Alichokisema Lema ni sahihi kabisa, ugali pia unadumaza akili

Alichokisema Lema ni sahihi kabisa, ugali pia unadumaza akili

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Alichokisema Lema hakina tofauti na alichowahi kusema Alfredo Bowman aka Dr Seby (huyu dr alivumbua tiba nyingi za asilia C.I.A wakamfyeka) kuhusu Ugali

Dr Sebi alishawahi kusema kuwa Ugali sio nzuri hata kidogo unadumaza akili na ni chakula.cha kimasikini kabisa kutwa kucha ugali wa dona akili utazitoa wapi?



Ndo maana jamii zinazokula Ugali Asubuhi, Mchana na usiku siku 7 za wiki, bila kubadilisha lazima hyo jamii iwe na IQ ndogo tu

Ukitaka kuamini, angalia jamii au familia wanazokula mixture yaani hawali ugali sana wanakula
viazi, ndizi, mihogo, samaki, nyama, dagaa, ngano, mchele, mboga, maziwa wadudu mfano senene na kumbikumbi wana IQ kubwa sana tofauti na jamii wanayotegemea ugali tu muda wote na hakuna chakula cha mbadala

Ugali unadumaza akili na sio chakula cha maana hata cha kujivunia hata kidogo, msisahau kuwa ugali wa mahindi sio chakula cha asili cha Mwafrika msisahau mahindi pia yaliletwa na mreno sisi tukadakia tu

Mimi binafsi huo ugali unaliwa mara chache tu nyumbani kwangu hili nililijua mapema sana sio chakula cha kukipa kipaumbele hata kidogo.

Lema yupo sahihi kabisa, maskini wengi ndo wapenda ugali maana hawana mbadala

=======

 
Alichokisema Lema hakina tofauti na alichowahi kusema Alfredo Bowman aka Dr Seby (huyu dr alivumbua tiba nyingi za asilia c.i.a wakamfyeka) kuhusu Ugali
Usitupangie,tutaendelea kula ugali kwa wingi mpaka mwisho wa uhai wetu.Sehemu ambazo watu wanakula ugali kwa wingi hakuna ushoga,kudeka deka na upumbavu pumbavu.
 
BAVICHA ukweli unaowauma huwa hawazungumzi kabisa, tukiwaambia Tanzania uchumi wetu unakua kuliko wa Marekani watakushambulia mbaya lakini mambo mengine wanapenda ku-compare.
 
Alichokisema Lema hakina tofauti na alichowahi kusema Alfredo Bowman aka Dr Seby (huyu dr alivumbua tiba nyingi za asilia c.i.a wakamfyeka) kuhusu Ugali
Wewe ni muwongo sana tena sana. Usiombee kupokea Mayai viza.
 
Pia ugali hauliki mfano Mimi ghetoni kwangu nanunuaga kg 20 mchele na kg 5 unga lakini unga unakaa miezi mitatu Hadi minne na mchele mwezi mmoja na nusu .
 
Mkitoka kwenye ugali,hamieni kwa sisi watembea kwa miguu

mkitoka huko,njooni tena kwa sisi tuiopanga mkimaliza huko

rudini kwa sisi tunaofanya biashara zamitaji ya 5000 kisha malizieni

na sisi tunaokunywa maji ya kandoro,nadhani bado mna mengi endeleeni.

ila Kaeni mkifahamu jambo 1 Watanzania wa sasa unaweza waona kama majinga

ila huwa hawakoseagi kwenye kupiga kura yani utacheka naooo,mwisho anajua yupi Fala yupi Zimo.
 
Ugali ni mboga,
Leo ugali samaki
Kesho ugali nyama
Kesho kutwa ugali dagaa na mboga mboga
Inayofuata ugali kitimoto
Ya tano ugali maziwa mtindi
Ya 6 ugali kuku
Hapo ni mchana jioni kitapikwa kingine, jumapili kitapikwa tofauti
 
Ungedumaza akili tungepata watu wa kubeba kibox chote cha pesa ya Tz kama Mtei, Mramba na wengine? Ni kazi inayohitaji utumiaji wa ubongo. Ubongo uliodumaa ungeweza??
 
Back
Top Bottom