Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...

Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...

Tanzania bara iache uoga! Kwanini wasiache mambo ya nje, sarafu na bank kuu, na ushuru wa forodha nje ya muungano?

Kwani ZNZ inachangia kiasi kukubwa sana nini au Tangayika bara inaogopa dumping kutoka ZNZ?

Huu ni muungano na wala sio ukoloni. Mambo ya kutishana kwamba ZNZ haiwezi kusimama peke yake hayana nafasi kwa wakati huu.
 
chabuso,

..data zangu nimezipata UN kwenyewe. bofya hapa http://www.un.org/en/members/growth.shtml

..kwani wewe data zinazosema Tanzania inatumia kiti cha Zanzibar umezipata wapi?

..hivi una uhakika kama serikali ya Mapinduzi, ilishateua balozi wake kwenda kuiwakilisha UN??

..kuna mambo mengi sana yasiyo ya kweli yanasemwa kuhusu Tanganyika. Jaribu kuyahakiki mambo hayo kabla hujayaamini.


Tanganyika was a Member of the United Nations from 14 December 1961 and Zanzibar was a Member from 16 December 1963.


Following the ratification on 26 April 1964 of Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar, the United Republic of Tanganyika and Zanzibar continued as a single Member, changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964.

cc: Nguruvi3, GHIBUU, kibungano, Nonda
 
Last edited by a moderator:
Huu muungano unapaswa kuwa wa kiulinzi tu. Hayo mambo mengine yote piga chini.

Tanganyika ndio itakuwa kama ndio mwanzo inapata uhuru. Maana itawalazimu kwenda kujitambulisha kimataifa kwamba mnaitwa watanganyika na sio watanzania!
 
Huu muungano unapaswa kuwa wa kiulinzi tu. Hayo mambo mengine yote piga chini.

Tanganyika ndio itakuwa kama ndio mwanzo inapata uhuru. Maana itawalazimu kwenda kujitambulisha kimataifa kwamba mnaitwa watanganyika na sio watanzania!
Watatuelewa tu kwa kuwa tulitoka kwao. Jamani huu muungano hata kama wanaung'ang'ania kiukweli ni kwamba hautakuwepo.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mbona wabunge wenu wa Zenj wa CCM na CUF walimdhihaki Tundu Lissu? Kiukweli we have put the cart before the horse
 
Sasa ukiyatoa hayo kuna muungano tena? semeni hamtaki muungano mtaeleweka!

Tanzania bara wengi wanashauri kudumisha muungano, Lakini hebu tunaomba Faida na Hasara za muungano ili na wengine tuzijue na tuache tu kusikia.
Haya yakiwekwa wazi kila mtu akajua atakuwa na uwezo wa kuchangia kwa kuzingatia hayo, Sio kama ilivyosasa wengi tunashabikia bila kujua kuna nini humo ndani.
 
But zanzibar ni sehemu ya Tanganyika kwa sheria za kimataifa, wako wapi wanadiplomasia watuambie inakuwaje ardhi iliyo kwenye maji/bahari ya Tanganyika iwe nchi huru, kama ni makosa yalifanyika hulo nyuma turekebeshe mapema
 
The principal is clear never surrender any piece of land, diplomasia ikishindwa, what is neccesary should be done at any cost
 
Barubaru, KVM,

..asanteni kwa marekebisho kwamba wanafunzi wa Tanzania hawakupata kufanya mitihani ya East African Examination Council. nakiri kwamba niliteleza.

..pamoja na ningependa kufanya marekebisho kidogo kwamba NECTA ilianzishwa kisheria mwaka 1973. zaidi, kama mlivyoeleza mitihani ya Cambridge ilisita mwaka 1970. sasa labda tujaribu kuangalia btn 1970 na 1973 mitihani ilitungwa na chombo gani.

cc: Kichuguu, Augustine Moshi, NasDaz, Kitila Mkumbo

Sikumbuki baraza hilo lilianzishwa lini kisheria; ila mitihani yake ilianza kutumika mwaka 1971. Inawezekana mwaka 1973 ndipo sheria ya uundwaji wa baraza ilipopitishwa rasmi bungeni, na in between kulikuwa na interim authority iliyoruhusu baraza kufanya kazi zake chini ya wizara ya elimu
 
Mambo ya muungano ni matatizo ya wanasiasa tu, kwa watu wa kawaida kama mimi muungano wala haunigusi popote pale.Ndugu zetu Wazanzibar wanafikiria kuwa watu wa bara wanau-mind sana huu muungano. Ila nawaomba tu waelewe kuwa kuendesha nchi na hizo mamlaka wanazozitaka itakuwa shughuli kidogo. Hata hiyo mitihani ya Cambridge wanayofikiria sio kazi ndogo wawaulize nchi kama Botswana kwamba mambo ya Cambridge yaliishia wapi.

Perhaps the union was only important when there were threats of coups and instability immediately after Zanzibar's revolution. Right now the focus is more on economic growth where we need patriotic inputs rather than big umbrela of union. It is high time Zanzibaris are left alone and mind on their own economy as well as Tanganyika.
 
kuna changamoto nyingi mno zaid ya elf zinawakabili (old)watanganyika mi nafikiri nyinyi mkae mjipange na changamoto zenu achaneni na mambo ya zanzibar kudai mamlaka kamili sio dhambi pambaneni na mafisadi wenu wanatafuna nchi kila uchao haya mambo ya zanzibar hebu yaacheni msiburuzwe watanganyika nyieee na hapa inaonyeha zanzibar kuna elimu kubwa sana ya uraia kuliko bara hamjui masikini mnataka nini tukipata mamlaka kamili tutakusaidieni kujua changamoto zenu
 
kama hii ni sauti ya wengi huko zanzibar basi wazanzibar wahautaki muungano ila kama haya ni maneno ya watu wachache basi muungano utadumu japo si sana
 
Hakuna sababu ya Muungano wa Serikali tatu watakazotumia kodi zetu za Watanganyika.. kutuongezea mzigo watanganyika wa kuendesha serikali tatu bora Zanzibar tuachane nayo waanze maisha.. hakuna kitu tunanufaika kutoka zanzibar...
 
Hatutaki serikali ya tanzania bara bali serikali ya tanganyika.............. Tume inaficha nini? Kwa nini wazanzibar nao wasitumie serikali ya tanzania visiwani? Wanatuharibia historia


Mimi nafikiri sasa ni kipindi kizuri sana cha jirani zenu kutoka Bara kuanza kufikiria kuchagua Tume yao ya kukusanya maooni ya kuandika Katiba yao ya Tanganyika.

Kwani kama alivyosema bosi wangu Mzee Edwin Mtei tume hii ya Muungano ilijaa vibalaghashia kibao na kazi yake mumeiona.


Sasa hiyo ya Bara ambayo iliyojaa wenzenu itakuwaje? au ndo zile za Mou.
 
chabuso,

..data zangu nimezipata UN kwenyewe. bofya hapa United Nations member States - Growth in United Nations membership, 1945-present

..kwani wewe data zinazosema Tanzania inatumia kiti cha Zanzibar umezipata wapi?

..hivi una uhakika kama serikali ya Mapinduzi, ilishateua balozi wake kwenda kuiwakilisha UN??

..kuna mambo mengi sana yasiyo ya kweli yanasemwa kuhusu Tanganyika. Jaribu kuyahakiki mambo hayo kabla hujayaamini.




cc: Nguruvi3, GHIBUU, kibungano, Nonda


JokaKuu kama unajua kin'gen'ge mambo hayo,ukweli ulio wazi



Bendera ya Kenya na Zanzibar zikipandishwa kwa mara ya kwanza UN baada nchi mbili hizo kujiunga na United Nation


Dunia imekua ndogo kwenye ukweli oungo hujitenga 😉

Hapo hamna mwanarabu,Tumeambiwa serikali iliyopinduliwa ilikuwa ya mwarabu,lakini hapo sioni mwanarabu hao walikuwapo hapo ni wazanzibar wenye asili ya Kiafrika kuanzia waziri mkuu na wafuasi wake........
 
Last edited by a moderator:
chabuso,

..mimi nimekuonyesha kwamba Tanganyika ilikuwa mwanachama wa UN in 1961.

..Zanzibar ilikuwa mwanachama wa UN in 1963. tena nyinyi mliwatungulia hata Oman ambao walipata uanachama in 1971.

..data nilizokuletea nimekupa mpaka link ya UN wenyewe.

..what more do u need ili kujiridhisha kwamba Tanganyika ilikuwa mwanachama wa UN kabla ya Zanzibar, Uganda, na hata Kenya??

..madai kwamba kiti cha Tanzania UN kilikuwa cha Zanzibar siyo ya kweli. Ukweli ni kwamba nchi hizo ziliunganisha uanachama wao baada ya muungano.
 
Last edited by a moderator:
kuna changamoto nyingi mno zaid ya elf zinawakabili (old)watanganyika mi nafikiri nyinyi mkae mjipange na changamoto zenu achaneni na mambo ya zanzibar kudai mamlaka kamili sio dhambi pambaneni na mafisadi wenu wanatafuna nchi kila uchao haya mambo ya zanzibar hebu yaacheni msiburuzwe watanganyika nyieee na hapa inaonyeha zanzibar kuna elimu kubwa sana ya uraia kuliko bara hamjui masikini mnataka nini tukipata mamlaka kamili tutakusaidieni kujua changamoto zenu
Ndio watu wanapambana na ufisadi wenyewe.
Bilioni 32 zinapochotwa kupelekwa znz bila sababu ni ufisadi.

Kutoa umeme watu wasiolipia ndio ufisadi.
Kufidia bajeti kwa bilioni 500+ kwa mzanzibar ndio ufisadi.
Kusomesha watoto wa znz bure kwa gharama za Watanganyika ndio ufisadi.
Kuwapa ajira wznz kwa kigezo cha uznz na siyo sifa ndio ufisadi.

Kuongeza serikali ya muungano ambayo znz haiwezi kuiendesha hata kwa mwezi mmoja ndio ufisadi.
Kutoa nafasi za uwiano katika mambo bila kuchangia sawa ndio ufisadi.

Kumlipia mznz ulinzi akiwa amelala bila yeye kutoa gharama ndio ufisadi.

Kwahiyo Watanganyika wanapambana na ufisadi sasa hivi, hao wamnaobia bilioni 2 ni wachache kuliko wale milioni 1 wanakwapua mabilioni kwa jina la muungano.

Unachokiona hapa ndio mapambano ya ufisadi, kwani unadhani ufisadi ni upi tena?

JokaKuu, Ghibuu, Jasusi,Kichuguu
 
Back
Top Bottom