Alikiba ameshinda Mtv Ema lakini hakustahili zaidi ya Wizkid!

Duh Watanzania tuna kazi kubwa na huu uteam, kumbe povu lote hili unamtetea mnigeria kwa vile uteam kwako ni zaidi ya utaifa!!
 
Chaaa, ww ndiye unapotosha,,kulikuwa na category nyingi ikiwemo 'winners category 'na siyo 'wenye Kura nyingi'kama unavyosema,, kuweni wakweli hata Mara moja tuu,, mnabadilisha story simply because mna chuki na ali
Hakuna alichopotosha alichosema ni kweli... kwenye website hawakutangaza washindi bali walionesha wenye kura nyingi... utaratibu wao ni kwamba, mshindi anatangazwa officially! Na utaratibu wa MTV upo wazi kwamba baada ya zoezi la upigaji kura; kura zitakuwa tabulated na MTV EMA na mshindi KUTANGAZWA! MTV Hawa hapa:

"In this phase you will be able to vote for the Best Local Act nominees in any participating country/local region. Local winners from each country/local region will be announced online on 6 November 2016...!" Na kweli, wao wakamtangaza mshindi tarehe 06 kama walivyosema wenyewe!


Tusaidie wewe sasa... ni wapi Kiba alitangazwa kwamba mshindi?!

Na siku hiyo hiyo wanaofahamu haya mashindano yanaendeshwaje, wakatoa pongezi kwa WizKid hata kama wana uhusiano wa karibu na Kiba compared to Wiz:


Kinyume chake, hayo ma-screenshot mnayoyasambaza ni ya tarehe 07 wakati winner ameshatangazwa tangu tarehe 06! But simple question... hivi kila siku awe anaonewa Kiba peke yake?! AFRIMMA anahujumiwa yeye! Kwenye show za Mombasa, anahujumiwa yeye! MTV nao wanamhujumu yeye! Ndo vile bado hajawahi kupata nomination BET... huko nako mtalia lia vile vile kama mlivyokuwa mnalia lia kwa kutopata nomination!!!
 
Hakuna jambo linalonikwaza Kama watu kusema Ali anapenda kulalamika,hana uwezo, ,, kwani hamuoni utata uliopo?? Kila aliyeshinda aliwekewa pink mark,,
Mshindi hawekewi pink bali ANATANGAZWA!!!! Ali Kiba hakutangazwa popote kwamba ni mshindi!
mtvbaseafrica (siyo mtvema)wakampost wizkid!
Hoja nyingine ya Team Kiba... mnadhani ni MTV EMA ndio walikuwa wanapaswa kutangaza mshindi wakati regional winners wanatangazwa na regional MTV Channels na sio MTV EMA kama mnavyodhani!
Mshindi waDenmark huyu hapa... hakutangazwa na MTV EMA bali na MTV Denmark na wao MTV EMA waka-RT announcment:


MTV ESpan hawa hapa na ndio alimtangaza mshindi wa Spain na wao MTV EMA wali-RT tu!



Ni MTV Netherlands ndio walimtangaza Mshindi wa Netherlands na MTV EMA wao wali-retweet tu matokeo yaliyotangazwa na MTV Netherlands!


Na washindi karibu wote, ndivyo ilivyokuwa! Kwahiyo hoja yenu kwamba MTV Base walim-post WizKid badala ya MTV EMA ni hoja isiyo na nguvu!
Yale yale... haioneshi mshindi ni nani wakati mshindi alishatangazwa! Na katika Stanadard Voting Rules za MTV EMA hakuna popote waliposema mshindi atawekewa alama kuonesha ushindi bali kura zitakuwa tabulated na mshindi KUTANGAZWA! Hakuna popote ambapo Kiba alitangazwa!
Hawakuweka popote kwamba mshindi bali walionesha wanaoongoza! Baada ya zoezi la upigaji kura kwisha, ndipo kura zinakuwa tabulated na wao MTV EMA wanatangaza mshindi!! Mshindi anatangazwa! Na endapo wanaona anything suspicious, wana mamlaka ya kupiga chini zoezi la kura na kutangaza mshindi kama wanavyoona wao!

If, for any reason, this voting process is interrupted for any reason, is found to have been tampered with in any way, or for any other reason that MTV EMA believes in its sole discretion to be reasonably necessary, MTV EMA reserves the right to select the winners at its discretion....!

Mssiwe mnakurupuka wakati hamjui taratibu! Hata Kiba alisema kwamba wanafuatilia kufahamu vigezo hii ni kituko kwavile kila kitu kilikuwa wazi from day one! Na MTV EMA waliweka wazi from Day One kwamba:

"By participating in this voting process, you agree to be bound by these How Voting Works For The 2016 MTV EMA rules. Failure to comply with these rules may result in a voter's disqualification solely at the discretion of Sponsor. Sponsor reserves the right to modify these How Voting Works For The 2016 MTV EMA rules at any time in its sole discretion."
 
Kwa mujibu wa iyo post kiba hakushindwa,kashinda ila tuzo kapewa mwingine kwa vigezo vilivyobuniwa siku iyo ya ugawaji tuzo
Ajifunze kukubaliana na matokeo,sio Tuzo zote kuamgalia idadi ya wapiga kula,lakin pia kwa mfano hio ya AFRIMA KAMA kula zako zote zinatoka kataifa kako tu hawakupi,inatakiwa kuwepo Msambazo wa kula kuwa karbu sehem ya kula itoke maeneo mengine yaani ukubalike na sehem zingine.Ndio moderators huwa mwisho wa sku wanakaa na kangali wao nani anastahili,sasa ukikosa unaanza kulalamika unalalamika nin? Tuawaache wao wenyewe wanaoandaa wafanye kaz yao!
 
Inaelekea Diamond anamzidi vitu vingi sana Alikiba. Kama ni suala la figisu figisu ina maana Kiba na ukongwe wake wote anashindwa nae kufanya hizo figisu akashinda hizo tuzo kama anavyoshinda Mondi?
Kama ishu ni Salam inamaana Tanzania hatuna mtu kama Salam nae akamsapoti Kiba? Kulalamika lalamika kila siku hakutamsaidia Kiba anachopaswa ajue udhaifu wake upo wapi ili ajiongeze.
Yoooooooooo[emoji3]
 
Kiba kazoea Kili,MTU ananunua magazeti ya Siku nzima anaajiri vibarua kutia tiki
 
Kuna haja gani ya kupiga kura sasa kama hawazifuati?
Sometimes natamani nijue nyie timu kiba mko darasa la ngapi? Mbona uwezo wenu wakureason ni mdogo hivyo jamani, SMH. Unataka kura zifutwe kivipi wakati ni kigezo lakini si kigezo pekee chakutoa ushindi. Bwana hebu jifunzeni vitu mpate na exposure. Mnachosha.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] pamoja na gazeti lako nimekuqoute hivyo hivyo. Wasipoelewa achana nao, Wataelewa wakikua.
 
Huwa kila cku kabla ya kulala naangalia video ya ally akiongea kizungu nabak nacheka sana
 
Duh Watanzania tuna kazi kubwa na huu uteam, kumbe povu lote hili unamtetea mnigeria kwa vile uteam kwako ni zaidi ya utaifa!!
Tuwe na Akiba ya Maneno Jamani. Sasa kikowapi? Mbona wamekubali makosa yao na Wizkid amefuta hiyo mijigambo yake yote.
 
ndo hapo unakuta sometyme wapumbavu wanamfananisha wizzy au tekno na diamond,yes diamond ni mkali kiaina yake ,lakini kwa hizo no hagusi.
mbaya zaidi ni kwamba lyrics,tune,appearance zake kwenye video ni copy and paste toka kwa wapopo.

kuna diamond yuleeee wa
kizai zai
nataka kulewa, hatutamsahau
 
na hapo tayari ishajulikana tatizo liko wapi,kuna watu walikua wanapigiwa kura nyiiingi sana wanachukua tuzo.hii juzi imetokea pia diamond kala tuzo 3 za wanaijeria lakini zikatolewa USA,kisha akalambishwa nyingine 3 hapoo karibuni naigeria na wapopo hao hao.jumla 6 bwana matuzo kwa nyimbo gani.

Alikiba kalilia katuzo hako kmoja tu maskini kwani ameona ni haki yake kanyimwa na ukweli umejulikana,kiba hashindani na mtu,ye nyimbo zake ni hizo na sauti unique anayo
 
Sele acha kutuletea wenge bwana kama wewe unaona hivo ni wewe angekua hiyo unayemshabikia ungesema hivo kiba kama kapigiwa kura nyingi basi ndo anastahili hiyo unayosema wewe ni ya kwako
 
Katika ishu kama hii kuna kila umuhimu wa MTV kujifunza kwamba kura zinaweza zikapeleka ushindi kwa mtu asiyestahili. Ni ukweli uliowazi pamoja na kwamba ni mchungu kuumeza, Alikiba si bora kumzidi Wizkid. Labda kwa sababu tunataka sifa za kuonekana tumepata tuzo ila mhhh kama ni kufuata ubora na mafanikio basi Wizkid ndiye aliyestahili.
 
Kuwa muelewa tuzo hazikuwa za ubora wa muda wote au wa miaka yote ilikuwa kwa mwaka mmoja tu. Go go Kiba&Diamond
 
haya tuzo ni yake bila collabo wala nini, una lingine la kukashifu
 
Nongwa tu... Ndio maana watu wa nongwa hawaishi miaka mingi... Mnajipa maumivu mambo ambayo hata hamuwezi kuyazuia,.. Mnajitafutia ugonjwa wa moyo bureeee. Kwani akipata Kiba wewe anakupunguzia nn ndg yangu!? Au akipata Diamond au wizkid una share yoyote? Waliopiga kura ndio walioamua babuuu... Isiwe tabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…