Alikiba ameshinda Mtv Ema lakini hakustahili zaidi ya Wizkid!

Alikiba ameshinda Mtv Ema lakini hakustahili zaidi ya Wizkid!

Angelalamika Mtu tofauti na ALLY KIBA au tofauti na TEAM KIBA ningeshangaaa!! Kwa kua ni hao hata sishangai ni kawaida yao!!!! Lini MT VEMA walipost kuwa Kiba anaongoza kwa kuraa?

Hata watanzania wote million 45 tungepiga kura kwa kura za wanigeria tusingefikia!!! Tuache kukurupuka na Post za kutengenezwaaaaa!!! Labda mlete ushahidi ambao unaonesha walipost kiba anaongoza

Ujue Diamond atabaki kuwa wakimataifa kutokana hata anaVo jibehave! Niwakumbushe mashabiki wa ALI KIBA! Diamond aliwahi wekwa katika kipengele fulani cha kupigiwa kuraa,watanzania walimpigia kura Diamond hadi upigaji kura ulisitishwa kwa muda kutokana na wingi wa kura na wao wakasema wanashindwa kuhesabu lakini mambo yalivyo kaa sawa hicho kipengele Diamond HAKUSHINDA! Tuzo akachukua mwingine lakini Diamond hakulalamika hata Robo kikubwa aliwataka mashabiki watulie na wafurahie kuwa nominated tuu ni ushindi tosha Mungu si adhumani mwaka unao fuata aKachukua tuzo!!!

Mjifunze kukubalii Kiba ni nani? Who is kiba in Afrika? Wizkid kafanya Show ngapi na za ukubwa gani?, alikuwa anaperfom vipii watu wanamuitikio kiasi gani?

Acheni ujingaaa.....Nje ya Tanzania Kiba show ya pekee ake Kafanya ngapi? Watu walikuwaje na wapi??? Semeni au hata Tanzania semeni kiba Kafanya show Ngapi hapa Tz? Mnalalamika bila Facts msanii wenu kutwa yupo K/koo halafu mnataka mchukue tuzo za mtumbuizaji bora mnadhani hizo ni KILL AWARDS?

Wizkid kafanya show kazunguka Africa.....kumbukeni Diamond aliwahi kuchukua hiyo tuzo kwa wingi wa show alioufanya mbele ya wizkid hadi show zaa kwenye CCM zilikuwa zinaangaliwa,nigeria alifanya maara kibao!!

Kumbukeni mashabiki wa kiba kuwa nominated sio unajua sanaaa au unastahili sometime unawekwa ili kunogesha tuu tunzo hizo!!!!

Shame on You kiba Fans!
Duh Watanzania tuna kazi kubwa na huu uteam, kumbe povu lote hili unamtetea mnigeria kwa vile uteam kwako ni zaidi ya utaifa!!
 
Chaaa, ww ndiye unapotosha,,kulikuwa na category nyingi ikiwemo 'winners category 'na siyo 'wenye Kura nyingi'kama unavyosema,, kuweni wakweli hata Mara moja tuu,, mnabadilisha story simply because mna chuki na ali
Hakuna alichopotosha alichosema ni kweli... kwenye website hawakutangaza washindi bali walionesha wenye kura nyingi... utaratibu wao ni kwamba, mshindi anatangazwa officially! Na utaratibu wa MTV upo wazi kwamba baada ya zoezi la upigaji kura; kura zitakuwa tabulated na MTV EMA na mshindi KUTANGAZWA! MTV Hawa hapa:

"In this phase you will be able to vote for the Best Local Act nominees in any participating country/local region. Local winners from each country/local region will be announced online on 6 November 2016...!" Na kweli, wao wakamtangaza mshindi tarehe 06 kama walivyosema wenyewe!
Wiz.png


Tusaidie wewe sasa... ni wapi Kiba alitangazwa kwamba mshindi?!

Na siku hiyo hiyo wanaofahamu haya mashindano yanaendeshwaje, wakatoa pongezi kwa WizKid hata kama wana uhusiano wa karibu na Kiba compared to Wiz:
Sauti.png


Kinyume chake, hayo ma-screenshot mnayoyasambaza ni ya tarehe 07 wakati winner ameshatangazwa tangu tarehe 06! But simple question... hivi kila siku awe anaonewa Kiba peke yake?! AFRIMMA anahujumiwa yeye! Kwenye show za Mombasa, anahujumiwa yeye! MTV nao wanamhujumu yeye! Ndo vile bado hajawahi kupata nomination BET... huko nako mtalia lia vile vile kama mlivyokuwa mnalia lia kwa kutopata nomination!!!
 
Hakuna jambo linalonikwaza Kama watu kusema Ali anapenda kulalamika,hana uwezo, ,, kwani hamuoni utata uliopo?? Kila aliyeshinda aliwekewa pink mark,,
Mshindi hawekewi pink bali ANATANGAZWA!!!! Ali Kiba hakutangazwa popote kwamba ni mshindi!
mtvbaseafrica (siyo mtvema)wakampost wizkid!
Hoja nyingine ya Team Kiba... mnadhani ni MTV EMA ndio walikuwa wanapaswa kutangaza mshindi wakati regional winners wanatangazwa na regional MTV Channels na sio MTV EMA kama mnavyodhani!
Mshindi waDenmark huyu hapa... hakutangazwa na MTV EMA bali na MTV Denmark na wao MTV EMA waka-RT announcment:
Denmark.png


MTV ESpan hawa hapa na ndio alimtangaza mshindi wa Spain na wao MTV EMA wali-RT tu!
Spain.png



Ni MTV Netherlands ndio walimtangaza Mshindi wa Netherlands na MTV EMA wao wali-retweet tu matokeo yaliyotangazwa na MTV Netherlands!

Dutch.png

Na washindi karibu wote, ndivyo ilivyokuwa! Kwahiyo hoja yenu kwamba MTV Base walim-post WizKid badala ya MTV EMA ni hoja isiyo na nguvu!
Hapa fans WA alikiba wakaanza kulalamika, mtvema walipoona malalamiko yamezidi na fans wana ushahidi walichofanya(mtvema) ni kuhamisha ile pink mark ya ushindi na kuipeleka kwa wizzie,,, hapo ndipo fans wakazidisha complains, haikuchukua muda mtvema haohao wakaondoa ile pink mark kwa wizzie, hivyo kwenye hii category ya bestafrican act haioneshi mshindi ni Nani mpaka sasa!!
Yale yale... haioneshi mshindi ni nani wakati mshindi alishatangazwa! Na katika Stanadard Voting Rules za MTV EMA hakuna popote waliposema mshindi atawekewa alama kuonesha ushindi bali kura zitakuwa tabulated na mshindi KUTANGAZWA! Hakuna popote ambapo Kiba alitangazwa!
Swali langu ni je??? Mtvema wanaweza fika mpaka stage ya kumueka alikiba kwenye website yao Kama mshindi KABLA hao mnaowaita majaji na wadhamini hawajaverify ushindi wake!??? Nyie mnachukulia hili swala kiushabiki lakini mnaacha kuangalia utata uliopo.
Hawakuweka popote kwamba mshindi bali walionesha wanaoongoza! Baada ya zoezi la upigaji kura kwisha, ndipo kura zinakuwa tabulated na wao MTV EMA wanatangaza mshindi!! Mshindi anatangazwa! Na endapo wanaona anything suspicious, wana mamlaka ya kupiga chini zoezi la kura na kutangaza mshindi kama wanavyoona wao!

If, for any reason, this voting process is interrupted for any reason, is found to have been tampered with in any way, or for any other reason that MTV EMA believes in its sole discretion to be reasonably necessary, MTV EMA reserves the right to select the winners at its discretion....!

Mssiwe mnakurupuka wakati hamjui taratibu! Hata Kiba alisema kwamba wanafuatilia kufahamu vigezo hii ni kituko kwavile kila kitu kilikuwa wazi from day one! Na MTV EMA waliweka wazi from Day One kwamba:

"By participating in this voting process, you agree to be bound by these How Voting Works For The 2016 MTV EMA rules. Failure to comply with these rules may result in a voter's disqualification solely at the discretion of Sponsor. Sponsor reserves the right to modify these How Voting Works For The 2016 MTV EMA rules at any time in its sole discretion."
 
Kwa mujibu wa iyo post kiba hakushindwa,kashinda ila tuzo kapewa mwingine kwa vigezo vilivyobuniwa siku iyo ya ugawaji tuzo
Ajifunze kukubaliana na matokeo,sio Tuzo zote kuamgalia idadi ya wapiga kula,lakin pia kwa mfano hio ya AFRIMA KAMA kula zako zote zinatoka kataifa kako tu hawakupi,inatakiwa kuwepo Msambazo wa kula kuwa karbu sehem ya kula itoke maeneo mengine yaani ukubalike na sehem zingine.Ndio moderators huwa mwisho wa sku wanakaa na kangali wao nani anastahili,sasa ukikosa unaanza kulalamika unalalamika nin? Tuawaache wao wenyewe wanaoandaa wafanye kaz yao!
 
Inaelekea Diamond anamzidi vitu vingi sana Alikiba. Kama ni suala la figisu figisu ina maana Kiba na ukongwe wake wote anashindwa nae kufanya hizo figisu akashinda hizo tuzo kama anavyoshinda Mondi?
Kama ishu ni Salam inamaana Tanzania hatuna mtu kama Salam nae akamsapoti Kiba? Kulalamika lalamika kila siku hakutamsaidia Kiba anachopaswa ajue udhaifu wake upo wapi ili ajiongeze.
Yoooooooooo[emoji3]
 
Niaje wadau.

Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu Alikiba kupokonywa ushindi huko MTV EMA.Naomba hapa nitumie nafasi hii kufafanua kilichotokea ili kuweza kuondoa huu utata.

Kwa mujibu wa Mtv Ema Alikiba ameshinda kwa kura nyingi sana alizopigiwa na mashabiki na wamemtangaza kuwa katika kipengele cha kura nyingi Ali ndio mshindi.

Naomba tufahamu kwamba Tuzo kubwa kama MTV EMA na BET kuna vipengele ambavyo maamuzi yake hayategemei kura za mashabiki bali huamuliwa na wadhamini, majaji pamoja na waandaaji wa Tuzo. Kipengele hiki huangaliwa ni kiasi gani msanii anafanya vizuri katika category aliyowekwa cz inawezekana msanii akakosa kura nyingi lakini anastaili kupata tuzo kutokana na mchango wake katika mziki.

Kipengele hicho ndicho kilichomfanya Wizzy ashinde Tuzo hiyo ya MTV EMA.
Kiukweli MTV EMA hawajakosea katika hilo cz watanzania wengi walimpigia kura Kiba bila kujali team zao lakini kwa viwango vya kimataifa kiba hawezi kumfikia hata Robo Wizkid.

Alikiba alitakiwa kuwaambia ukweli mashabiki zake na sio kulalamika kwenye media kuwa haelewi kilichotokea wakati anafahamu ukweli wote. Kulalamika kwa Ali kutamsababishia picha mbaya na sidhani kama MTV EMA watakuja tena kumchagua kuwania Tuzo hizo katika Category yoyote ile.

Natumaini nimeeleweka japo kwa uchache.
Kiba kazoea Kili,MTU ananunua magazeti ya Siku nzima anaajiri vibarua kutia tiki
 
Kuna haja gani ya kupiga kura sasa kama hawazifuati?
Sometimes natamani nijue nyie timu kiba mko darasa la ngapi? Mbona uwezo wenu wakureason ni mdogo hivyo jamani, SMH. Unataka kura zifutwe kivipi wakati ni kigezo lakini si kigezo pekee chakutoa ushindi. Bwana hebu jifunzeni vitu mpate na exposure. Mnachosha.
 
Hivi sasa viroja! Hadi jana Kiba alikuwa anaonekana ndo mshindi wakati Mshindi alishatangazwa tangia juzi??!
View attachment 430878

Halafu ngoja tuwasemee hawa Sauti Sol kwa King... yaani pamoja na kufanya nae collabo lakini bado anatambua ushindi wa WizKid??!! Ina maana haoni wenzie tunavyoendelea kulia lia??
View attachment 430880

Jecha Salim Jecha anawahusu... kumbe mlitaka kujitangazia ushindi wenyewe wakati wenye wajibu huo ni MTV!!!! Hakina Mshindi vipi wakati Mshindi alishatangazwa tangia juzi?? Angalia hapo juu... hata colleagues wa Kiba, yaani Sauti Sol, walishatoa pongezi za mshindi wa hiyo category tangia juzi!!!! Assumptions with no evidence!! Hebu tuone website ya MTV ilikuwa inasema nini for Korea:
View attachment 430892

Nani alitangazwa Best Worldwide Act?


View attachment 430893

Kwahiyo madai yako kwamba kwavile WizKid asingeweza kuwa Best Worldwide Act bila kuwa Best African Act ni madai yasiyo na msingi manake hao jamaa wamechukua hiyo tuzo bila kuwa Best Korean Act!
Team Kiba mnatia aibu... mnadiriki kujihalalishia kuwa manyani wakati issue ni nyinyi wenyewe kushindwa kufahamu hata mambo madogo!!! Majority mnadhani MTV Base Africa hawakuwa na wajibu wa kumtangaza winner huku mkidhani mwenye wajibu huo ni MTV EMA!!!

Angalia hapo juu... Winners kutoka nchi na regionals mbalimbali wametangazwa na local MTV channels na sio MTV EMA! Local MTV Channel kwa Africa ni MTV Base Africa... wao wamefanya kilichofanywa na wengine wote! Pamoja na mifano ya hapo juu; wengine hawa hapa:
View attachment 430895

Mshindi wa Spain huyo, hakutangazwa na MTV EMA bali na MTV Espana
View attachment 430896
Mshindi wa Denmark huyo, hakutangazwa na MTV EMA bali na MTV Denmark!!

View attachment 430898
Mshindi wa Uholanzi huyo, hakutangazwa na MTV EMA bali na MTV Netherlands.

So, again, madai yenu kwamba MTV Base Africa wamefanya kazi isiyo ya kwao ni madai yasiyo na msingi wowote!!!!


Team Kiba ndo mnajifanya hamjaelewa...
Millard Ayo is smart guy... bado anayakumbuka ya Maalim Seif na Salum Jecha! Asingeweza ku-post kitu ambacho hakijatangazwa officially!!!

Let's take a break kisha tupitie MTV EMA Standard Voting Rules zinasemaje:

The Best Local Act category gives viewers and fans to vote for the Best Local Act in each of 32 separate countries/regions, as outlined on the Website/App, and such categories may be referred to locally by names such as "Best Dutch Act", "Best Belgian Act", etc. Voting for the Best Local Act category has two phases:

  • Phase 1: Pre-nomination.
  • Phase 2: Final Voting: In this phase you will be able to vote for the Best Local Act nominees in any participating country/local region. Local winners from each country/local region will be announced online on 6 November 2016...
Kumbe washayasema hayo kabla... kura zinapigwa, MTV EMA wanafaya tabulation na hatimae MSHINDI ANATANGAZWA!!!! Nisaidie wewe sasa... ni wapi Kiba alitangazwa kwamba mshindi?!

Tuendelee!!


Uamuzi wa kumtangaza Mshindi upo vipi? MTV EMA hawa hapa tena:

The total number of votes submitted during the Voting Period for the "Nominees" in each of the eligible categories will be tabulated by MTV EMA and the "Nominee" with the most votes in its applicable category, as determined by MTV EMA, will be declared the winner of such category. If, for any reason, this voting process is interrupted for any reason, is found to have been tampered with in any way, or for any other reason that MTV EMA believes in its sole discretion to be reasonably necessary, MTV EMA reserves the right to select the winners at its discretion and may take into consideration the number of votes received by a Nominee up until the time of the interruption or cancelation of the voting process.

Lini na kupitia wapi Kiba alikuwa declared kwamba ni winner kama si kwamba mlitaka kujitangazia ushindi wenyewe?


Tuendelee!!

Wala hakuna cha scandal wala nini na ndio maana ingawaje winners wametangazwa tangia juzi usiku, ni Team Kiba peke yake ndo wanalalamika... Team wale wale ambao walilia lia kwenye karibu kila tuzo including show ya Mombasa kwamba wamezimiwa mic...!

MSHAZOELEKA!!!

Waliopata kuonesha dharau za wazi kwa King ni wale ambao walipata kusema: "Go tell that man to leave the stage in less than two minutes or else we will physically get him out of the podium...."
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] pamoja na gazeti lako nimekuqoute hivyo hivyo. Wasipoelewa achana nao, Wataelewa wakikua.
 
Huwa kila cku kabla ya kulala naangalia video ya ally akiongea kizungu nabak nacheka sana
 
Duh Watanzania tuna kazi kubwa na huu uteam, kumbe povu lote hili unamtetea mnigeria kwa vile uteam kwako ni zaidi ya utaifa!!
Tuwe na Akiba ya Maneno Jamani. Sasa kikowapi? Mbona wamekubali makosa yao na Wizkid amefuta hiyo mijigambo yake yote.
 
Sio mkuu kura sio kila kitu kwenye hizi tuzo za kimataifa ngoja nikupe mfano hai
Tuzo za mwaka huu za BET kwenye kura diamond aliongoza akiwa na 53% akifuatiwa na yemi alade akiwa na 29% black coffie alikuwa wa mwisho akiwa na 5%
Lakini BET walimtanga black coffie kuwa mshindi.
Kipengele cha kupiga kura wameweka tu ili kuleta msisimko lakini hazina mchango kuamua mshindi.
Mtv ema ni ya europe sasa ukiangalia impact ya wizkid kwa ulaya inajieleza vizuri.
ndo hapo unakuta sometyme wapumbavu wanamfananisha wizzy au tekno na diamond,yes diamond ni mkali kiaina yake ,lakini kwa hizo no hagusi.
mbaya zaidi ni kwamba lyrics,tune,appearance zake kwenye video ni copy and paste toka kwa wapopo.

kuna diamond yuleeee wa
kizai zai
nataka kulewa, hatutamsahau
 
na hapo tayari ishajulikana tatizo liko wapi,kuna watu walikua wanapigiwa kura nyiiingi sana wanachukua tuzo.hii juzi imetokea pia diamond kala tuzo 3 za wanaijeria lakini zikatolewa USA,kisha akalambishwa nyingine 3 hapoo karibuni naigeria na wapopo hao hao.jumla 6 bwana matuzo kwa nyimbo gani.

Alikiba kalilia katuzo hako kmoja tu maskini kwani ameona ni haki yake kanyimwa na ukweli umejulikana,kiba hashindani na mtu,ye nyimbo zake ni hizo na sauti unique anayo
 
Sele acha kutuletea wenge bwana kama wewe unaona hivo ni wewe angekua hiyo unayemshabikia ungesema hivo kiba kama kapigiwa kura nyingi basi ndo anastahili hiyo unayosema wewe ni ya kwako
 
Katika ishu kama hii kuna kila umuhimu wa MTV kujifunza kwamba kura zinaweza zikapeleka ushindi kwa mtu asiyestahili. Ni ukweli uliowazi pamoja na kwamba ni mchungu kuumeza, Alikiba si bora kumzidi Wizkid. Labda kwa sababu tunataka sifa za kuonekana tumepata tuzo ila mhhh kama ni kufuata ubora na mafanikio basi Wizkid ndiye aliyestahili.
 
Katika ishu kama hii kuna kila umuhimu wa MTV kujifunza kwamba kura zinaweza zikapeleka ushindi kwa mtu asiyestahili. Ni ukweli uliowazi pamoja na kwamba ni mchungu kuumeza, Alikiba si bora kumzidi Wizkid. Labda kwa sababu tunataka sifa za kuonekana tumepata tuzo ila mhhh kama ni kufuata ubora na mafanikio basi Wizkid ndiye aliyestahili.
Kuwa muelewa tuzo hazikuwa za ubora wa muda wote au wa miaka yote ilikuwa kwa mwaka mmoja tu. Go go Kiba&Diamond
 
Mkuu hio sio account official ya MTVEMA,Ni fake account tu ambayo teamkiba wameanzisha,hakuna sehemu walipojibiwa na MTV niamini mimi.

Halafu hata hizo Link wanazosema waliweka sijui mstari baadae wakautoa pia ni fake...tembelea account yao MTVEMA huko instagrama ukaone kilichopo cha ukweli.

Allykiba anatafuta kiki tu ila ajulikane nje kwa njia za panya,
Anahisi labda atajibiwa kama alivyojibiwa EddyKenzo na MTVBASE.
Anasahau kama hakunaga shortcut kwenye mafanikio!
Yaani mtu hana collabo hata moja ya kimataifa wala award halafu leo anataka apewe BEST AFRICAN ACT NA BESTWORLDWIDE ACT kweli jamani?![emoji38][emoji38]

Hizo collabo na NuhMziwanda na Abbyskills ndio zimpe tuzo kubwa kama hizo?!anautani kweli
haya tuzo ni yake bila collabo wala nini, una lingine la kukashifu
 
Nongwa tu... Ndio maana watu wa nongwa hawaishi miaka mingi... Mnajipa maumivu mambo ambayo hata hamuwezi kuyazuia,.. Mnajitafutia ugonjwa wa moyo bureeee. Kwani akipata Kiba wewe anakupunguzia nn ndg yangu!? Au akipata Diamond au wizkid una share yoyote? Waliopiga kura ndio walioamua babuuu... Isiwe tabu.
 
Back
Top Bottom