Alikiba atoa tamko , awataka mashabiki waache kumtukana Wizkid aseme yeye ni shabiki wa Wizkid


Kaka naomba uchukue ile Fanta mpya ya bariiiiid nakuja kulipa. Umesema kile nilichokua nakiwaza. Tuweke mambo ya uteam pembeni.. Halaf tuchukue mfano huu, Diamond kakosa tuzo mbili kwenye MTV mama awards na huyu kaka alifanya vizuri sana mwaka jana vizuri mnooo halipingiki na MTV wanajua maana walikua bingwa wa kusapoti kazi zake pia. Mchuano wake na wizkid ulikua mkali sana, I'm sure mpaka tuzo kwenda kwa wizkid MTVwenyewe walifanya maamuzi ya kishujaa sana(lol). Now how did Diamond react immediately baada ya kukosa tuzo zote? 1. Alifanya bonge moja la Perfomance mpaka BET na MTV Africa walionyesha hisia zao kwenye page zao kufurahia perfomance ile. 2. Kesho yake mapema sana alituma ujumbe wa shukurani kwa MTV, alitoa pongezi kwa washindi wote 3. Aliwashukuru voters wote na kuonyesha kiasi gani anathamini michango yao. 4. Kubwa kabisa alianza kupost kazi zake, matukio yake, kazi mpya ya stylist wake qboy msafi na kukimbiza gurudumu lake kama kawaida.
Mashabiki wa Diamond walijaribu kuonyesha kukasirika na matokeo lakini kwa kawaida sana, walirusha matusi ya hapa na pale kwa MTV lakini ni jambo ambalo hata MTV wenyewe waliona linakuja na litapita. Na kweli lilipita within 24hrs na maisha yakaendelea
Sasa kaka yetu wa Sony (Ali kiba) baada ya kukosa tuzo alikaa kimya, hakupost hata tangazo kwa takriban siku tatu, kisha wakati team yake inaendelea na mashambulizi ya mvua ya matusi yeye akaanza kupost picha tu kama kawaida bila kuongelea lolote kuhusu tuzo wala kuwaasa waache kutukana, hali iliendelea hivi mpaka ikawa out of control na MTV EMA kuanza kuwapa mashabiki majibu(ina maana waliona situation is getting out of control) mind you wizkid alikua akiona yanayoendelea na alikua kimya. Mwisho wa siku Tuzo ilirudi kwa Kiba (honestly MTV EMA hawakutoa sababu zozote za kueleweka za kuirudisha wamejibaraguza tu) Kiba hakusema kitu na wala hakupata promo kubwa from the MTV team maana hawakupost chochote kwenye page zao zenye influence za insta(mpaka leo hii). Kaka akakaa kimya mpaka juzi cjuy jana ndo kapost. Halaf kikafata na kipost cha msamaha kwa Wizkid (mhh ama kweli). Point yangu ni kuonyesha how two people handle their issues. Ndo maana wahenga walisema how you handle the problem is what defines you. Ndo maana mwisho wa siku Kiba kashindwa kupata shangwe na heshima kutoka kwa taifa maana hiyo tuzo yenyewe imekuja bila heshima. Plus asahau tena nominations huko kwa wenzetu maana sidhani kama watarudia makosa. Yale yaleee ya KTMA mpaka tuzo hadi leo zimekufa.
 
Yani ndio mana Wizkid aka tweet kuwa "there are so many dumb people in this world"...yani watu hawajui kabisa ku read between the lines...Kosa lime fanywa na MTV victims ni Wizkid na Alikiba...wote wawili ni wahanga wa yaliyo tokea,wanatokea watu wanao mlaumu/mtukana Wizkid kwa kosa lililo fanywa na MTV EMA, ambao ukiangalia kwa picha kubwa atakae onekana mbaya ni Alikiba, wengine wanatumia kivuli cha Alikiba kuonekana ni Alikiba ndio mwenye hayo maamuzi, kuna wangapi wenye nia mbaya na Ali wanao weza kuchukua hii nafasi kumchafua, okay tuyaache hayo, anakuja Alikiba kama mhanga mkuu wa tukio anapo jaribu ku neutralize situation na kutoonyesha uhasama baina yake na Wizkid, wanatokea watu na kusema asinge fanya hivo/ sasa mlitaka afanyaje ? He is simply showing a good gesture never the less a positive one but watu wanakua driven by emotions na utimu usio na msingi, according to his words ame claim kua ni it's in his belief that none of his true fans could be a part of that and he is actually condemning the whole situation but sjui tatizo ni kiingereza ??you guys are better than that, ndio mana wa Kenya wana tucheka kila siku ikija kwenye swala la kuelewa na kudadavua mambo
 
Source ya Matusi ni nini? Ilianza lini? Usimtetee....HUKUSIKIA KWENYE JAHAZI ALISEMA NINI?
 
Source ya Matusi ni nini? Ilianza lini? Usimtetee....HUKUSIKIA KWENYE JAHAZI ALISEMA NINI?

Kwenye Jahazi Gadna ndio alimuuliza imekuaje kwenye website ya MTV inaonyesha kua alikiba ndio mshindi (ameongoza kwa kura) lakini tuzo imeenda kwa Wizzy, yeye akamjibu kua management yake inafuatilia hilo suala, sasa sijui ni kipi kingine walichoongea ambacho wewe ulikisikia na mimi siku kisikia mkuu nifahamishe na mimi nijue....na simtetei najaribu tu kuiangalia situation nzima kwa pande zite tatu
 
Bulaza hongera sana tena sana,maana hiki kiingilishi chako kama sio Exford basi ni UDSM. Lakini kaka msomi mi nakuuliza kitu kimoja,hivi tatizo linatatuliwa kwa kuanzia juu au chini ................. Maana mwanzo wa YOOOOOOOOOTE NI YEYE,KWAHIYO ALILOLITENGENEZA LINAMRUDIA KUMWADHIBU MWENYEWE. NA ATAENDELEA KUOMBA POO SANA KAMA HAJAJICHUNGUZA VIZURI.
 

Labda nikuulize, Ali amekosea wapi ? Kabla sijajibu swali lako ningependa kujua unavyo ongelea kutatua tatizo, je ni tatizo gani haswa unalo liongelea na ni nani alie tatua hilo tatizo kuanzia wapi kuelekea wapi ? Maana nahisi tunaongea vitu visivyo shabihiana
 
Angewakataza mashabiki wake from the beginning na kwa nn kafanya baada ya tuzo kurudishwa inamaana isingerudishwa hadi leo wangekuwa wanatukana....
 

What's your take?

Wewe msanii wako nani?
 
Angewakataza mashabiki wake from the beginning na kwa nn kafanya baada ya tuzo kurudishwa inamaana isingerudishwa hadi leo wangekuwa wanatukana....

Unajua kosa la Alikiba ni nini ? Mimi ntakwambia, kosa la Alikiba ni kuwa Alikiba, nna maana gani, angeongea kitu mngesema anajipendekeza/mngesema ana jikweza/mngesema anatafta kiki...hatukosagi la kusema hata asipo sema kitu...ifikie wakati tujitahidi ku support mziki wa kila mwanamziki Kutoka Tanzania anae onyesha juhudi kwa maana heshima inarudi kwetu wenyewe, ukiangalia kwa mtazamo mdogo utaona anaye komolewa ni Ali lakini kwenye picha kubwa tunaonekana ni vituko katika nchi za wenzetu nje ya Tanzania, nahisi tunahitaji zaidi kuji tafakari kwa mapana zaidi
 
Yeye aendelee kujitekenya tu na kucheka mwenyewe,sisi tushapita level hizo,sijui kulilia tuzo,sijui kuomba msamaha,sijui nini ona level hizi.
Tuzo za ujanja ujanja tumeshazistukia nyie wazee wa fitina na figisu figisu Kama CCM hizo tuzo hazina maana tena Wenda kuna watu walizurumiwa
 
Yes kaka msomi, ni kweli unaongea kitu husichokijua, maana ungekuwa unajua mambo ya huyu "king wetu" husingemtetea labda uwe ni kati ya wale mashabiki wasio mnufaisha kwa lolote zaidi ya uwezo wao wa matusi. Picha linaanza wakati huo anatoa wimbo wake na kujitapa redioni "nimekuja kufuta vumbi kiti changu" "mimi ndio king huyo mwingine wanamsikiliza kwa vile kilicho bora hakipo" "mimi siwezi kutoa wimbo chini ya miezi 6" "mimi siwezi kuweka dancers kwa vile mimi mwenyewe ni zaidi ya dancer" "kwangu tuzo si kitu" "nimeshafanya kazi na R. kelly wanigeria kitu gani" Sasa angalia hizo kauli kwa undani anamlenga nani ............. Sasa juzi kati kasema "hata mashabiki wangu wanashangaa hizi tuzo zina zigezo gani kama sio kupiga kura" kwahiyo taarifa ya mashabiki wake wanafanya nini kwenye page ya Wizkid na MTV EMA ALIKUWA NAYO ILA ALIKUWA ANASUBIRI APEWE NDIO AONGEE SASA WALE MASHABIKI WAKAENDELEZA NA MATUSI YAO,LEO MUKISEMA ETI YUKO SAHIHI MNAKOSEA KWASABABU MATUSI WAMEANZA KABLA HAJAPATA HURUMA YA KUPEWA.
 
Tuzo za ujanja ujanja tumeshazistukia nyie wazee wa fitina na figisu figisu Kama CCM hizo tuzo hazina maana tena Wenda kuna watu walizurumiwa
Chukua na hii,Zenji hiyo.
 

Maneno yako yame jaa chuki kidogo lakini tuyaache hayo maana mada hapa ni kuhusiana na kinacho endelea na si kilicho wahi kutokea...kwa uelewa wangu kutokana na maandishi yako inaonekana kilicho kuumiza wewe ni muda wa Alikiba kutoa tamko, kwamba "ULIVYO KUA UNATAKA WEWE" ni atoe tamko kipindi mashabiki ambao kulingana na pande zote mbili (ambao hawaja julikana ni wa nani) walivo anza ku comment kwenye page ya Wizkid na Mtv na si alivyo AMUA YEYE kutoa tamko baada ya kupewa what was rightfully his kulingana na kura zilizo pigwa ? Maana ndicho cha msingi ulicho kiongea kwenye maandishi yako hapo juu ???
 

Na huja nijibu maswali yangu hapo juu kulingana na ulicho kua una zungumzia
 
Diamond na tim yake watu wa fitina Sana wakalimpa tecno PESA ili ataje Simba ili kumdhoofisha king.
Na atazidi kumuacha mbali sana kama kila linalomtokea anamuona DIAMOND tu,soma caption hiyo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…