Rais Dr Magufuli alikubali uwepo wa corona, ilipoingia nchini alichukua hatua za awali za kupambana nao kama muongozo ukiotolewa na WHO na Africa CDC.
Baada ya muda akaongeza njia zake na kuachana na miongozo ya hizo tasisi kubwa na tukatumia maombi ya siku 3 na nyungu ambapo ndani ya siku chache hizo njia zilionyesha "mafanikio" makubwa na tukaambiwa ugonjwa haupo, japokuwa wapo watu walipata maambukizi kipindi ambacho tulikuwa tunafurahia "mafanikio" hayo na wapo waliopoteza uhai, lakini tulifanikiwa kuishangaza dunia kwa "kuidhibiti" corona na kuendelea na maisha kama kawaida bila tahadhari yoyote.
Mpaka January 27/2021 ambapo kulikuwa na mfululizo wa vifo vinavyotokana na matatizo ya mfumo wa upumuaji ndipo alikiri kuwa "corona haijawa kubwa na haipo, ipo chache sana".
Kinachoshangaza serikali ya sasa inasema tupo wimbi la tatu, na wimbi la pili lilituathiri kuliko wimbi la kwanza lakini hatukuwahi kuambiwa wimbi la pili limeanza lini na lilileta athari gani kwa maana kulikuwa na magonjwa mengine yaliyoathiri mifumo ya upumuaji na sio corona.
View attachment 1897791