Alichofanyiwa Zitto ndani ya CHADEMA: Akili ndogo inatawala akili kubwa

Hata kama ni akili ndogo kutawala akili kubwa ndo asifuate taratibu na katiba ya chama chake? Acha hizo bwana Mwigulu.
 
leo umekuwa ni mtetezi wa zitto,mambo ya ajabu haya.....na leo una nukuu kauli ambazo huwa zinawachoma hsa hiyo ya msigwa....tafuteni wengine wa kuwatumia....mwigulu nakuchukia sana.....
 
Mwigulu ni vema mkajifunza kufanya maamuz magumu kama walivyofanya CDM. Tatizo letu Tanzania tumefika hapa kwa kukosa watu wanaoweza kufanya maamuz mazito yaliyo sahihi. Binafsi nawapongeza CDM kwa kuthubutu. Hyo ndo kamati tunayoamin wakipewa nchi, likija swala la kuwafunga na kuwafilisi mafisadi wataweza. sio kama hao akina pinda wanaosema serikali inaogopa kuwachukulia hatua eti kisa wana nguvu ya hela. kuliko Serikali? kituko. Nasubiri kwa hamu utetez wao Zito, kitila, na Mwigamba.
 

mwigulu leo unamtetea hasimu wako dr. Mkumbo?zitto sishangai!hivi wamekueleza wamefanya makosa gani?na je hayo makosa yanastahili adhabu gani hata kwa ccm?mpango wenu umefaili wachukueni sasa muwape uongozi ili muwatumie kama resource zenu.
 

Hivi kama Kamati Kuu ingemfukuza Dr Slaa hizi hudhuni na matanga yangekuwepo Lumumba? Yaani hawa jamaa wameshindwa kabisa kuficha hisia zao za maumivu waliyopata kwa mission yao ku backfire. Tena kwa taarifa yao Mwigulu ndio kaharibu kabisa,maana ndani ya siku hizo 14 pengine Zitto angeweza kuandika barua nzuri na kuomba radhi na kibinadamu angeweza kufikiriwa kwa kukumbuka walao kile kidogo alichofanya lakini sasa Mwigulu kadhibitisha kuwa ni mtu wao hivyo itakuwa ngumu.
Niseme tuu kwa dhati ya moyo wangu,POLENI SANA CCM KWA MASAHIBU YALIYOWAPATA KWA MTU WENU KUVULIWA MADARAKA KABLA HAJAKAMILISHA KAZI MLIYOMLIPA.
 

mtuma pepo huwa anakuwa furahani pindi pepo mchafu anapokuwa kule alikompeleka lakini pindi pepo anapotolewa na kurudishwa kwao hali huwa mbaya zaidi ya kule alikotumwa
 
Nalo hili limetokea kwnye chemba lipi tena?
 

Prof baregu amesema CDM nikampuni ya Mtei na Mbowe.Kama walikua wana vielelezo vya kutosha na tuhuma zinazo wakabili kwanini wasinge vionesha mapema kabla ya kipindi hiki cha uchaguzi wa CDM?
huu ni ushaidi una onesha mbowe na ma-vilaza wa div0, wenzake hawataki kutoka madalakani

1.walimpiga mwenykiti wa arusha(Mwigamba) kwa madai ya kuvujisha siri kwenye huu mtandao.(ila madai ya mwenyekiti yalikua sahihi kwani jamaa walibadilisha katiba kinyemela.)
2.kwa kua zitto ni zaidi ya CDM na mwenyekiti mbowe akaona amvue uanachama ili asigombee nae na kumpa visingizio visivyo na msingi kwa wakati huu .
OMBI LANGU KWA MBOWE PLEASE USIJE UKAFANYA KWA ZITTO KAMA KWA CHACHA WANGWE .ULIMVUA UANACHAMA PILI UKATUMA JASUSI WAKAMUUA .SASA MAJASUSI WALIO LETA ILE RIPOTI FEKI KWA ZITTO USIJE UKAWA TUMIA TENA KUMMALIZA ZITTO
 

Nimeamini nchi inatawaliwa na vilaza, mwigulu wewe cheo chako hakiruhusu kuongea huu uozo! mwachie mtela, shonza na nape. Ama kweli nyani haoni kundule, hii ndo akili ndogo kabisaaaaaaaa!
 
Msaliti ni msaliti tu. ZZK ni msaliti ndani ya CDM kwa sababu ana akili ndogo. Akili ndogo kwa maana kwamba anadhani yeye ndio kila kitu na anadhani bila yeye CDM haipo. Hizo ni viashiria vya mtu kuwa na akili ndogo. Sisi wanachama na wapenzi wa cdm tunaamini kuwa maamuzi ya kamati kuu ni sahihi na yamekuja muda muafaka. Zzk hawezi kutufanya watu wote hatuna akili isipo kuwa yeye tu. Kimsingi, cha kumfahamisha ni kuwa hatapata umaarufu wowote akiwa nje ya CDM. Jeuri lote hili alipata tokana na hela za mijizi ccm, ambayo hayana huruma kwa mateso wanayopata watanzania maskini. Naunga mkono hoja, wasaliti wote wasipewe nafasi hata sentimita moja.

A luta continua
 
Inawezekana CHADEMA wamekosea kufanya maamuzi hayo. Lakini ukijipa muda wa kutafakari utagundua kuwa ni UTHUBUTU wa hali ya juu katika kushughulikia kansa ya unafiki kama kweli wamepatia!!! Nani atathubutu tena kuwachezea? Kama kiongozi/viongozi wao wa ngazi hizo wamethubutu kuwaondoa katika nyadhifa zao nani ataachwa akichezee chama? Ni uthubutu, hata CCM naamini wanatamani lakini hawataweza kwa kuwa haujawahi kuwa utamaduni wao baada ya Nyerere kuwaachia chama na nchi!!!
 
huyu Mwigulu ndo walicheza mchezo wa kuongea asubuhi star tv yeye na zitto halafu zitto akala kona ili mwigulu achafue chama vizuri.....
 


Tehtehteheee hata kipima joto kina digirii tena mia na kinakaa kwapani yashinda hao ulowataja wana vidigirii vikizidi vitatu tu. Embu tuache na chama chetu chenye uthubutu
 
STOP YOUR FOOLISHNESS.....

Wewe unayejiita BANGOO? nini kipimo cha akili ndogo kwako maana neno hilo ni Subjective! Lakini kumbuka Rais wa Jamhuri ni mwakikishi wa watanzania wote uwe ulimpigia kura au hukumpigia kura. Nadhani sio kila wakati wa kumkashifu na kumuongelea maneno ya dharau kiasi hicho kwani yanadhihirisha kuwa wewe ndio miongoni mwa AKILI NDOGO zinazoelezwa na Mh. Mwigulu Nchemba. Jibu hoja na sio kusema kila neno linalokuja mdomoni ili na wewe tu uwe umejibu post... Kuwa Professor sio KIPIMO CHA AKILI KUBWA pia..
CHADEMA ni chama kinachoongoza nchini kwa kuwa na maamuzi ya kukurupuka sio tu kwa wanachama, wapenzi, mashabiki ila hata wabunge wake na viongozi wa kamati kuu.. Kinaonekana ni chama chenye misimamo lakini swali la msingi ni wanasimamia nini? Suala la ukanda na ukabila ndani ya chama ni changamoto ya siku nyingi inayowaumiza vichwa hata viongozi waandamizi wa chama hicho hasa yanapotokea mambo kama haya, lakini je wasifanye maamuzi magumu ya kuokoa chama kwa hofu hiyo? Ni swali jepesi lenye jibu Hapana kwani chama kitabaki watu watapita.. Kingine lazima wajifunze POLITICAL SHOCK ABSORPTION ili kulinda watu muhimu ndani ya chama pasipo kupoteza wanachama wachache walionao na mashabiki lukuki walionao pia..
Niliwahi kusema CHADEMA inahitaji muda mzuri wa kujipanga na kujenga chama ila mashabiki wa chadema kama walivyo-viongozi wao ni wakurupukaji wakasema sio kweli ila naimani sasa ukweli umeanza kujidhihirisha la sivyo suala la kuchukua dola litakuwa ni ndoto ya daima kwani kati ya waliobaki pia wamo wanaompenda na kumkubali kaka na kipenzi cha vijana wengi Mh. Zitto Zuberi Kabwe!
Kwako Mh. Mwigulu waswahili husema "ajidhaniaye amesimama aangalie asianguke" hivyo ni vyema nyinyi pia kuwa makini kwa kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama huku mkikemea hadharani makundi yanayozuka kwa kasi ndani ya chama kwa sasa ili yasije kutokea haya yaliyotokea kwa CHADEMA..
Viva Tanzania...... Sauti ya Jukwaa la Vijana Kanda ya Kati
 
Sidhani kama wamefukuzwa nakushauri Mwiguru maswala ya vyama waachie wenyewe kwani hata CCM tunafukuzana tangu izaliwe Tanzania washefukuzwa na kupotezwa viongozi wengi tu. Leo CDM imekuwa nongwa?
 
Sidhani kama wamefukuzwa nakushauri Mwiguru maswala ya vyama waachie wenyewe kwani hata CCM tunafukuzana tangu izaliwe Tanzania washefukuzwa na kupotezwa viongozi wengi tu. Leo CDM imekuwa nongwa?
Halafu akili siyo elimu uliyonayo mbona tunawaona wasomi waliobobea na uprofesori na udaktari wao wakishindwa kuongoza hata idara, wizara au taasisi, ingekuwa hivyo sidhani kama CCM kunabaadhi ya watu tungewapa uongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…