Ngurubhe
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 1,840
- 1,049
Ndugu zangu,kumradhi Kama kuna watu watanielewa vibaya,lakini tufike hatua tujue kuwa nyeupe itabaki kuwa nyeupe,na nyeusi itabaki kuwa nyeusi.
Nimekuwa nikiwaskia Alikiba na Diamond wakihojiwa hasa na Sporah kila mmoja hunipa picha fulan hivi,lakini Huwa nuona Diamond hana tatizo na kiba,lakini kiba huwa anahisi kuna mtu anamuonea na kuwa yeye ndio mwimbaji bora lakini anaonewa na hata asionekane bora.Sjui mentality hii anaitoa wapi.
Inawezekana tunaowashabikia ndio tunawafanya wafike hatua hii,kwani hata nikirejea kilichotokea huko kenya juzi unaona kabisa ALIKIBA HATA AKISHINDWA AU KUKOSEA KWA KITU AMBACHO NI MAZINGIRA TU ATATAFUTA NAMNA YA kumsa vibaya Diamond.
Mim namshauri ALIKIBA AJUE KUWA kila mmoja anafaa,na kila mmoja kati yao ni mzuri lakini kila mmoja ana radha yake.
Ni ujinga chenza kujisfia ni tamu kuliko chungwa.
Au ndimu kujisifia ni bora kuliko limao.
Kila mtu atafaa na kukubalika katika mazingira fulani na kwa radha yake,namuona Alikiba akifaa na hata Diamond pia lakin kila mmoja na radha yake.
Diamond hadi sasa anazidi kupenya katika mziki wa kimataifa,Alikiba badala ya kutaka kujishusha ili ajue mwenzie anafanyaje yeye anatumia mda mwingi kuwaskliza mashabiki wa kibongo ambao aslimia kubw a huwa ni mara chache husema ukweli.
Mim nakushauri Alikiba ni kweli ulianza msiki mapema kuliko Diamond,yaani you are a senior lakini hii tu haitoshi kukufanya ushindwe kushirikiana na mwenzio baada ya kuwa amepanda chati kiliko wewe.Najua mashabiki wako huwa wanakupotosha hata hapa wataishia kuanglia na kuongea ujinga ujinga tu badala ya mambo ya msingi...
Usilewe sifa za kibongobongo ambazo zina radha ya hira,wivu,unafiki na majungu na u-dogmtism hii haitakusaidia chochote...hata Harmonize atakupita mim nakuambia....just hold on will soon see and understand my language.
Utabaki hata ukilala usingizi kwenye gari unahisi manager wa diamond kapita karbu na wewe..
Na nyie wabongo msemo wa nabii hakubaliki kwao ni msemo tu...Diamond is now an international muscian....najua ati akifa ndio huwa mnaanza oooo he used to be a good man acheni unafiki.....
Staki kusema juu ya TUZO walizopta huko Marekani nikiamin wote mnajua