Bueno
JF-Expert Member
- Aug 16, 2022
- 34,600
- 59,760
UtanitagITAENDELEA NA ITAKUWA FINAL EPISODE IKIWA NA MAJINA MA KILA KITU
UtanitagITAENDELEA NA ITAKUWA FINAL EPISODE IKIWA NA MAJINA MA KILA KITU
Kazi unayo...utasumbuliwa hadi kweny PMDuh,
Hatimae nimeelewa.
Ipi?Mbona sehemu ya tatu imefutwa?
Soma tenaMbona sehemu ya tatu imefutwa?
Aseee sikujua kama kuna movie hapa, britanicca tag me on every episodeNi jumapili Nyingine ambayo imejaa utulivu wa aina yake, ni miezi kadhaa imepita Mrembo ambaye ntampa jina la NISHA, Ambaye alitumwa kwa kazi maalumu kutafta Nywila kwa Boss Ambaye nitamuita SASHA,
Ikatangazwa kazi na Kampuni fulan maarufu hapo nchini, lengo ni njia ya mwanadada NISHA toka Nchi ya jiran kwa wafugaji ili apewe kazi kwa maelekezo maalumu akisaidiana na mmoja wa wapelelezi ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye taasisi kubwa ya kupeleleza ambayo kwa jina kwa uzi huu ntaiita TWISHI,
Huyu Dada mrembo mrefu mithili ya twiga alikuwa amemaliza masomo yake nchini Urusi ila alikuwa anatumia Passport ya nchi ya boss SASHA, kabla ya hapo dada alishawahi fanya matukio mawili makubwa, miaka kadhaa kabla hajaenda Urusi alikuwa na genge lake la wadada ambao walidukua taarifa kutoka kwenye laptop ya waziri wa nchi hiyo hiyo akiwa hotelini.
View attachment 3055291
kabla NISHA au genge lake halijatekeleza jambo uwa wanahakikisha wanapata usaidizi toka kwa mamlaka za viongozi vijana waliozaliwa miaka ya 1970, mmoja alikuwa kwenye ngazi ya kuhakikisha mpango unasukwa vizuri, wasiweze kupatikana kwa kuwa tracked, hata malipo yao ni cash siyo benk au mobie money,
Kazi inaanza sasa ,
NISHA anaamka asubuhi kuelekea kuanza majukumu akiwa na gari aina ya lexus, anaingia getin kama kawaida, anakaguliwa kila kitu, anaruhusiwa, wakati wa kuscan kuna kitu kilionekana ila walinzi walipuuzia kwa kuwa alikuwa ana ingia mara kwa mara na vipodozi na na perfume kama wanawake kawaida yao ilivyo, kumbe mle kwenye beg ana posionous perfume, na unga wa sumu wa kupakaa kwenye viti na faili lolote atakalogusa SASHA.
Alibeba aina 5 za sumu, kuna ya kupuliza, kuna ya kuweka kwenye kinywaji, kuna ya kumfanya asinzie, sumu hiii si ya kuua kabisa ila inadhoofisha mtu hadi kushindwa majukumu yake makubwa ndani ya muda mfupi yaan kwenye miezi miwili mtu nywele zinakuwa zimenyonyoka na kuisha kabisa, na mwili unavimba sana kupita kiasi,
akaingia kwenye majukumu akisubiria kwenye ofis ambayo lazima SASHA aingie, na alipea mashart kama anapuliza ndani awahi kuondoka eneo husika ili naye asidhulike maana unapopuliza ukawai kupata dawa ya kukuondolea madhara ndani ya nusu saa haudhuliki, ile ya kumwaga kwenye mafaili, ilikuwa ni kama kupuliza ineshindikana,
NISHA akiwa na wadada wengine wawili wanamwambia katibu wa SASHA kwamba kuna ujumbe muhimu wanataka kuonana naye, kama kawaida katibu ananyanyua simu kumpigia SASHA anapokea
Basi SASHA katika Mazungumzo akaruhusu wakaingie kumuona, NISHA anagonga kifua kwamba dili limekamilika vya kutosha hapa, na ile mpango wa vijana wa miaka ya 70, imekwiva sasa , na hitavuruga ratiba ya kuwa Mabosi kama yeye,
NISHA akanyanyuka kuelekea ofisi ya SASHA , Anafunguliwa mlango,
INAENDELEA hapa Mwendelezo: Alikataliwa kabisa kuingia, baada ya miezi ndio wakajua ni mwenyewe, usidharau mtu (2)
Sio Zuu kweli..??To me NISHA ndo code ngumu kuing'amua
Huyo ni agent si lazima awe mtu mkubwa tunayemjua sana. Tutafute ni mbongo gani mwenye asili ya Rwanda (ambaye ni Rwandese ila anatumia passport ya Tanzania akijifanya mbongo). Ambaye somehow sio myonge mpaka anapanga appointment na Rais, ila pia alipewa kazi si muda mrefu kwenye wadhifa fulani au cheo fulani hata kama ni private sector. TafutaTo me NISHA ndo code ngumu kuing'amua
Kisha akafutwa kazi kabla ya ramadhani 😂Huyo ni agent si lazima awe mtu mkubwa tunayemjua sana. Tutafute ni mbongo gani mwenye asili ya Rwanda (ambaye ni Rwandese ila anatumia passport ya Tanzania akijifanya mbongo). Ambaye somehow sio myonge mpaka anapanga appointment na Rais, ila pia alipewa kazi si muda mrefu kwenye wadhifa fulani au cheo fulani hata kama ni private sector. Tafuta
Hadithi Tamu lakini.Baada ya MASUDI kufika kwa katibu na simu ikapigwa kwa SASHA, kwamba wana jambo Muhimu la kumueleza Huku sauti ikisikika Kama kuna jambo haliko Sawa, ikabidi amuambie BEGA wa kushoto kwamba mwambie NISHA anisubirie nje kidogo, alitahamaki badala ya kumweleza yeye kwakuwa wamekaa wote Ila alimweleza BEGA WA KUSHOTO amwambie NISHA,
Baada ya NISHA kutoka nje zikaanza serious screening kwa kila aliye pale na wakakuta NISHA Ana Vimiminika kadhaa Kama ambavyo MUHA alikuwa kasema, ikabidi aitwe MUHA, na watu wa Ulinzi akawekwa mtu kati, jambo ambalo halikutegemewa SASHA akafichwa kutokana na protocol husika, na uwajibishwaji wa aina ile si wa mchezo,
Watu wa TWISHI wakamchukua wakamuweka mtu kati NISHA na MUHA,
MUHA nahojiwa amepata wapi taarifa zile ? Lakin pili wakemia wakalazimika kutumika kujua nini NISHA alibeba, ikathibitika pasina Shaka kwamba ni sumu kutokana na ingredients zake,
TWISHI kupitia KITUO CHONGEO wakambana sana NISHA kaanza kufunguka japo ilichukua muda sana kusema ukweli,
Ikagundulika Tarehe ** 024 Mbele ya Tawi la Benk ya NNAMDI ilipaki gari landcruiser prado yenye namba T* D*** ikiwa na MABENDERA ni mzee wa makamo ambaye pia alikuwa ni msaidizi wa SASHA kwenye ukanda wa South Afrika wala si Madagaska na Huyu amehusika zaidi aliitwa mabendera kisa meli zote zilizokuwa zinasafirisha nyusi za Sungura Kimagendo Kwenda ngambo alikuwa anaweka bendera za south Afrika yake, wakati nchi haijui, na ni Kama mshauri wa vijana wa 70,
Basi Waliletewa bahasha kubwa maana hawapokei kupitia benki, na huo mzigo ilikuwa kwa ajili ya kutekeleza Suala hili,
Wakagundua kwamba si wavulana wa miaka ya 70 tu wanaotaka wanayotaka bali nyuma kuna mkono wa Mkuu wa wale wa TWISHI, na Baadhi ya wafanyakazi wa ofis ya SASHA,
Ikaandikwa report uchunguzi ukaendelea huku NISHA akiendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi, nini hasa lengo la kufanya hivo,
MUHA alihojiwa na maelezo yote alosema ni Kama ambavyo walipata kwa NISHA kwa kumtega asilimia 60 yalioana,
Ikabidi sasa mzee yule afuatiliwe kwa kina kabisa kabla hawa hawajapeleka faili kwa SASHA, katika kufuatilia zaidi Hiyo ya sumu ilikuwa cha mtoto
Kuna mbinu ambayo ilikuwa imepangwa kabla ya Moon mtufuku wa Mazaran mtu awe kaondoka kabisa, si kubaki hai bali akawahi matendo ya watesalonike,
Ikabainika huyo mzee MABENDERA mtandao mkubwa sana sana ambao upo hata pale pale kwa ofis ya SASHA , ikabidi wananwe zaidi wakatajwa watu wengi katribani miezi 3 sasa NISHA Kataja orodha ya watu 12 wanaojua na kuhusika na mpango ule na orodha itawekwa,
Baada ya kubanwa zaidi ikabidi NISHA awapeleke kwenye vikao wanapogifanyia na huko ndo orodha itatajwa,
Akawekwa kwenye gari wakaelekea kwenye Ukanda Magaribi ushoroba, wakawa wanaelekea Kwenye kwenye gari Simu ya NISHA ambayo wameishika ikaita Kama Mara Tatu na namba inayopiga si namba Kama tunazotumia Sisi wakamsogezea NISHA aongee,
Simu kupokelewa ikakwekwa Loud speaker
Maongezi kuanza kumbe sauti ni ya ………..
ITAENDELEA NA ITAKUWA FINAL EPISODE IKIWA NA MAJINA MA KILA KITU ,
Kwa kusaidia tu kituo cha chongeo kituo cha upanga mabaka baka 😂Nmeambulia tu meya wa sauz alietokea Madagascar
Uzi hautembei kabisa 😄SHIDA NINI MODS?
NaamTupo hapa
Haah kwaniniUzi hautembei kabisa 😄
Sawabritanicca naomba utanitag mkuu
Usitoke sifuriNimetoka sifuri.