Alichonifanyia huyu mama Ubungo stendi ya mabasi sio uungwana

Alichonifanyia huyu mama Ubungo stendi ya mabasi sio uungwana

Pamoja na wema wako, muda mwingine usifanye huo wema mtu humjui unajipa majukumu ya kukaa na mtoto wa mtu, uongozi wa hiyo kampuni ya hilo bus ulipaswa kufanya hilo jukumu. Lingetokea la kutokea?? Dunia haiko hivyo kama tunavyofikiria.
Umeongea point sana,mana lingetokea la kutokea ingekua ndo msalaba wake huo.
 
Nimeishia alipotamka atashukia mqosho wa gari Ubungo.

Daaj uongo kazi
ukiacha mbezi pale ndo zilipo ofice za mabasi mengi ya mkoa, na ndo zinapoanza na kumaliza safari zao pia.
 
Hi
Sikuhitaji anishukuru wala sikuhitaji anilipe hapana ila mikausho aliyo nionyesha kwa kweli ameninyanyasa kihisia

Nilikua natoka Mwanza nakuja Dar niliwahi mapema sana kufika pale ofisini kwao yanakolala magari panaitwa Nata nikapanda nika kaa kwenye seat yangu ilikua msitari wa tatu kutoka mlango wa kuingilia na abiria wengine wakaingia sasa kuna dada mmoja kaingia akiwa na mtoto wa kiume mwenye umri kama miaka kumu hivi wakatafuta seat yao wakaipata

Kumbe seat yake ilikua pamoja na mimi basi yule dada akaniuliza samahani kaka unashuka wapi nikamjibu nashuka mwisho ubungo yule dada kanikabidhi yule mtoto eti nimfikishe ubungo atapokelewa na mzazi wake na akanipa namba yake na namba ya mama wa huyo mtoto ambaye anatusubiri ubungo

Chuma ikaondoka ikapitia stendi kuu ya mabasi Nyegezi ikakusanya abiria wengine ilipofika saa 06:00 AM chuma zikaruhusiwa zikaanza kuikata mikoa kuitafuta Dar sasa huko njia yule mama ambae yuko Dar anasumbua kwenye simu kibaya zaidi ana beep mimi ndio nampigia anauliza mmefika wapi namueleza tuko sehemu fulani anatulia baada tena ya saa moja ana beep tena nampa maelezo yote tulipo fika mara abeep napiga anataka kuongea na mwanae okay sio mbaya nampa simu anaongea na mwanae

Sikuweza hata kumnunulie dogo snacks sababu alikua anatapika kichefu chefu kinamshika mara kwa mara hata tulipo fika pale singida hotelini msosi alio nunua hakumaliza tumekuja mpaka giza linaaza kuingia bado hatujaingia hata Moro town yule mama bado ana endelea kuuliza tumefika wapi nampa maelezo yote tulipofika anatulia mpaka tunaingia Dar saa 23:58 PM
Mpaka tunaingia stendi ananiuliza namwabia ndio tunaingia stendi bus tuliomo sisi ni Zuberi no2 chuma kimetafuta sehemu kika park vizuri abiria tukaanza kushuka nikampigia ndio tunashuka akasema haya na mimi niko hapa hapa tumeshuka huku dogo nimemshika mkono dogo kaniponyoka bwana kamkimbilia mama ake wameonana wana kumbatiana nikawasogelea nikasubiri wakumbatiane wamalize ili niwaage kua mimi naenda mwanao usha muona maana mmenikabidhi inabidi na mimi niwakabidhi

Huwezi amini yule dada namemkaribia namsalimia kajikausha nikajua hajasikia nikaongeza sauti nikasalimia tena kanisikia hajaitikia kaniangalia alafu kanipotezea nikaona isiwe tabu niwaage mimi niende haya mimi naenda kimya hakuna hata mmoja alie nijibu nikaondoka zangu nimefika home nimelala kesho nampigia simu yule dada wa mwanza alie nikabidhi mtoto ili nimjulishe kua mtoto alifika kwa mama yake salama yule dada wa mwanza nae pia hapokei simu

Sijui ni kabila gani watu wale
Aisee!, Pole sana.
 
Tunakupa pole na pia tunasema endelea na mambo yako wengine wameenda mbali wakaweka na lugha ya malkia eti (Mind your own bussiness).

Ndugu zangu naungana nanyi pia kutoa pole ila niwakumbushe kuwa huyu ndugu haitaji pole tu ila kuponywa saikolojia yake maana mpaka hapo ameathirika vibaya.

Sasa nakutibu rafiki.
Kwenye saikolojia kwa hiko kitendo kuna kitu tunaita misexpectation yaani unategemea A ila inakuja B

Rafiki najua ulitegemea waseme asante hata ya mdomo pasipo chochote ila haijawa hivyo na mwisho ukaathirika kisaikolojia na pia ukajikatia tamaa kwa lile dogo ulilofanya

Sasa ili ukae sawa , tafuta sehemu kaa mwenyewe kumbuka ni mangapi uliwahi wadispoint watu waliokutendea wema ila walikusame na maisha yakaendelea ( usiniambie hukuwahi kumdisappoint mtu )

Chukua muda mwingi kuyakumbuka hayo uliyowadisappoint watu walau lisaa kumbuka kila moment then kaa kumbuka ulivyotoa msaada kwa hao wadada mwisho utajihisi amani ya moyo.

Ni hapo utasema wacha yapite , nakuhakikishia within a week hata ukilikumbuka hilo utaona kawaida.

Pole embu tibika kwanza.

Tanzania my country.[emoji120]
 
Mambo mengine unakausha tu mura sio kila kitu ni cha kuweka kwenye mtandao
 
Back
Top Bottom