Alichohoji Profesa Muhongo ni kama bei ya umeme itakuwa nafuu kuanzia siku ya kwanza au baada ya kurudisha gharama za uwekezaji?

Gas wa weke kwenye mitungi wakauze nje ya nchi serikali ipate kodi ya Dollari.

Gas inayochakatwa hadi sasa hapa nchini sio ya mitungi. Ili iwezekane hiyo ya mitungi ni lazima kiwanda cha LNG kijengwe. Na hicho kiwanda cha LNG ndio hicho kimejaa porojo.
 
wapinzani ili iweje. Yeye alikuwa na kipaza sauti na sisi tuna masikio. Kwahiyo tulikuwa tunapa dozi moja kwenda nyingine
 
Ukitaka kujua dunia iko mwisho ni pale ukutapo "wapumbavu wakitoa hoja dhidi ya mweledi na wakashangiliwa..."
 
Ndugu zangu, kwa kipindi kirefu sana tumekuwa tunawaachia wanasiasa watoe ufafanuzi hata kwa mambo ambayo kitaaluma na kiuzoefu hawana weledi wa kutosha.
Kupitia jukwaa hili naomba nitoe wito kwa wanajamvi hili tuwe tayari kuelimisha wengine yanapojitokeza masuala mtambuka kama hili la Power Generation kwa kutumia njia mbalimbali kama maji, mafuta, jua, nk. Kwa kufanya hivi tutapunguza malumbano yasiyo na tija na upotoshaji ambao wanasiasa wanaweza wasijali as long as upotoshaji huo ni neema kwa upande wao.
Naandaa maelezo ya kitaalamu yahusuyo Electrical Power Generation, Transmission, Distribution and Utilization. Sambamba na hilo nitagusia kinachodetermine bei ya umeme kwa watumiaji, njia sahihi za kufanya makadirio ya mahitaji ya mbeleni, nk.
 
Yule professor ni wa hovyo sana na hana aibu, aliwahi kudhihaki wawekezaji wa ndani kua wana mitaji ya pipi hawawezi kuwekeza kwenye gas. Dunia nzima ina encourage wawekezaji wa ndani yeye anatukana

Wasomi wa nchi hii wengi ni vilaza na wamekariri madesa, hawana akili. Ndio maana akina msukuma wapo huru, wameona mapungufu
 
Ulisikiliza vizuri mchango wa Muhongo?

Ukiacha upotoshaji unaofanywa,Muhongo alitoa mchango mzuri sana hususani katika suala la madini,halafu akazungumzia kwa ufupi sana suala la hydropower,wala hakuponda mradi wa JNHP,alichosema hydropower,kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,haziaminiki na uwekezaji wake ni mkubwa mno ukilinganisha na gesi.
 
Niliona mahali kuwa trillion almost 3 hivi zingewezesha kupata MW nyingi zaidi ya bwawa la Nyerere. Kurudisha Trilliln 3 ni karibu zaidi kuliko kurudisha trillion 10 za bwawa la Nyerere hivyo kimahesabu wananchi wangepata nafuu ya umeme mapema zaidi kwa chanzo cha gesi kuliko hiko cha bwawa la Nyerere.

Kwa mfano labda kurudisha gharama ya uwekezaji kwa bwawa la Nyerere yaweza kuwa miaka 15 lakini kwa chanzo cha gesi pengine ingekuwa miaka 5 na huku ukiwa umepata MW nyingi zaidi ya zile za bwawa.
 
Ukitaka kujua dunia iko mwisho ni pale ukutapo "wapumbavu wakitoa hoja dhidi ya mweledi na wakashangiliwa..."
Duu!

Umetema madini ya hatari! Mungu akubariki.

Jambo la kusikitisha ni,tangu walipojaza hao darasa la saba bungeni,wajinga wameongezeka sana nchi hii. Hivyo,mwerevu akitoa hoja hawaelewi kabisa!

Halafu,jambo la kushangaza,hao darasa la saba serikali ya Magufuli iliwaomdoa serikali hata kwenye kazi za chini kabisa kama umesenja na udereva. Lakini wakajazwa bungeni,ili washabikie hoja za kijinga za kubeza mawazo ya wenye akili!
 
Muhongo ana bahati mbaya sana na siasa za CCM na Tanzania kwa Ujumla, anachosahau ni kwamba Waafrika ni Wanafiki, hawapendi kuambiwa ukweli ila wanapenda sifa za kijinga na kipumbavu, hao la saba c sifaham kama wanajua lolote kuhusu umeme ama wamewahi fanya tafiti yoyote lkn ndio Think Tanker wetu yaani wanaonekana na uwezo mpaka wa ku mu outsmart Mtafiti na Mbobezi, haya twende na la saba tutafika tu
 
Yaani ni mambo ya ajabu kabisa!

Halafu spika anashabikia huo ujinga! Wasiojua abc yoyote katika sekta ya nishati kumdhalilisha mtaalamu na mtafiti ambaye ana current information za industry!
 
Hilo bwawa si linajengwa kwa fedha za ndani? Ikiwa ni hivyo basi from day 1 bei yake inaweza kuwa ndogo na nafuu kama inavyotarajiwa halafu faida kubwa itapatikana kutokana na jinsi ambavyo unafuu wa hiyo bei ya umeme itakavyochochea maendeleo na uwekezaji zaidi ktk sekta nyingine. Na hapa naamini ndio dhana ya kutumia fedha za ndani ilipo.
 
Prof. Muhongo ametoa hoja kisomi achana na wengine wa darasa la saba wanaopayuka hovyo.
 
Bado ni pumba tu.. kwani umewahi sikia panakauka maji kule?

Yani mradi ulipofikia sahivi ni wa kutoa hoja kama hiyo kweli??..


Kuhusu mabadikiko ya hali ya hewa si angeshauri misitu iliyozunguka eneo husika ilindwe??..

Kwanini alete hoja ya gesi huku akijua kwenye gesi hatutopata kitu?..
 
Hivi hata umeweza kupata 'mantiki' ya swali lake ? Umeelewa msingi wa hoja yake ?
 
Kuna yule dogo aliyeitwa njuka na mdee, kuna huyo kibajaji, kuna msukuma,, huku speaker na pm wakifurahia ,,lakini maneno yao yanambeza mama yetu moja kwa moja.
Mama achukue hatua za haraka,, la sivyo wataendelea kumtaka afate nyayo za jpm.
Japo moja ya nyaoyo za jpm ni kuwananga watangulizi wake. Ila naona kuna vijitu vinataka kumcontroll mama. Avichape hivi ili wengine washike adabu zao.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu..hiyoo mantik wewe umeipatia wapi? Wakat yeye alisema waz waz kabisaa huo upupu wake..tena akaongezea na hili..kuwa umeme wa maji umepitwa na wakat na haufai..wakat norway ndo wanautumia huo umeme had leo..USA wanajenga mabwawa kila siku..ethiopia wanajenga pia..
We mbatizaji nawe umeshalishwa poda nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…