Nami nakushangaa kuilinganisha Tanzania na Uchina bora ungeilinganisha na nchi mojawapo ya Afrika. Halafu Province si mkoa. Mkoa ni Region.Ukienda China kuna mfumo wa mikoa kama kwetu. Wao wanaita Provinces, na tofauti yao na sie ni kuwa wao mikoa yao ni mikoa ya kiuchumi ( Economic provinces) wakati sie mikoa yetu ni mikoa ya kisiasa (political provinces)
Wanapotushinda China ni watu wanaoteuliwa kuongoza hizo provinces. Kwao wanateua watu wenye uwezo na mawazo makubwa ya kiuchumi unaweza sema watu creative na innovative ambao wamesoma, wana exposure na wana uelewa mkubwa wa masuala ya kiuchumi na kidunia.
Provinces za China zinashindana kiuchumi, hawa wanaanzisha viwanda wa mafriji hawa wanaanzisha viwanda vya washing machines. Ili mradi siku ya mwisho provinces moja iwe zaidi ya nyingine kiuchumi na kimaendeleo.
Leo Mkuu wa Mkoa wa Arusha kapewa mic aongee kwenye tukio la Kumbukumbu cha kifo cha Sokoine. Pamoja na kumuelezea Sokoine , kwa watu wenye akili walitegemea ni kitu gani ambacho atakiongea katika kuelezea namna ambavyo ataweka mipango kabambe ili Jiji lile liwe namba moja kiuchumi Tanzania.
Tofauti na hayo Makonda ameelezea kuweka baiskeli za polisi, camera za usalama barabarani mambo ambayo unaweza sema kuwa ni just petty issues!
Mbaya zaidi kama kawaida yake, ametoa vitisho kwa watu eti wanaomsema Rais Samia.
Napenda kuwaambia wana JF huyu ndo makonda sasa na alilofanya leo ndo mambo anayoweza. Ufitini, uchonganishi, kujipendekeza na kujifanya yeye ndo anayempenda zaidi kiongozi wake kuliko mtu yeyote yule ili angalau aendelee kupata vyeo na kuishi kupitia hivyo vyeo.
Alivyo Makonda ndo walivyo watu na vijana wengi kuanzia Chama cha Mapinduzi hadi sehemu nyingine. Hawana muda wa kuonesha uwezo wao kwenye mambo ya msingi bali kujipendeleza kwa watu wenye nafasi ili waendelee kula.
Naionea huruma Tanzania. Kesho yetu inasikitisha hakika.
Kauli ya Makonda kuwataja wanaomchafua Rais Samia, soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri
Mwacheni Makonda afanye kazi yake au ndiyo wewe Waziri uliyetajwa?
Atawanyosha !!