Alichokifanya Gerson Msigwa, New York alipaswa akifanye Siku Zote Ikulu. Zuhura Yunus Asiwe Bubu!

Paskali, professional na siasa haviendani, yaani hata msigwa ni bahati tu kufanya hivyo akiwa hapo America ila akiwa hapa ikulu ni ngumu sana.

Kwa dadaenu zuhura pia ni vigumu kufanya hicho unachotaka, bahati mbaya upo nje ya field ila ukibahatika kuingia and in one week tu ahahahaa, sijui kama utaandika uliyokutana nayo huko.

Kila ofisi ina utaratibu wake ila hatuhufahamu kwa sababu tupo kwa nje.
Nakubalina na wewe, maana nikiwa uwanjani nangalia mpira, mipira ya pasi nzuri za kuelekezwa golini najiona ningekuwa mimi ningepiga bonge la shuti na kufuga goli, huku nikipiga mguu hewani!.

Hata wife aki ni drive, nakosa amani sometimes nakanyaga miguu kama kukanyaga break au natamani kukunja staring, hivyo kuna vitu ni easier said than done ukiwa nje!.
P
 
Tungekuwa tunatumia hizi bidii kuboresha utalii at ground level na kuitangaza Kilimanjaro, Serengeti na mengineyo kama hii Filamu nadhani tungekuwa na wageni mpaka tungeanza kutafuta mbinu za kuwapunguza...

Yaani ni kama tunakisifia / tangaza kikombe kuliko hata chai iliyomo
 
Kipengele namba 4 kimenifikirisha sana 😂

4. Kitendo cha Msemaji Mkuu wa Serikali kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu ni mahojiano ya kupendeza Sana
 
Ushauri mzuri sio rahisi kuupata,,, pia ni vigumu kuufuata... hasa kwa Mswahili.

Acha tuone kama wamesikia
 
Wanabodi,
leo nilikuwa naangalia TBC Ardhio.

  1. Nikashuhudia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akirudia kazi yake ya zamani ya utangazaji wa TV Reporting akiripotia TBC live mubashara moja kwa moja kutokea jijini New York, nchini Marekani kutuarifu maandalizi ya uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour, utakaofanyika usiku huu mida ya Saa 1:30 Kwa saa za Marekani ambapo ni saa 8:30 za usiku wa manane kwa saa za Tanzania.
  2. Msigwa ambaye sasa ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, amejikumbusha enzi zake za utangazaji, kwa kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu Dr. Hassan Abasi ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni na ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya filamu ya Royal Tour,
  3. Dr. Hassan Abbas amesema uzinduzi utahudhuriwa na wageni mashuhuri 400 akiwemo Mayor wa Jiji la New York.
  4. Kitendo cha Msemaji Mkuu wa Serikali kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu ni mahojiano ya kupendeza Sana.
  5. Kiukweli kipaji cha TV Reporting na composeture yake, hiki ni moja ya vipaji vikubwa sana ambavyo TBC ilivipotezea serikalini. Ndani ya TBC anayemkaribia Msigwa ni Khalid Gangana.
  6. Hongera Sana Gerson Msigwa kurudia kazi yako ya utangazaji!. Hiki ulichokifanya leo jijini New York, nchini Marekani, ndicho ulipaswa ukifanye Ikulu yetu, siku zote ilipokuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
  7. Kazi ya Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, sio tuu ni kuandika Press Release, bali pia kuiripoti direct from Ikulu kwa piece to camera kama ulivyo fanya leo.
  8. Ulipaswa kuturipotia shughuli muhimu za rais ikitokea Ikulu, na kuiripoti moja kwa moja into the news.
  9. Pia ulipaswa kuitisha Press Conference na kufanya Press Briefing kwetu sisi waandishi kama walivyofanya Balozi Choks, Balozi Nkurlu na Balozi Kalaghe, na kama wafanyavyo ma Press Sec wa wenzetu Duniani.
  10. Naamini Zuhura Yunus hata kuwa Bubu, ikitokea rais ana shughuli muhimu, asiishie kutusambazia just a press release bali sasa sambazeni multi media release yenye press release, photo gallery, audio footage, TV footage, social media footage na Peace to Camera.
All and all, hongereni sana for all that you are doing, Leo sisi huku Bongo ni hakuna kulala mpaka hiyo saa 8:30 usiku wa manane.
Tunawasubiria tushuhudie.
Paskali.
Mabandiko mengine kuhusu Royal Tour

Baada ya kuona hatuteuliwi na wale tuliokuwa tukiwadharau na Sisi tunaojifanya Manguli wa Tasnia na wenye Akili Wakiteuliwa na Sisi kuendelea tu kupiga Kazi za Deiwaka katika Media na Maisha yakitupiga sasa tumeamua Kujipendekeza kwa Wateuwaji na Wasaidizi Kiutendaji wa Mteuwaji akina Msigwa na Dkt. Abbas ili basi nao wakiwa karibu na Mteuwaji wa Nafasi za Nyadhifa waweze Kutuombea ( Kutupigia Chapuo ) ili ikiwezekana katika Teuzi zijazo basi nasi Wanafiki tuwezee Kuula ili tupate Unafuu wa haya Maisha yetu Magumu ( ambayo hatukuyategemea ) tunayoyapitia sasa.
 
nimekipenda kiingereza cha Msigwa cha go -go -go(sic) kizungu cha Iringa go - go -go no worry (msemaji wa Serikali) nakushauri uwekeze kwenye ku-polish kizungu chako
 
Baada ya kuona hatuteuliwi na wale tuliokuwa tukiwadharau na Sisi tunaojifanya Manguli wa Tasnia na wenye Akili Wakiteuliwa na Sisi kuendelea tu kupiga Kazi za Deiwaka katika Media na Maisha yakitupiga sasa tumeamua Kujipendekeza kwa Wateuwaji na Wasaidizi Kiutendaji wa Mteuwaji akina Msigwa na Dkt. Abbas ili basi nao wakiwa karibu na Mteuwaji wa Nafasi za Nyadhifa waweze Kutuombea ( Kutupigia Chapuo ) ili ikiwezekana katika Teuzi zijazo basi nasi Wanafiki tuwezee Kuula ili tupate Unafuu wa haya Maisha yetu Magumu ( ambayo hatukuyategemea ) tunayoyapitia sasa.
Mimi ni kawaida yangu, kwenye mazuri napongeza, na ikitokea issue ya spana, napiga spana, ila spana zangu sio spana tuu ili mradi kupiga spana, spana zangu ni constructive criticism huku nikitoa ushauri wa the right thing to do.

Kama issue ni kumfagilia na kumpongeza Gerson Msigwa, angalia tarehe ya bandiko hili,
ujiulize wakati nikiandika hayo, Gerson alikuwa nani na alikuwa wapi?.

Na kama unadhani kazi yangu ni kumfagilia tuu, kanisome hapa uangalie nimesema nini kumhusu Gerson na Dr. Abbas Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Hata hapa

Hivyo please stop this nonsense kuwa kila anayepongeza, anasaka uteuzi!, maana hata Mama mwenyewe kuna wakati tunambananisha

P
 
Wanabodi,
leo nilikuwa naangalia TBC Ardhio.

  1. Nikashuhudia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akirudia kazi yake ya zamani ya utangazaji wa TV Reporting akiripotia TBC live mubashara moja kwa moja kutokea jijini New York, nchini Marekani kutuarifu maandalizi ya uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour, utakaofanyika usiku huu mida ya Saa 1:30 Kwa saa za Marekani ambapo ni saa 8:30 za usiku wa manane kwa saa za Tanzania.
  2. Msigwa ambaye sasa ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, amejikumbusha enzi zake za utangazaji, kwa kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu Dr. Hassan Abasi ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni na ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya filamu ya Royal Tour,
  3. Dr. Hassan Abbas amesema uzinduzi utahudhuriwa na wageni mashuhuri 400 akiwemo Mayor wa Jiji la New York.
  4. Kitendo cha Msemaji Mkuu wa Serikali kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu ni mahojiano ya kupendeza Sana.
  5. Kiukweli kipaji cha TV Reporting na composeture yake, hiki ni moja ya vipaji vikubwa sana ambavyo TBC ilivipotezea serikalini. Ndani ya TBC anayemkaribia Msigwa ni Khalid Gangana.
  6. Hongera Sana Gerson Msigwa kurudia kazi yako ya utangazaji!. Hiki ulichokifanya leo jijini New York, nchini Marekani, ndicho ulipaswa ukifanye Ikulu yetu, siku zote ilipokuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
  7. Kazi ya Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, sio tuu ni kuandika Press Release, bali pia kuiripoti direct from Ikulu kwa piece to camera kama ulivyo fanya leo.
  8. Ulipaswa kuturipotia shughuli muhimu za rais ikitokea Ikulu, na kuiripoti moja kwa moja into the news.
  9. Pia ulipaswa kuitisha Press Conference na kufanya Press Briefing kwetu sisi waandishi kama walivyofanya Balozi Choks, Balozi Nkurlu na Balozi Kalaghe, na kama wafanyavyo ma Press Sec wa wenzetu Duniani.
  10. Naamini Zuhura Yunus hata kuwa Bubu, ikitokea rais ana shughuli muhimu, asiishie kutusambazia just a press release bali sasa sambazeni multi media release yenye press release, photo gallery, audio footage, TV footage, social media footage na Peace to Camera.
All and all, hongereni sana for all that you are doing, Leo sisi huku Bongo ni hakuna kulala mpaka hiyo saa 8:30 usiku wa manane.
Tunawasubiria tushuhudie.
Paskali.
Mabandiko mengine kuhusu Royal Tour
Acha uongo, Dr.Abasi hakusitaafu, Ungesema msemaji wa Serikali wa zamani.
 
Sio hivyo bali mlengwa ni mtalii wa nje na hivyo kule ndio kunaibeba kwanza kabla ya kuletwa huku na kufanyiwa Swahili subtitles!
Ulichojibu ndo hicho ninachosisitiza.
Anyway: Kabla ya #RoyalTourTanzania; Peter Greenberg alitengeneza #RoyalTourTanzania miaka 8 iliyopita.
Screenshot_20220419-155543.png
Sasa ushajua idea ni ya nani...
 
Back
Top Bottom