BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
IAM DEEPLY CONCERNED.
YAWEZEKANA TUKO KATIKA JANGA LA KISHERIA – UHALISIA WA KUTISHA KIDEMOKRASIA !?
Hili linaweza kuwa moja ya zuio la kipekee kabisa, la upande mmoja, kuwahi kutolewa katika historia ya nchi zinazofuata mfumo wa Common Law.
Kwa kawaida, zuio (injunction) hutolewa kwa lengo la kulinda hali iliyopo (status quo) ili kuzuia madhara zaidi mpaka haki itakaposikilizwa kikamilifu.
Lakini zuio linalotumika hapa linaonekana si tu linaharibu hali iliyopo, bali linafuta kabisa uhalali, uwepo, na utambulisho wa taasisi halali ya kisiasa.
Ni vema tukajiuliza: Mgawo wa Matumizi ya Zanzibar unahusuje mkutano wa wanachama wa BUSOKELO, TANDAHIMBA, LONGIDO au SERENGETI?
Je siyo kweli kwamba Jimbo linapimwa kwa msingi wa mgawanyo wa ruzuku ya kitaifa, si kwa mipaka ya hisia au muktadha wa kisiasa.
Je siyo sahiji kwamba kuzuia au kuingilia vikao halali vya wanachama wa chama cha siasa kwa kutumia hoja ya mgawanyo wa matumizi ya Zanzibar na Tanganyika ni sawa na kujaribu kueneza mihemko ya kisiasa kwa kutumia misuli ya kimahakama.
Je siyo jambo la kushangaza zaidi kwamba kesi inayowasilishwa kwa HATI YA DHARURA ambayo kisheria hulenga hatua za haraka kwa madhumuni ya ulinzi wa haki nageuzwa kuwa jukwaa la sarakasi hadi kuhitaji kuandikwa “ufafanuzi wa kina” kuhusu zuio husika?
Je, huu muda wa kuandika maelezo ya kina umetoka wapi kama kweli kulikuwa na dharura ya kweli? Je udharula iliisha baada ya amri kutolewa kwa Upande mmoja?
Je yawezekana tuko katika janga la Mkwamo wa kisheria na uminywaji wa demokrasia na haki za kikatiba kupitia Mahakama?
Unawezaje kutoa amri ya kusimamisha shughuli zote za chama cha siasa wakati wa uchaguzi bila kusimamisha shughuli zinazohusiana na uchaguzi?
Je, kuna jaribio la kihistoria la kupindua kanuni za haki, kutumia mahakama kama chombo cha kisiasa, na kuua uhuru wa vyama vya siasa?
NAULIZA NA WEWE UJIULIZE ILI WAULIZANE.
Pia soma : Wakili Marijani: Waliozuiwa CHADEMA hawatakiwi kuzungumza na Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya vyama