Kuna wanasiasa naona wanatumika kuwa kama mashionari..
Hiyo Phd ya Muhongo Mimi sina lakini nina mashaka nayo kwakweli..
Ipo hivi gharama za mwanzo za ujenzi wa mradi umeme wa maji siku zote Huwa juu kutokana na kuchukua eneo kubwa tofauti na mradi wa umeme wa gesi(Yani kwenye ujenzi)..
Lakini tukija kwenye gharama za uendeshaji zinakuwa ni kama sifuri Yani kwenye hesabu Huwa tunasema (the value can be neglected kutokana na faida kuwa kubwa kuliko gharama za uendeshaji) hapa ndipo tunapo pata faida yake, tukumbuke mvua hailipiwi ni bure kabisa na vilevile umeme wa maji ni moja ya vyanzo umeme ambavyo havichafui mazingira kwa kuongeza gesi ya ukaa(Carbondioxide) vilevile hudumu miaka mingi mfano tuangalie bwawa la mtera..
Sasa tukija kwenye umeme wa gesi.. bila hata kuambiwa wote tunajua gharama ya gesi ilivyo juu ukiona gesi unaungua ujue ni pesa tunaunguza.. na hapo tukumbuke kwenye mradi wa gesi tulishapigwa nchi yetu haita faida pakubwa kwenye uuzwaji wa hiyo gesi kuzalisha umeme..
Sasa hapo tujiulize hao wanaopinga huu mradi wapo kwa maslahi ya nani..??
Mi nadhani wataanzania pamoja na Hayati kuwa na mapungufu yake.. alitufungua akili lakini pia kila maamuzi aliyofanya yalikiwa ni kwaajili ya hii nchi yetu tuwe makini sana.
View attachment 1751169