mtwamvina
Senior Member
- Jun 29, 2016
- 178
- 207
Muziki sio mashindani, na humpangii shibiki wa muziki ampende msanii huyo na amchukie huyu. Katika muziki tunaupenda kutokana na burudani na ujumbe tunaoupata katika muziki wenyewe. Sasa ushabiki wa wasanii ni namna fulani ya kutojielewa. Ushabiki kama huu upelekwe kwenye masumbwi tu.kama unamchukia msanii hautaona uzuri wake maana utausikiliza ukiwa tayari una majibu yako kichwani. Tupendeni mziki mzuri na sio kua na ushabiki kwa wasanii tena kwa kuwajengea chuki wengine.