Alichokifanya leo Makonda ndo Jambo analoweza zaidi. Naionea huruma Tanzania

Alichokifanya leo Makonda ndo Jambo analoweza zaidi. Naionea huruma Tanzania

Makonda ni Sokoine wa Karne hii 🐒

Sokoine hakupendwa na wavivu hata kidogo, alikua hafurahishi mtu...

alisema na kutenda.
kwa sababu ya utendaji wake wa wazi hakupendwa mpaka alipo kufa 🐒

Makonda na Sokoine ni twins 🐒
Nani kakuambia makonda ni mpigaji kama wapigaji wengine
Anacheza na skili zenu nyie wanyonge

Ova
 
Nani kakuambia makonda ni mpigaji kama wapigaji wengine
Anacheza na skili zenu nyie wanyonge

Ova
hakuna haja ya kuambiwa kitu na mtu 🐒

vitu viko bayana vinafanyika mchana kweupe mbona🐒
 
Mkuu nondo ya Uchina na "Provinces" umeichambua vyema sana.
Nimepata kitu kwenye huu uchambuzi.
Kuhusu Makonda ni kweli unaloongea.
 
Narudia tena, Makonda akimaliza miezi 6 kwenye uRC nakunya kwenye daladala.
 
Mfumo mzima wa uongozi wa Tanzania ni wa kunyenyekea na kujipendekeza kwa bosi ili uonwe na upandishwe.

Mfumo huu uliasisiwa na Mwalimu, angalau Mkapa alijitahidi kuangalia umahiri wa kitaaluma na utendaji kazi.

CCM imepandikiza mfumo huu kwenye maisha ya Watanzania kiasi kwamba sasa imekuwa ni "part & parcel" ya maisha ya wengi wetu.

Kwani tunaishi kwa hisani ya CCM ama ya Mwenyezi Mungu!!??
Kiongozi apatikane kwa utaratibu wa kugombea zaidi kuliko kuteuliwa.
Kama ikibidi kuteua, wawe watu wazima wenye uzoefu wa maisha katika nyanja mbalimbali badala ya sarakasi za siku hizi za kutafuta uteuzi.
 
Kuna mzee mmoja alifanikiwa kumwoza binti yake.
Siku ya sendoff alipewa mic akasema; binti yangu sasa umeolewa naomba uachane na Emanuel atakuharibia ndoa yako.

alimwacha?
 
Ukienda China kuna mfumo wa mikoa kama kwetu. Wao wanaita Provinces, na tofauti yao na sie ni kuwa wao mikoa yao ni mikoa ya kiuchumi ( Economic provinces) wakati sie mikoa yetu ni mikoa ya kisiasa (political provinces)

Wanapotushinda China ni watu wanaoteuliwa kuongoza hizo provinces. Kwao wanateua watu wenye uwezo na mawazo makubwa ya kiuchumi unaweza sema watu creative na innovative ambao wamesoma, wana exposure na wana uelewa mkubwa wa masuala ya kiuchumi na kidunia.

Provinces za China zinashindana kiuchumi, hawa wanaanzisha viwanda wa mafriji hawa wanaanzisha viwanda vya washing machines. Ili mradi siku ya mwisho provinces moja iwe zaidi ya nyingine kiuchumi na kimaendeleo.


Leo Mkuu wa Mkoa wa Arusha kapewa mic aongee kwenye tukio la Kumbukumbu cha kifo cha Sokoine. Pamoja na kumuelezea Sokoine , kwa watu wenye akili walitegemea ni kitu gani ambacho atakiongea katika kuelezea namna ambavyo ataweka mipango kabambe ili Jiji lile liwe namba moja kiuchumi Tanzania.

Tofauti na hayo Makonda ameelezea kuweka baiskeli za polisi, camera za usalama barabarani mambo ambayo unaweza sema kuwa ni just petty issues!

Mbaya zaidi kama kawaida yake, ametoa vitisho kwa watu eti wanaomsema Rais Samia.

Napenda kuwaambia wana JF huyu ndo makonda sasa na alilofanya leo ndo mambo anayoweza. Ufitini, uchonganishi, kujipendekeza na kujifanya yeye ndo anayempenda zaidi kiongozi wake kuliko mtu yeyote yule ili angalau aendelee kupata vyeo na kuishi kupitia hivyo vyeo.

Alivyo Makonda ndo walivyo watu na vijana wengi kuanzia Chama cha Mapinduzi hadi sehemu nyingine. Hawana muda wa kuonesha uwezo wao kwenye mambo ya msingi bali kujipendekeza kwa watu wenye nafasi ili waendelee kula.

Naionea huruma Tanzania. Kesho yetu inasikitisha hakika.

Kauli ya Makonda kuwataja wanaomchafua Rais Samia, soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri
Mtatajwa wote.
Endeleeni kumsimanga rais ohooo 😀
 
Mbona huyu Makonda katujazia sana server zetu za Jf?

Nadhani mimi sasa nifungue jicho langu la tatu kuangazia u special wa huyu binadamu!

Nasema hivi kwa sababu, kila anayeandika kumuongelea makonda, anaibuka na sababu 'finye' inayoshindwa kumbana Makonda sawasawa, ili tuweze kuyaona makosa yake yanayopelekea kusemwa vibaya namna hii!

Kwenye logic ya thread hii, ni kiongozi gani kwa cheo cha Rc aliyeteuliwa kutokana na exposure na ubunifu wake wa maendeleo, si ni wale wale tu wenye majina ya koo za marehemu viongozi waasisi, kwa nini leo iwe kwa Makonda?

Tunapozidi kujaza ma page humu kuongelea mtu mmoja bila shutuma za maana tunamjenga badala ya kumbomoa na kuonekana wenye chuki naye kawashika pabaya sana mwaka huu na hawana pa kupumulia.
Mkuu upo sahihi sana.Nashauri,hawa wanaompiga vita Makonda,wajutathimini,maana wananchi wengi wanamkubali sana huyu mtu kwa utendaji wake [namna anavyotatua changamoto zao].Waelekeze nguvu zao kwenye mambo mengine ya msingi,ila kwa Makonda hawatafanikiwa.
 
Makonda ni Sokoine wa Karne hii [emoji205]

Sokoine hakupendwa na wavivu hata kidogo, alikua hafurahishi mtu...

alisema na kutenda.
kwa sababu ya utendaji wake wa wazi hakupendwa mpaka alipo kufa [emoji205]

Makonda na Sokoine ni twins [emoji205]
Acha kupayuka na kumsingizia Sokoine wakati humjui na hujawahi kufanya naye kazi.
Unatenda kosa kubwa sana kumfananisha Sokoine na huyu muhuni mshamba na asiye na elimu wala weledi.
Makonda ni wa kufananisha na kina Steve Nyerere au Mwijaku sio Sokoine ambaye aliogopwa sio kuchukiwa na wale wote wasio wajibika na hakuwa mtu wa drama hata kidogo.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom