Alichokisema Rais mstaafu Kikwete kuhusu Sukari na Umeme

Kwa hiyo amesema wananchi wakikosa umeme,maji,sukari nk ndiyo inaonyesha ushupavu wa kiongozi aliyeko madarakani siyo? Kwa hiyo nchi ikiwa na umeme wa uhakika,maji ya ugakika na sukari ya kutosha itakuwa kiongozi aliyeko madarakani ni goigoi siyo? Aisee sasa tumeelewa lengo la ccm kungangania madaraka, so bad Lucas mwashambwa
 
Wakati kilio cha mgawo wa maji na umeme, na uhaba wa sukari kikiendelea nchini, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwa imara anapoendelea kutafuta suluhisho la changamoto hizo kwa kuwa ni mambo ya kawaida kwenye uongozi.

Kikwete amesema anachoonyesha Rais Samia katika kipindi hiki, kinadhihirisha ushupavu wake katika uongozi, akieleza changamoto ni sehemu ya uongozi na utulivu wake unawafanya wananchi pia kuwa watulivu.

Kauli ya Kikwete ameitoa katika kipindi ambacho kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa umeme, maji na sukari, ambayo bei yake imepanda maradufu.

Credit - Mwananchi
Hakuna mstaafu chenga tu.umeme kwa sasa sio changamoto ni janga la Taifa.Halafu kutwa kucha wapumbavu wanamsifia Samia upuuzi wa hali ya juu kabisa.
 
HahHa mstaafu aliyegoma kustaafu
 
Wakati kilio cha mgawo wa maji na umeme, na uhaba wa sukari kikiendelea nchini, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwa imara anapoendelea kutafuta suluhisho la changamoto hizo kwa kuwa ni mambo ya kawaida kwenye uongozi.

Kikwete amesema anachoonyesha Rais Samia katika kipindi hiki, kinadhihirisha ushupavu wake katika uongozi, akieleza changamoto ni sehemu ya uongozi na utulivu wake unawafanya wananchi pia kuwa watulivu.

Kauli ya Kikwete ameitoa katika kipindi ambacho kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa umeme, maji na sukari, ambayo bei yake imepanda maradufu.

Credit - Mwananchi
Kikwete muulizeni kwanza kama yeye ananunua Sukari bei hii tuliyonayo wengi!
Je anazimikiwa umeme na kuharibikiwa vyakula kwa Friji?
Ananunu mafuta ya Gari yake?
Hayo tu!
 
Mzee ameona atoke vipi kubadili upepo wa maneno ya msiba wa ENL
 
Back
Top Bottom