troiker
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 1,551
- 2,573
Ukitizama kwa jicho la ndani zaidi, Lukuvi na Palamagamba, kwa watanzania makini, na wazalendo wa kweli, bila ushabiki wa milengo ya kisiasa, watu hawa ni makini na weledi katika utendaji wa kazi ,na hili limedhihirika kwa michango ya watanzania wote kupitia mabadiliko ya baraza la mawaziri, wamesemwa kwa wema zaidi, na wananchi walishangazwa kuachwa kwao kwenye mabadiliko ya baraza la mawaziri.
Hawa viongozi waengeunganisha nguvu na wasiokubaliana na utendaji wa rais Samia +wapinzani wasio na vyama na wa vyama vya upinzani ilikuwa ni kazi ngumu sana kwa yeye 2025.
Pili imedhihirika mabadiliko haya ya baraza la Mawaziri yalilenga kuwaingiza watoto wa vigogo ,na ili waingie ilitakiwa panga pangua kupoteza maboya kwa kugusa mpaka makatibu wakuu na manaibu (kiini macho).
Hivyo ametolewa Waitara na Kitila kama wageni kupisha watoto wa wenye chama chao .ile dhana ya kila mtanzania aweza kuwa kiongozi inaondoka taratibu.
Ifahamike nje ya hii CCM ya sasa hakutakuwa na jipya, zaidi ni kusindikiza watawala na familia zao mpaka messiah atakaporudi.
Ukombozi utapatikana wa kisiasa na kiuchumi kwa watanzania kusema sasa basi imetosha,kama tutaendelea kusema hewala Mungu yupo bila kuchukua hatua tumekwisha Watanzania.
Mwisho bila CCM kupasuka tutateseka daima ile tabia ya kuacha Mbowe anateseka mahakamani na kuvalia njuga mambo ya CCM haifai hata kidogo.