang Pissa.
 
Najaribu kuunga dots kati ya hii historia ya mzee wangu na kisa cha askofu, connection inakuja kwa mbali na kukata.

1. Anataka kusema msaada wa wakristo usipuuzwe ?
2. Waislamu tumuunge mkono mkristo yoyote mwenye nia ya dhati kutukomboa, kuleta maendeleo kwenye taifa, kama ambavyo waislam walimuunga mkono mkristo.
3. Wakristo wasilete tabu, nchi uhuru ulipambaniwa na waislam, tumuache huyu hata kama hana sifa kisa muislam tu?
Na nyingine nyingi kibao..

Namba 2 ndio nzuri zaidi kama ndio lengo lake
 
Kwa hiyo ni kweli unapenda Tanzania iwe Islamic Republic, na tufuate Sharia Law ?
 
Najaribu kuunga dots kati ya hii historia ya mzee wangu na kisa cha askofu, connection inakuja kwa mbali na kukata.

1. Anataka kusema msaada wa wakristo usipuuzwe ?
2. Waislamu tumuunge mkono mkristo yoyote mwenye nia ya dhati kutukomboa, kuleta maendeleo kwenye taifa, kama ambavyo waislam walimuunga mkono mkristo.
3. Wakristo wasilete tabu, nchi uhuru ulipambaniwa na waislam, tumuache huyu hata kama hana sifa kisa muislam tu?
Na nyingine nyingi kibao..

Namba 2 ndio nzuri zaidi kama ndio lengo lake
 
Makaveli,
Hayo uliyosoma yanatoka katika kitabu cha Abdul Sykes na nilipoandika kitabu hicho kusudio langu lilikuwa kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Kwa hiyo ni kweli unapenda Tanzania iwe Islamic Republic, na tufuate Sharia Law ?
Che...
Umesoma popote mimezungumza kuhusu Islamic Republic?

Unajua kwa nini Nyerere alipewa nafasi ya Urais wa TAA 1953?

Wakati ule Abdul Sykes alikuwa Secretary na Act. President na ilikuwa imeshaamuliwa TANU iundwe mwaka 1954 na waliokuwa mbele katika mipango hiyo alikuwa Hamza Mwapachu na Abdul Sykes.

Abdul Sykes yeye alitaka sana Chief David Kidaha Makwaia achukue nafasi ya TAA President kisha waunde TANU na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru.

Hili halikuwa kwa kuwa Chief Kidaha hakuwa tayari kubeba jukumu hilo.

Hamza Mwapachu yeye alitaka Nyerere ndiye apewe nafasi hiyo na Abdul Sykes ahakikishe hili linafanikiwa.

Hiyo nafasi kwa uhakika ilikuwa achukue Abdul Sykes.

Hamza Mwapachu fikra yake ilikuwa kwa kuwa TAA imetawaliwa na Waislam na kwa kuwa TANU nia yake ni kupambana na Waingereza hadi waondoke, kazi hii ilihitaji umoja wa Watanganyika wote.

Ikiwa Abdul atakuwa President wa TAA picha itakayojengeka ni kuwa wanaotaka uhuru ni Waislam na ndiyo sababu wamejazana katika siasa.

Hamza Mwapachu akamwambia Abdul kuwa Nyerere anafaa zaidi kuwa President mbali na elimu yake kubwa bali ni Mkristo na atawafanya wale walio nje ya ulingo wa siasa kuingia ndani kwani Nyerere atakuwa alama ya umoja wa Watanganyika wote.

Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan Bin Ameir akamuunga mkono Nyerere.

Kilichobaki ni historia.
Leo wewe unazungumza serikali ya Kiislam?

Soma kitabu cha Abdul Sykes kuns mengi.
 
Hapa leo ndio nimegundua kwanini pamoja kwamba waislam walikuwa wengi huko tanu ila wakampa nafasi Nyerere, walifanya vyema sana,
Basi hata sasa sisi waislam tusione tabu kumuunga mkono mkristo kwenye kuichukua nchi na kuleta maendeleo, sisi hatuna udini, maana kama muislam mwenzetu anatuamgusha ya nini tumgande, kwanza hana maslahi na waislam na uislamu wenyewe kiujumla, lakini kubwa zaidi ni kuwa hii nchi sio ya kidini hivyo yoyote ambae anaweza kutupa maendeleo badi anatufaa sana kwenda pamoja na sisi, kama vile waislam wa tanu walipomuona nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…