Nimeona alichozungumza makonda Jana, na hiki ndicho kinachoakisi mawazo ya watawala wetu wengi..
Nini kosa la Pierre "Konki liquid", Amevunja Sheria gani ya nchi?.
Makonda hajui kwamba Pierre ni comedian na anaitumia Sanaa yake kupitia pombe?, Kati ya Pierre na msiba ni nani ni mtu wa hovyo kwa taifa hili?
Makonda, umemkosea Pierre sijui alijisikiaje konki liquid baada ya kudhalilishwa kule na yeye akiwepo, pamoja na kwamba una cheo kumzidi lakini hukupaswa kumdhalilisha vile, ungepaswa kutumia busara na hekima za kiuongozi., Sidhani Kama vituko na media kumtangaza Pierre ndivyo vinavyosababisha kuporomoka kwa maadili na kujenga kizazi Cha hovyo hapa nchini, sio kweli tusimsingizie Pierre ambae anahangaika na ubunifu wake wa kutumia pombe kuutafta mkate wake.
Walikuwepo wasanii akina John walker, utofauti wa Hawa wawili mmoja ni msanii wa music na mwingine comedian.., Kaka makonda unafanya kazi nzuri ila unakosa hekima na busara., Kwa kauli yako ya Jana kampuni nyingi zitasitisha mkataba na huyu bwana unaeenda kumrudisha kwenye umaskini .. hakika hii ni dhambi, huyu hajaiba, hajakwepa kodi na Wala sio mla rushwa, hakustahili udhalilishaji uliomfanyia.
Anyway nyie ndo Aina ya Viongozi mnaotupeleka Tanzania ya viwanda na uchumi wa Kati...Pole kwako konki liquid kwa hili najua wameshakupoteza tayari, ila mungu yupo anaweza kukutoa kivingine.. hakuna ridhiki inayozimwa na binadamu