Alikiba: Tunafuatilia kujua vigezo gani vilitumika kupata mshindi wa Mtv EMA

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Mkali wa bongo fleva Alikiba au King Kiba akiongea kwenye kipindi cha Jahazi clouds fm amesema management yake inafuatilia kujua vigezo gani vilitumika kupata mshindi wa mtv ema iliyotelewa jana huku Wizkid akitangazwa mshindi wa Best african act.

Alikiba anasema alipata kura za kutosha kumuwezesha kushinda lakini imekuwa tofauti, huku mashabiki wake pia wakilalamika kupokwa ushindi



Alikiba pia amesema atafanya show ya kufungia mwaka kama kawaida huku akianzia mikoani.

 
Kiba nae aache unafiki, si alisema hana mpango na awards, alafu wanafuatilia category ipi maana maana kama wiz kid alikuwapo ktk hiyo category wala hamna mchawi hapo. Zile alizoshindanishwa na Mond, Mond kamzidi kiba kwa mashabiki, kama ni suala la popular votes Mond fanbase yake ni kubwa!
 
Nina idea kidogo jinsi MTV (various awards) wanavyopata washindi wao! Ninaposema "various awards" kwa sababu MTV wana awards mbalimbali kama vile MTV MAMA, MTV Korea, MTV EMA, MTV Video Awards n.k!

Miongoni mwa wote hao, ni MTV EMA ndio wana utaratibu mzuri kupita wote! Majority ya awards zinazotolewa na MTV, Sponsor ndie ana Final Say. Hata kama umeona kura na unaongoza kwa 99%, hutakiwi kufurahi hadi siku mshindi anapatikana manake Sponsor manake mwisho wa siku Sponsor anaweza kusema "NO!"

Kinyume chake, kwa MTV EMA, ni MTV EMA wenyewe ndio wana final say... hapa hakuna commercial interests zinazoweza kutokea kwenye MTV Awards zingine!
 
Nimetoka kapa ebu rudia tena maelezo yako
 

Kaka naomba maelezo ya hiyo

 
Napenda mziki wa kiba ananiboa sana anavyopenda kulalamika vitu vingine unapiga kimya tu
Kiba sema nyota yake mbaya basi kila baya ni lake.....mi nimesikiliza mwanzo aliyeanza kumhoji kamwambia mashabiki wanashangaa kwann hakushinda wakati alikua na kura nyingi...ndio akajibu kuwa menejiment yake inafatilia....aliyeonyesha kulalamika ni mtangazi mwenyewe
 
Team mondi mnapenda kupindisha maneno, yeye kaulizwa washabiki wasemavyo. Kiba yupo sahihi lazima afuatilie kwa nini alishindwa ili kama kuna mapungufu ayafanyie kazi. Bila kumnanga kiba humu siku yenu inakuwa haijakaa vyema.
 
Kiukweli jamaa wamechemka sema wabongo wengi wanaroho mbaya yan mtu anaina bora mbongo mwenzake akose eti sababu ya miteam, Kama uliingia asubuhi mpaka mida ya saa saba mchana kwenye web ya mtvema yenye washindi kulikuwa kuna alama ya mstari mwisho kwa huo mstari kuna nembo ya mtv kwenye category zote. So kwa best african act hiyo alama ilikuwa ipo kwa kiba sasa walipo chemka baada ya watu kuandika sana wakahamisha kale kamstari wakakipeleka kwa wizzy kile kimstari kilivyotolewa kikaondoka na kura za kiba baadae wakakirudisha kwa kiba mwisho wakatoa kabisa!! Tatizo nini??


 
Sema tuzo zenyewe zengwe jingi ndomana zinachanganya watu Jana kuna icon iliwekwa kwa kila mshindi kwenye kila categorie na kiba ilionyesha ameshinda picha hizi
 
Nimetoka kapa ebu rudia tena maelezo yako
Wapi hapajaeleweka ndugu?

In short, MTV Awards wana kitu wanaita Officia Voting Rule. Moja ya hiyo Official Voting Rule, wana kipengele kinasema "The total number of votes submitted during the Voting Period for the "Nominees" in each of the eligible categories will be tabulated by Sponsor and the "Nominee" with the most votes in its applicable category, as determined by Sponsor, will be declared the winner of such category."

Nadhani unaona nguvu za sponsor hapo katika kufanya maamuzi ya nani awe mshindi! Na kipengele kingine kinasema wazi kwamba, endapo Sponsor kwa namna yoyote atajiridhisha kwamba kumetokea mapungufu kwenye upigaji wa kura; basi ni yeye ndie (sponsor) anaweza kuchagua ni nani mshindi kwenye category husika!!

Awards nyingi za MTV zina hiyo voting rule! Kinyume chake, kwa MTV EMA, hiyo sehemu ilipoandikwa Sponsor anasimama MTV EMA... ina maana, hicho kipengele cha juu kwa upande wa MTV EMA kinasema: "The total number of votes submitted during the Voting Period for the "Nominees" in each of the eligible categories will be tabulated by MTV EMA and the "Nominee" with the most votes in its applicable category, as determined by MTV EMA, will be declared the winner of such category.

Vipi umeona tofauti?! Hapo juu kuna hatari kukaingia commercial interests... ndicho kile ambacho alilalamikia Eddy Kenzo lakini suala kama hilo haliwezi kutokea kwa MTV EMA kwa sababu hamna commercial interests from sponsors.
 
Kaka naomba maelezo ya hiyo
Hiyo screenshot ni ya Instagram, Facebook; au?! But all in all, narudia... utaratibu wa MTV EMA upo wazi sana! Kwenye Standard Voting Rules za MTV EMA, wamesema wazi kwa zile categories ambazo winner anakuwa declared kwa kura; ni wao MTV EMA ndio wata-tabulated kura na kutangaza mshindi! Aidha, wamesema wazi kwamba endapo ANYTIME wakiona palikuwa na udanganyifu katika zoezi la upigaji kura (wametoa aina ya udanganyifu), basi MTV EMA wana haki ya kufuta kura hizo na kutangaza mshindi wanaeona wao kwamba alistahili!

Hizo hapo juu ni Standard Voting Rules ambazo zitakuwa practiced at MTV EMA's sole discretion...!! Lakini mwisho wa yote, wamesema wazi kwamba Sponsor wanaweza kubadilisha hizo standard voting rules anytime.
 
Muacheni alalamike tuu...wenzake wanaendelea kufanya Kazi.Yeye alfikiri kupiga KURA za "KIMARUHANI" ndio suluhisho la UKAME wa TUNZO....Ajiulize kati yake na DAVIDO ni nani wa kulalamika...!? Hamuoni/ajiulizi kwa nini mwenzie kapotezea....!! KING KIBA...It's time to GROW...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…