Zitto alitengeneza mtandao wake wa siri unaoelezwa hapa. Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo huu hapa
Lengo la mtandao huo ni Zitto KUWA MWENYEKITI WA CHADEMA.
Lengo hilo si baya, lakini namna ya kulifikia, ilikuwa ni kwa gharama yoyote hata kama CHAMA kitavurugika.
Zitto alipata support kubwa toka CCM na hata hapa JF CHAMVIGA, ZeMarcopolo, FaizaFoxy, Chabruma, Simiyu Yetu, Shelui, Mwigulu Nchemba, Taswira, MwanaDiwani, Ritz, TandaleOne n.k. walikuwa wanashambulia CHADEMA huku wakimlinda Zitto kwa nguvu zao zote. B
aadhi ya dhihaka waliyokuwa wakiitupia Chadema.
- Chadema hawana ubavu wa kumgusa Zitto, wakimgusa tu wamekwisha!
- Chadema wanawashughulikia tu vidagaa, hebu kama wana ujasiri wamguse Zitto!
- Viongozi wa Chadema hawana ubavu wa kumfukuza Zitto au Shibuda.
- Zitto ndiye nguzo ndani ya Chadema wakimgusa tu chama kinasambaratika.
- Vijana wengi wanaokiunga mkono Chadema ni kwa sababu ya Zitto.
- Sasa hawa Chadema kama hawampendi Zitto si wamfukuze waone kitakachofuata.
- Umaarufu wa Chadema umetokana na jitihada za Zitto.
- Mbowe na Slaa si chochote, si lolote kwa kijana Zitto.
- Siku Zitto akiondoka Chadema tu na Chadema inakufa.
- Zitto ni zaidi ya Chadema.
Sasa Zitto kavuliwa uongozi CHADEMA, na ndani ya siku 14 atafukuzwa CHADEMA.
Zitto akihamia CCM atasaidia sana kuimarisha CCM Kigoma, ambapo kati ya majimbo 8 CCM iliambulia majimbo matatu tu tena kwa mbinde sana. Bila shaka CCM watampokea kwa kuwa wanapenda kurudisha viti hivyo vitano mkoani Kigoma.
Zitto ni kiongozi mwenye karama kubwa na mvuto kwa jamii, na akihamia CCM atapenda, kama ambavyo alipenda akiwa CHADEMA, karama hiyo yake aitumie kufikia kwenye nafasi za UONGOZI WA JUU KABISA. Uenyekiti wa CCM.
Wanaounga mkono CCM humu jamvini
CHAMVIGA, ZeMarcopolo, FaizaFoxy, Chabruma, Simiyu Yetu, Shelui, Mwigulu Nchemba,[URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=114003"]Taswira[/URL], [B][URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=132973"]MwanaDiwani[/URL], [B][URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=34266"]Ritz[/URL], [B][URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=25971"]TandaleOne[/URL] [/B][/B][/B]waliamini kuwa Zitto alikuwa sahihi kufanya aliyoyafanya kwa namna alivyofanya akiwa CHADEMA.
Bila shaka watampa ushirikiano kuyafanya hayo hayo, ndani ya CCM kwa kutumia namna hizo hizo.
CCM,
[B][B][B] [B][URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=1681"]Zitto[/URL] [/B][/B][/B][/B]yuko mlangoni anabisha hodi, anataka kuingia, mkaribisheni. Lakini hataki kufikia sebuleni tu, anataka mpaka ndani kabisa, kwenye KITI cha Mwenyekiti wa CCM. Anaomba mumpe ushirikiano na mvumilie mbinu zote atakazotumia kufikia azma yake.