Alichokifanya leo Makonda ndo Jambo analoweza zaidi. Naionea huruma Tanzania

Alichokifanya leo Makonda ndo Jambo analoweza zaidi. Naionea huruma Tanzania

Mleta mada ulichotakiwa kushangaa na kuchambua KWANZA kabisa ni huyo anayemteua kwenye hizo nafasi. PILI nini umuhimu na matarajio ya hizo nafasi kwa taifa? How relevant are these positions plus how can they be?

Kumzungumzia Makonda ni wrong target; haina maana. Nchi ina wajinga na wagonjwa wa akili wengi tu. Yule anayeteua watu wa aina hiyo kwenye nafasi muhimu za uongozi ndiye wa kutafakariwa; ndiye habari ya kujadiliwa. Sio mbwa anayeuma mtu.
 
Badala ya kuongelea tunu za Sokoine yeye ni mama.., mama..., mama..., hivi Makonda kwanini anahangaika sana na mama za watu, hajui kuwa Samia si mama yake?
Mama yake kamkana leo na mama yake ni Samia.
 
Ukienda China kuna mfumo wa mikoa kama kwetu. Wao wanaita Provinces, na tofauti yao na sie ni kuwa wao mikoa yao ni mikoa ya kiuchumi ( Economic provinces) wakati sie mikoa yetu ni mikoa ya kisiasa (political provinces)

Wanapotushinda China ni watu wanaoteuliwa kuongoza hizo provinces. Kwao wanateua watu wenye uwezo na mawazo makubwa ya kiuchumi unaweza sema watu creative na innovative ambao wamesoma, wana exposure na wana uelewa mkubwa wa masuala ya kiuchumi na kidunia.

Provinces za China zinashindana kiuchumi, hawa wanaanzisha viwanda wa mafriji hawa wanaanzisha viwanda vya washing machines. Ili mradi siku ya mwisho provinces moja iwe zaidi ya nyingine kiuchumi na kimaendeleo.

Leo Mkuu wa Mkoa wa Arusha kapewa mic aongee kwenye tukio la Kumbukumbu cha kifo cha Sokoine. Pamoja na kumuelezea Sokoine , kwa watu wenye akili walitegemea ni kitu gani ambacho atakiongea katika kuelezea namna ambavyo ataweka mipango kabambe ili Jiji lile liwe namba moja kiuchumi Tanzania.

Tofauti na hayo Makonda ameelezea kuweka baiskeli za polisi, camera za usalama barabarani mambo ambayo unaweza sema kuwa ni just petty issues!

Mbaya zaidi kama kawaida yake, ametoa vitisho kwa watu eti wanaomsema Rais Samia.

Napenda kuwaambia wana JF huyu ndo makonda sasa na alilofanya leo ndo mambo anayoweza. Ufitini, uchonganishi, kujipendekeza na kujifanya yeye ndo anayempenda zaidi kiongozi wake kuliko mtu yeyote yule ili angalau aendelee kupata vyeo na kuishi kupitia hivyo vyeo.

Alivyo Makonda ndo walivyo watu na vijana wengi kuanzia Chama cha Mapinduzi hadi sehemu nyingine. Hawana muda wa kuonesha uwezo wao kwenye mambo ya msingi bali kujipendekeza kwa watu wenye nafasi ili waendelee kula.

Naionea huruma Tanzania. Kesho yetu inasikitisha hakika.

Kauli ya Makonda kuwataja wanaomchafua Rais Samia, soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri
Ila tuseme ukweli, Makonda anawatesa sana! Yaani saver zote humu JF zimejaa Makonda tu!!!
 
Acha kupayuka na kumsingizia Sokoine wakati humjui na hujawahi kufanya naye kazi.
Unatenda kosa kubwa sana kumfananisha Sokoine na huyu muhuni mshamba na asiye na elimu wala weledi.
Makonda ni wa kufananisha na kina Steve Nyerere au Mwijaku sio Sokoine ambaye aliogopwa sio kuchukiwa na wale wote wasio wajibika na hakuwa mtu wa drama hata kidogo.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
sio suala la kujuana hapa au kusubiri mpaka afe ndio tuanze unafiki kwamba ooh Fulani alikua nini nini n.k....

sokoine aliogopwa sana na wavivu, viongozi wasio wabunifu, wala rushwa, wavunja sheria na waliozoea kufanya kazi kimazoea the same way Makonda alivyo 🐒

so,
ukimchukia Makonda na utendaji wake huna tofauti na anaemchukia hayati sokoine 🐒

sokoine hakuwa anakusudia kumchekesha au kumuudhi mtu, ispokua alitamani watu wote kufanya kazi kwa bidii na hatimae wote wafurahie matunda ya bidii katika kazi zao.........

And that,
hayati Moringe Sokoine is now, Paul Christian Makonda,The RC, Arusha Region 🐒
 
Nani kakuambia makonda ni mpigaji kama wapigaji wengine
Anacheza na skili zenu nyie wanyonge

Ova
hili si suala la kuambiwa 🐒

ni Jambo bayana kabisaa, liko wazi mchana kweupe na linaonekana kwa maneno na matendo 🐒

mchapakazi RC Paul Makonda anazidi kudhihitisha si tu ujasiri wake katika kufanya kazi lakin pia jinsi alivyojizatiti kwa umakini na umahiri wa viwango vya juu sana,

kwamba he determined, committed and very able to confront both setbacks and challenges ahead of transforming Arusha region into prosperous 🐒
 
Mkuu upo sahihi sana.Nashauri,hawa wanaompiga vita Makonda,wajutathimini,maana wananchi wengi wanamkubali sana huyu mtu kwa utendaji wake [namna anavyotatua changamoto zao].Waelekeze nguvu zao kwenye mambo mengine ya msingi,ila kwa Makonda hawatafanikiwa.
Nani ampige vita makonda? Ili iweje? Hivi nyie watu akili zenu ziko sawa kumtetea huyo mpuuzi wenu?
 
Ila tuseme ukweli, Makonda anawatesa sana! Yaani saver zote humu JF zimejaa Makonda tu!!!
Your name reflects your thinking capacity! Makonda anamtesa nani?

Hivi ana kipi cha kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi bora let's say in the next 50 years tu? Umeona hata kama ana vision yeyote?
 
hili si suala la kuambiwa 🐒

ni Jambo bayana kabisaa, liko wazi mchana kweupe na linaonekana kwa maneno na matendo 🐒

mchapakazi RC Paul Makonda anazidi kudhihitisha si tu ujasiri wake katika kufanya kazi lakin pia jinsi alivyojizatiti kwa umakini na umahiri wa viwango vya juu sana,

kwamba he determined, committed and very able to confront both setbacks and challenges ahead of transforming Arusha region into prosperous 🐒
Hamna kitu nyie endeleeni kusikia porojo na umbea wa wanasiasa

Ova
 
😂Daah Makonda anatakiwa apatiwe washauri maana anaongea tu bila kujali muktadha au mazingira
 
Hamna kitu nyie endeleeni kusikia porojo na umbea wa wanasiasa

Ova
actually,
Mwanasiasa makini hawezi kupuuza chochote. whether ni hicho unachoita porojo na umbea au vinginevyo 🐒

kupuuza ni among political mistakes ambazo zinaweza kukupelekea ukafanya blunders ambayo itaweza kukufanya politically irrelevant in political sphere 🐒

so,
in professional politics we don't underrate political issues, allegations or statements. we work on it in a very serious way 🐒

and for your information, what RC is doing is going to swip some political giants as soon as possible 🐒
 
Mmekalia kuwaza siasa na vyeo tu. Hamuwazi mambo ya msingi ya kuipeleka nchi yetu mbele. Ni ujinga na upuuzi tu.

Ni laana kwa nchi kuwa na watu wa namna yenu.
 
Mmekalia kuwaza siasa na vyeo tu. Hamuwazi mambo ya msingi ya kuipeleka nchi yetu mbele. Ni ujinga na upuuzi tu.

Ni laana kwa nchi kuwa na watu wa namna yenu.
Tupo pazuri, tupo vizuri na kwakweli tunaelekea pazuri zaidi, chini ya uongozi shupavu na madhubuti sana wa Dr.Samia Suluhu Hassan 🐒

wanainchi wengine humu nchini wanafurahia sana, matunda ya mipango mizuri sana ya kimaendeleo yanayotokana na ilani bora kabisa ya chama cha Mapinduzi 🐒

wavivu bado mtaendelea kulalamika mpaka muongeze bidii katika kufanya kazi, kwani mtaji ulionao ni nguvu zako mwenyewe 🐒
 
Hongera sana! Endeleza kipaji giza chako
 
Your name reflects your thinking capacity! Makonda anamtesa nani?

Hivi ana kipi cha kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi bora let's say in the next 50 years tu? Umeona hata kama ana vision yeyote?
Jukwaa la Siasa jana lote lilijaa nyuzi za Makonda. Hukuona hilo?
 
Eti mama angu Samia Suluhu, yaani unaweza kudhania Samia ni mama ake mzazi aliyemzaa...
 
Back
Top Bottom