Alichokifanya leo Makonda ndo Jambo analoweza zaidi. Naionea huruma Tanzania

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Ukienda China kuna mfumo wa mikoa kama kwetu. Wao wanaita Provinces, na tofauti yao na sie ni kuwa wao mikoa yao ni mikoa ya kiuchumi ( Economic provinces) wakati sie mikoa yetu ni mikoa ya kisiasa (political provinces)

Wanapotushinda China ni watu wanaoteuliwa kuongoza hizo provinces. Kwao wanateua watu wenye uwezo na mawazo makubwa ya kiuchumi unaweza sema watu creative na innovative ambao wamesoma, wana exposure na wana uelewa mkubwa wa masuala ya kiuchumi na kidunia.

Provinces za China zinashindana kiuchumi, hawa wanaanzisha viwanda wa mafriji hawa wanaanzisha viwanda vya washing machines. Ili mradi siku ya mwisho provinces moja iwe zaidi ya nyingine kiuchumi na kimaendeleo.

Leo Mkuu wa Mkoa wa Arusha kapewa mic aongee kwenye tukio la Kumbukumbu cha kifo cha Sokoine. Pamoja na kumuelezea Sokoine , kwa watu wenye akili walitegemea ni kitu gani ambacho atakiongea katika kuelezea namna ambavyo ataweka mipango kabambe ili Jiji lile liwe namba moja kiuchumi Tanzania.

Tofauti na hayo Makonda ameelezea kuweka baiskeli za polisi, camera za usalama barabarani mambo ambayo unaweza sema kuwa ni just petty issues!

Mbaya zaidi kama kawaida yake, ametoa vitisho kwa watu eti wanaomsema Rais Samia.

Napenda kuwaambia wana JF huyu ndo makonda sasa na alilofanya leo ndo mambo anayoweza. Ufitini, uchonganishi, kujipendekeza na kujifanya yeye ndo anayempenda zaidi kiongozi wake kuliko mtu yeyote yule ili angalau aendelee kupata vyeo na kuishi kupitia hivyo vyeo.

Alivyo Makonda ndo walivyo watu na vijana wengi kuanzia Chama cha Mapinduzi hadi sehemu nyingine. Hawana muda wa kuonesha uwezo wao kwenye mambo ya msingi bali kujipendekeza kwa watu wenye nafasi ili waendelee kula.

Naionea huruma Tanzania. Kesho yetu inasikitisha hakika.

Kauli ya Makonda kuwataja wanaomchafua Rais Samia, soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri
 
Ukienda China kuna mfumo wa mikoa kama kwetu. Wao wanaita Provinces, na tofauti yao na sie ni kuwa wao mikoa yao ni mikoa ya kiuchumi ( Economic provinces) wakati sie mikoa yetu ni mikoa ya kisiasa (political provinces)

Wanapotushinda China ni watu wanaoteuliwa kuongoza hizo provinces. Kwao wanateua watu wenye uwezo na mawazo makubwa ya kiuchumi unaweza sema watu creative na innovative ambao wamesoma, wana exposure na wana uelewa mkubwa wa masuala ya kiuchumi na kidunia.

Provinces za China zinashindana kiuchumi, hawa wanaanzisha viwanda wa mafriji hawa wanaanzisha viwanda vya washing machines. Ili mradi siku ya mwisho provinces moja iwe zaidi ya nyingine kiuchumi na kimaendeleo.

Leo Mkuu wa Mkoa wa Arusha kapewa mic aongee kwenye tukio la Kumbukumbu cha kifo cha Sokoine. Pamoja na kumuelezea Sokoine , kwa watu wenye akili walitegemea ni kitu gani ambacho atakiongea katika kuelezea namna ambavyo ataweka mipango kabambe ili Jiji lile liwe namba moja kiuchumi Tanzania.

Tofauti na hayo Makonda ameelezea kuweka baiskeli za polisi, taa za usalama barabarani mambo ambayo unaweza sema kuwa ni just petty issues!

Mbaya zaidi kama kawaida yake, ametoa vitisho kwa watu eti wanaomsema Rais Samia.

Napenda kuwaambia wana JF huyu ndo makonda sasa na alilofanya leo ndo mambo anayoweza. Ufitini, uchonganishi, kujipendekeza na kujifanya yeye ndo anayempenda zaidi kiongozi wake kuliko mtu yeyote yule ili angalau aendelee kupata vyeo na kuishi kupitia hivyo vyeo.

Alivyo Makonda ndo walivyo watu na vijana wengi kuanzia Chama cha Mapinduzi hadi sehemu nyingine. Hawana muda wa kuonesha uwezo wao kwenye mambo ya msingi bali kujipendeleza kwa watu wenye nafasi ili waendelee kula.

Makonda ana tofauti gani na Samia ?

Pamoja ya kwamba mengi uliyo andika kuhusu China ni uzushi tu.
 
Sasa hivi ndio wanaccm wengi wamekuwa hivyo, ni kuwa chawa wa mteule Ili wapate vyeo. Na kwenye hizo mbio zao ndio wanaishia kufanyiana fitina, umbea na upuuzi mwingine wa aina hiyo.
 
Teh binafsi sishangai, ndio mfumo wa utawala wa bongo ulivyo. Mkuu wa Mkoa ni just mwakilishi wa Raisi mkoa aliopo na Mwenyekiti wa usalama. So kua chawa wa aliemueka hapo ni "Given" sio ombi.

Pili, mfumo wa hicho chama chao umefanya cheo cha ukuu wa mkoa ama ukuu wa wilaya kua kama vyeo vya "kupozana" baada ya mhangaiko chawa mwenye mdomo mrefu anaopitia katika mapambano ya kumpamba mwenyekiti wao.

Kwa kifupi ukuu wa mkoa, ukuu wa wilaya tz ni more of "ulinzi" kuliko maendeleo kwa wananchi. Kazi ambayo kila mmoja anaeza ifanya ukizingatia watanzania hatuna maajab sana kwenye matukio mabovu.

Lau kama ukuu wa mkoa au wilaya ingekua mithili ya China ambayo umeitolea mfano sidhani kama kuna hata 10% ya waliopo wamekidhi vigezo.
 
Katiba

Tunarudi palepale "KATIBA"
 
Ukienda China kuna mfumo wa mikoa kama kwetu. Wao wanaita Provinces, na tofauti yao na sie ni kuwa wao mikoa yao ni mikoa ya kiuchumi ( Economic provinces) wakati sie mikoa yetu ni mikoa ya kisiasa (political provinces)

Wanapotushinda China ni watu wanaoteuliwa kuongoza hizo provinces. Kwao wanateua watu wenye uwezo na mawazo makubwa ya kiuchumi unaweza sema watu creative na innovative ambao wamesoma, wana exposure na wana uelewa mkubwa wa masuala ya kiuchumi na kidunia.

Provinces za China zinashindana kiuchumi, hawa wanaanzisha viwanda wa mafriji hawa wanaanzisha viwanda vya washing machines. Ili mradi siku ya mwisho provinces moja iwe zaidi ya nyingine kiuchumi na kimaendeleo.

Leo Mkuu wa Mkoa wa Arusha kapewa mic aongee kwenye tukio la Kumbukumbu cha kifo cha Sokoine. Pamoja na kumuelezea Sokoine , kwa watu wenye akili walitegemea ni kitu gani ambacho atakiongea katika kuelezea namna ambavyo ataweka mipango kabambe ili Jiji lile liwe namba moja kiuchumi Tanzania.

Tofauti na hayo Makonda ameelezea kuweka baiskeli za polisi, taa za usalama barabarani mambo ambayo unaweza sema kuwa ni just petty issues!

Mbaya zaidi kama kawaida yake, ametoa vitisho kwa watu eti wanaomsema Rais Samia.

Napenda kuwaambia wana JF huyu ndo makonda sasa na alilofanya leo ndo mambo anayoweza. Ufitini, uchonganishi, kujipendekeza na kujifanya yeye ndo anayempenda zaidi kiongozi wake kuliko mtu yeyote yule ili angalau aendelee kupata vyeo na kuishi kupitia hivyo vyeo.

Alivyo Makonda ndo walivyo watu na vijana wengi kuanzia Chama cha Mapinduzi hadi sehemu nyingine. Hawana muda wa kuonesha uwezo wao kwenye mambo ya msingi bali kujipendeleza kwa watu wenye nafasi ili waendelee kula.

Naionea huruma Tanzania. Kesho yetu inasikitisha hakika.

Kauli ya Makonda kuwataja wanaomchafua Rais Samia, soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri
Mbona huyu Makonda katujazia sana server zetu za Jf?

Nadhani mimi sasa nifungue jicho langu la tatu kuangazia u special wa huyu binadamu!

Nasema hivi kwa sababu, kila anayeandika kumuongelea makonda, anaibuka na sababu 'finye' inayoshindwa kumbana Makonda sawasawa, ili tuweze kuyaona makosa yake yanayopelekea kusemwa vibaya namna hii!

Kwenye logic ya thread hii, ni kiongozi gani kwa cheo cha Rc aliyeteuliwa kutokana na exposure na ubunifu wake wa maendeleo, si ni wale wale tu wenye majina ya koo za marehemu viongozi waasisi, kwa nini leo iwe kwa Makonda?

Tunapozidi kujaza ma page humu kuongelea mtu mmoja bila shutuma za maana tunamjenga badala ya kumbomoa na kuonekana wenye chuki naye kawashika pabaya sana mwaka huu na hawana pa kupumulia.
 
Back
Top Bottom