Alienishauri kufungua biashara ya video production ameniingiza chaka

Alienishauri kufungua biashara ya video production ameniingiza chaka

Kabisa yani.

Maana mtu ana issue Yake anataka kushoot umwambie alipe laki moja wakati wakati kwa simu yake anashoot kazi zote na anazipata kwa wakati
Mwenye issue anacapture vipi matukio yake mwenyewe? Anakuhitaji wewe kuyacapture. Fanya marketing vizuri.
 
Nakubaliana na wewe. Ila wanasema naturally kila binadamu anapenda mambo ya camera na picha
Ili ufanikiwe inabidi upende hicho kitu unnatural way. Yaani upende masuala ya camera, fashion, editing, event planning and decor, kujua make-up vyote hivyo uvijue isivyo kawaida. Na uwe social.

Ukijua kwa kawaida sasa unakuwa kama watu wengine, ili uwe Sheikh mzuri lazima uijue Quran kuzidi kawaida, usijue Quran kwa vile "naturally kila Mwislamu anajua Quran".

Lazima service provision iendane na interest na kipaji. Sio hujui kupika alafu unaanzisha catering services au au mgahawa. Unaowaajiri wakiharibu hujui.
 
Kweli aisee 📌
 
Ukiwa mbunifu huko kwenye content creator utapiga pesa,

Idea zipo kede wa kede.
 
Thank you
Duh yani imebidi nianze tu kufanya content. Nimelazimika kuwa content creator
Ungekua MC angalau ingekusaidia ila mjini bila connection na uwajibikaji tenda utazisikia tu kwa wenzio.
 
Video Production yako una vifaa vipi na vipi labda tunaweza kukushauri
 
Zingatia vitu hivi...
1. QUALITY
Vifaa unavyotumia vinaendana na usasa? Siwezi kukupa tenda kama simu yangu inachukua video zenye quality nzuri kuliko camera yako. Why not just use my phone for free? (It's just a simple logic)

2. STYLE
Hakikisha kazi yako inakua ni enye utofauti yaani unique, Wengi wana vifaa vya kisasa lakini style yako ndio itaamua upige pesa zaidi ya wenzako.

3. CONSISTENCY
Usikate tamaa mapema, kua consistent.

4. MARKETING
Nobody knows you until they know you. Unaweza kuwa na vifaa vya kisasa na style kutoka mawinguni, but if Nobody knows you ni kazi bure!! bora ujifungie chumbani ufanye video za make-up.
 
Kuna watu wanapiga ela kwenye hii kazi tuliza akili
Yes hii kazi ina hela ila inahitaji akili nyingi maana ina ushindani mkubwa. Na asilimia kubwa ili kutoboa lazima uingie front.
Sasa kama umeajiri vijana umekaa ofisini unasubiri wateja wakufate utume vijana aloooh utapaukaaa! kwanza vijana hao hao ndo wanakuzunguka kukuibia wateja 😂🤣
Ushauri wangu kwa kuanza kubali hasara fanya hata free event mbili tatu nyoosha kazi then zitumie kujitangaza,also jitahid sana kupost on social media na kufanya promotions za kutosha kujenga jina.
 
Hio biashara inahitaji ubunifu na kujituma ila inalipa sana ukipata team sahihi na wateja sahihi. Komaa piga kazi ndani ya miaka mitano utanishukuru
 
Back
Top Bottom