Alichofanyiwa Mrisho Ngassa ni uhuni, TFF, TPLB mnawajibika

Alichofanyiwa Mrisho Ngassa ni uhuni, TFF, TPLB mnawajibika

Ngasa ana hela bado ana nyumba za biashara mwanza na dar anakosaje elfu kumi ya kiingilio,kongole kwa walinzi kazi nzuri wamefanya.
Alipe kiingilio kama wengine
 
Huyu boya alikataa kwenda Sudan acha umaskini umtese
 
Kwanini asilipe...au akitaka bure afuate utaratibu......waafrika tukishakuwa mastaa yaa it's like you have a tick to do whatever......huo Ni ujinga

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni mwananchi, lakini pia mshabiki wa Mrisho Khalfan Ngasa. Sijajua chanzo hasa cha huo mzozo!
Ila kama ni kweli mchezaji wetu Mrisho Ngasa alitaka kuingia uwanjani kuangalia mpira, pasipo kufuata utaratibu; mfano kuwa na tiketi kama mashabiki wengine, au kitambulisho maalum! nadhani hapo atakuwa amekosea.

Siamini kama Mrisho Ngasa ni mchezaji wa kukosa hela ya kiingilio. Na kama alitaka kuingia uwanjani kupitia jina/umaarufu wake, hilo nalo ni tatizo. Maana kila mtu akiamua kutumia njia hiyo, nchi haiwezi kusonga mbele.
 
Nimeona mahali kwamba eti nyota wa zamani wa Yanga, Azam, Simba, Ndanda, Mbeya City na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mrisho Khalfani Ngassa, juzi alizuiwa kuingia uwanjani kushuhudia mechi ya Ligi Kuu.

Ngassa alizuiwa na walinzi wa milangoni maarufu Steward, ambao walimfanyia kitendo cha udhalilishaji sana, jambo ambalo nadhani linapaswa kupigiwa kelele, vinginevyo, litatuletea matatizo makubwa hapo baadaye likiota mizizi.

Kibaya zaidi, wakati wa kumzuia haukutumika hata utu, uungwana wala ustaarabu. Ilikuwa ni nguvu zaidi, kukabwa, kusukumwa na naneno ya kashifa, huo ukiwa ni udhalilishaji wa hali ya juu sana.

Alizuiwa kuingia na walinzi wa getini, waliodai wameelekezwa kusimamia mapato, ambayo yamekuwa yakishuka siku hadi siku, hivyo eti ni lazima mapato hayo ya getini yasimamiwe kikamilifu ili hela ipatikane kwa wingi.

Hivyo, Ngassa ambaye amelitumikia taifa hili kwa moyo wake wote, akiwa ndiye mfungaji kinara wa muda wote kwenye kikosi cha Stars, aliambiwa ili aingie, anatakiwa awe na tiketi au kitambulisho maalumu cha kuingilia uwanjani.

Kwa kiasi fulani walikuwa sahihi madai yao, ila walikosa hekima, busara na utu, walitumia nguvu zaidi kuliko akili, kwani mbali na kumfahamu, hawakutaka japo sekunde moja kumsikiliza kwa nini yuko hapo, walichokifanya ni kumkaba, kumvuta, kumsukumiza na maneno kibao ya kashifa!

Kwa mwili wake kusukumizwa na wale jamaa, unadhani hali ilikuaje, piga picha upate uhalisia wake, ni hatari sana ilikuwa, asikwambie mtu! Kwa kawaida, Shirikisho la Soka nchini TFF au Bodi ya Ligi TPLB hutoa vitambulisho maalumu vya kuingilia uwanjani kwa wadau maalumu pamoja na viongozi wote wa klabu za Ligi Kuu.

Hao walinzi wa getini na viongozi wa timu husika kama walivyodai, wanalitambua hilo, ingawa ni mara chache vitambulisho hivyo vinatolewa kwa wachezaji wa zamani.

Kuna haja ya TFF, TPLB na Vilabu kuwa na utaratibu maalum kwa wachezaji wetu wa zamani. Mtu kama Mrisho hapaswi kuusotea mpira wetu akitaka kuja kiwanjani. Amewahi kutupa furaha na heshima kwa nyakati tofauti tofauti kupitia mpira huu huu, inakuwaje leo akija kiwanjani anapata shida kuingia?

Wako mastaa wengi wa zamani ambao wamekuwa wakikutana na adha hii ya kidhalilishaji.
Kuna wachezaji wengi wamecheza miaka ya nyuma kwenye klabu zao pamoja na timu zao za taifa. Nchi zetu zina wachezaji waliostaafu soka kwa sababu tofauti.

Kuna sabu nyingi mno za kibinafsi, majeraha, umri, kukosana na viongozi, ukosefu wa fedha za kujikimu kimaisha kutokana na fedha ambazo wanalipwa kuwa ndogo na kadhalika. Hata hivyo, wachezaji wakishastaafu tu huwa hawaheshimiwi na baadhi ya viongozi wa soka kwa sababu zisizoepukika.

Hii ndiyo sababu viongozi wengi wanaendesha soka wanavyotaka, kisa na maana ni kuwa wachezaji hawana nguvu za kifedha kupingana nao.
Wachezaji wanapojaribu kuingia katika uendeshaji wa soka wanafungiwa.

Ni mapendekezo yangu kuwa, soka lingeachwa liendelezwe na wachezaji, hakuna siku mwanariadha ama mwanandondi atakuwa mkuu wa soka, ama mwanasoka awe mkuu wa masumbwi na kadhalika.

Shughuli hazitaweza kuendeshwa vizuri, atakuwa hana ufahamu wa kutosha wa mchezo huo unavyoendeshwa.
Hakuna siku rubani wa ndege atakuwa nahodha wa meli, daktari wa kutibu binadamu hawezi kuwa sawia na daktari wa kutibu mifugo.

Ni mengi sana ambayo mchezaji hupitia, ikifika wakati soka letu likaanza kuendeshwa na waliobobea ndipo tutaanza kuona mabadiliko halisi.
Ni aibu mchezaji unasukumwa na walinzi wa milangoni bila kuwa na heshima.

Hawa ni mastaa wa hapo awali, bila wao soka letu lisingefika lilipo sasa.
jamani mambo mengie bwana hivi ngasa nae alishindwa kua na kiasi cha pesa alipe tu aingie,mambo mengine jamani tuyaepuke
 
Hilo lapaswa kuwa somo kwa wachezaji woote wapuuuzi, wanaocheza mpira huku wakiendekeza ushabiki kwa timu zao, badala wacheze mpira kama ajira watengeneze kipato wao wanacheza kiushabiki, matokeo wastaaf tuu kipato hawana na club walizokuwa wakizichezea kiushabiki haziwathamini tena
Mfano makubwa ni huyu Ngasa,
Kwa herufi kubwa ALIPE KIINGILIO AKILI IMKAE SAWA NA LIWE FUNDISHO KWA WACHEZAJI WA SASAAA
 
Utaratibu upi, kuna Watu wanapewa Vitamburisho na kuingia bure wakiwa hawajafanya jambo lolote la Maana kwenye Mpira wetu.
Kwani uyo ngasa ili kuaje aende bila utambulisho na anajua una takiwa
 
Bongo mambwiga ni wengi,wakati hayo yanatokea hakukuwa na mashabiki kweli?
Kama kwenye level ndogo kama hii tunashindwa kuchukua hatua sishangai viongozi wa kisiasa kutufanyia utumbo na kupeta
Sisi wabongo tutanyasisika Hadi siku ya mwisho. Mamtu mengi ni zero brain.
 
Azipate kwako wewe unayelialia! Tunapenda vya bure mno
vya bure mwisho wake ndo huo sasa mabaunsa wa getini wanakubeba tupa kule alafu unakuja kulia lia hapa nani akusaidie sasa.lipa kiingilio akuna huruma pale mlangoni.
 
vya bure mwisho wake ndo huo sasa mabaunsa wa getini wanakubeba tupa kule alafu unakuja kulia lia hapa nani akusaidie sasa.lipa kiingilio akuna huruma pale mlangoni.
Kuna kitu huwa kinaniuma ni mentality ya sie! ati hiki kitu nilifanya mimi enzi hizo, tatizo unasahau ulipofanya ulipewa mshahara na mkamalizana na mwajiri. Unataka kuendelea kukamua kama ng'ombe? Mrisho wakati akicheza alikuwa analipwa. Baada ya kutoka uwanjani anakuwa mtazamaji, hivyo lazima alipe kiingilio ili anayecheza sasa apate mshahara. Ukitaka akina Kajole, Sunday Manara, Sunday Juma, Athumani Chama, Zamoyoni Mogella, Dilunga etc wote waingie bure mapato yatatoka wapi?
 
Walinzi wamefanya, wakulaumiwa ni Yanga, na iwe funzo pia kwa vilabu vingine vyote. Watoe at lease ticket za bure za home matches zote kwa legends wao kila msimu ukianza.
 
Mimi ni mwananchi, lakini pia mshabiki wa Mrisho Khalfan Ngasa. Sijajua chanzo hasa cha huo mzozo!
Ila kama ni kweli mchezaji wetu Mrisho Ngasa alitaka kuingia uwanjani kuangalia mpira, pasipo kufuata utaratibu; mfano kuwa na tiketi kama mashabiki wengine, au kitambulisho maalum! nadhani hapo atakuwa amekosea.

Siamini kama Mrisho Ngasa ni mchezaji wa kukosa hela ya kiingilio. Na kama alitaka kuingia uwanjani kupitia jina/umaarufu wake, hilo nalo ni tatizo. Maana kila mtu akiamua kutumia njia hiyo, nchi haiwezi kusonga mbele.
Dah! Kumbe kuna wakati huwa unakuwa na akili?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Uwanja wetu kuna upuuzi mwingi sana, ndiyo maana unaweza kuwa na ticket ya eneo fulani unafika hapo unakuta pamejaa na kwasababu kiwanja chetu hakina namba unaishia kukaa kwenye ngazi,moja ya upuuzi ni hawa wachezaji wa zamani kuingia free bila kadi wala eneo maalum wao wanaenda kukaa popote.Mfano wameingia 20 hiyo ni tatizo tayari.......wengi naona wanalaumu kuona Ngasa hajaheshimiwa ila kama vipi wapewe kadi maalum na eneo lao, tofauti na hapo ni fujo
 
Hakuwa na hela ya kununua tiketi? Utaratibu lazima ufuatwe.
 
Hivi Karia amewahi kucheza soka?timu ipi?
 
Back
Top Bottom