Alikiba: Tunafuatilia kujua vigezo gani vilitumika kupata mshindi wa Mtv EMA

Alikiba: Tunafuatilia kujua vigezo gani vilitumika kupata mshindi wa Mtv EMA

Kwenye ukweli bora tuseme tu, kila mtu ana mapungufu yake, kiba ana mapungufu kama binadamu ila anapostahili support wacha apewe tu, hawa mtvema wameonesha udhaifu sana kwenye kumtangaza mshindi kwenye kipengele cha Alikiba, vipengele vingine wote waliokuwa wanaongoza kura ndio walioshinda tuzo na muda wa kupiga kura ulipoisha kila mshindi kuna alama ya tuzo aliwekewa kwa mbele ya picha yake, imefanyika hivo kwa washindi wote na ile alama ilikuwepo kwa Alikiba pia

ila akaja kutangazwa wizkid tena yeye akatangazwa na mtvmama badala ya ema na pia akawa na cover tofauti na zile za washindi wenzie kama kina justin, drake na kama hiyo haitoshi baada ya team kiba kualalamika sana kwenye page ya mtvema ikabidi ile alama ya ushindi waitoe kwa Alikiba na kuiweka kwa wizkid ili kuweka mambo sawa ila baada ya muda wa kama nusu saa wakairudisha tena kwa Alikiba hadi hapo mtu ukitoa chuki za kike na zakitoto lazima utaona hawa jamaa wameboronga

Nakumbuka mwaka jana wakati tunabeba hizi tuzo kupitia kwa Diamond, tulipotoka kushinda best African act ndo akachaguliwa kwenda kwenye best worldwide act na tulipiga kura kwa siku kadhaa hadi pale Diamond alipoibuka mshindi tena kwenye best worldwide act, ila cha ajabu kwa wizkid tuzo zote best African act na best worldwide act ameshinda ndani ya siku moja kweli jamani????

Ata kama humpendi kiba ila weka chuki pembeni basi ata kwa muda tu na tuongelee utata wa hizi tuzo kwa mwaka huu
 
Kiba aache kulalama halafu hawa mtv kidogo wanachanganya sana
 
Ni kweli,ila ajabu kuu ni pale watu wanapo -overlook utata uliopo Kwenye hizi tuzo na kumkandia alikiba
 
Kiukweli jamaa wamechemka sema wabongo wengi wanaroho mbaya yan mtu anaina bora mbongo mwenzake akose eti sababu ya miteam, Kama uliingia asubuhi mpaka mida ya saa saba mchana kwenye web ya mtvema yenye washindi kulikuwa kuna alama ya mstari mwisho kwa huo mstari kuna nembo ya mtv kwenye category zote. So kwa best african act hiyo alama ilikuwa ipo kwa kiba sasa walipo chemka baada ya watu kuandika sana wakahamisha kale kamstari wakakipeleka kwa wizzy kile kimstari kilivyotolewa kikaondoka na kura za kiba baadae wakakirudisha kwa kiba mwisho wakatoa kabisa!! Tatizo nini??
tatizoooo nyotaaaa mbona mond alishawaambia kitambo au mnaboa bana
 
Kama vigezo ni kura tu diamond platnumz angekuwa tayari kashachukuliwa BET na tuzo MTV mama mwaka huu, wenzetu Kuna kitu extra wanakitazama, mtv mama wana panel (mmoja ya watu wanaounda panel bdozen, na ndio maana kila award zikifanyika lazima asafiri), Ukija MTV EMA mtu kama wizkid mwaka huu wake, one dance imefanya vizuri kuanzia marekani mpaka ulaya, mama cita tinnie tempah ft wizkid unakimbiza inchi za ulaya, shabba imeingia A list radio one extra ya uingereza, alikuwa na tour ya ulaya aliyofanya na cris brown (MTV EMA ni kwa ajili ya nchi za ulaya) sasa mnashangaa nn wizkid kushinda, kama kigezo kura nina uhakika black coffee asingechukua BET mwaka huu na tuzo ingekuwa ya platnumz, mimi kama ningekuwa kiba Namshauri aipotezee hii ishu inaweza ikamwaribia upande wa promotion wa nyimbo zake ktk kituo cha mtv, aachane nayo, kama mwenzake platnumz .
 
Asubiri akina tim wema au joket na wa kariakoo waje wapige kura za kilimanjaro wampe za kimagumash
 
Sema tuzo zenyewe zengwe jingi ndomana zinachanganya watu Jana kuna icon iliwekwa kwa kila mshindi kwenye kila categorie na kiba ilionyesha ameshinda picha hizi
d54d51d928b35604a6ed25d342781efa.jpg
28d7a5fb48796b48ef6af98bd7e5fa19.jpg
5cf274e5970617b2647410c991fcb3de.jpg

hiyo yenye African acts

naomba link nijionee mwenyewe, rusha tu hata kama wamebadili mshindi kama wanavyodai watu.
 
Aisee umenifurahisha sana mwenzie hata akikosaga humsikii ng'o akilalamika

alijua "aje" itampa tuzo ndio maana anaweweseka kwani anajua kujikinya na kudondosha "aje" nyingine lazima ajikunje sana manake ubunifu hana yeye anajazwa bichwa na kipaji cha sauti tu,wakati hata lunyamila alikuwa na kipaji cha soka,yupo wapi sasa hivi
 
MTV wanaelewa kwamba watz ni Machizi mtandao, linapokuja suala La kuvote tupo vizuri, lakini kweli kiba na starboy wampe kiba kweli? Hata kwa Sir God ni dhambi jamani tuacheni unafiki kiba hana hadhi ya kuchukua hiyo tunzo hata MTV mama hajawahi kuwa nominated Leo akachukue tunzo kubwa hivyo no way.
 
Kiukweli huwa siwapendi kabisa wasanii wengi wa Bongo hususani Ali Kiba, lakini katika hili nitamtetea kabisa, Kiukweli Ali Kiba ameonewa. Sioni mantiki kwanini ashindane vizuri na watu wampigie kura kwa wingi kuliko wengine wote halafu mwisho wa siku mshindi awe mwingine.

Sijaona tofauti kati ya MTV na Jecha wa Zanzibar.
[emoji23][emoji23][emoji23]mkuu achana na hizi siasa chafu za bongo[emoji38]utapata Ulcers bure kwa stress....unadhani sisi tunang'ang'ana na hili jukwaa la Celebrities tunapenda sasa?!heri huku kuna amani kuliko kule[emoji23][emoji23]...Jecha usimuwaze sana utakonda[emoji23][emoji23]
 
Hivi nyie munafikiri uwingi wa kura ndio kushinda?!ingekuwa hivyo Diamond angeshinda BET mwaka huu.

Sasa tuseme tu ukweli,hivi Alikiba unaweza ukamfananisha na hata Casspernyovest?!wachilia mbali Wizkid..

Wizkid anastahili kila aina ya tuzo mwaka huu,amejitahidi sanaa!!
 
Komando kipensi wapeleke ICC hao,MBNA kila tuzo wewe unakosa wakati domo anapewa kuna mkono wa MTU hapo mfalme tembo a.k.a bush man
 
Back
Top Bottom