Alikiba unakera sana wakati mwingine!

Alikiba unakera sana wakati mwingine!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Umetoa bonge la wimbo, 'Mahaba'. Ni booonge la wimbo, HAKUNA UBISHI. Views zinapanda tu bila kushuka mwezi wa tatu huu sasa. Ingawa shooting si bora (kwa mtazamo wangu lakini watu wameipenda hivyo hivyo).

Badala ya kutulia kidogo kwa muda ili utuletee kitu zaidi ya kile au ikishindikana basi kifanane nacho, unakurupuka na kuja kutuletea huu wimbo wa 'on fire' ambao hauna maajabu yoyote ukilinganisha na 'mahaba'. Ulichopatia ni shooting tu basi lkn ladha ya nyimbo si ipo chini sana. Una haraka ya nini?!!! Unakimbilia wapi?!!! Wewe asili yako ni utulivu, kuwa mtulivu. Tathmini tu nyimbo ambazo ulizitoa baada ya muda mrefu zilikuaje.

Usijiweke kundi la konde boy ambaye; anatoa nyimbo yenye jina linalotisha, 'ZANZIBAR', lkn ukiisikiliza nyimbo yenyewe unaweza kumfuata jukwaani mkapigane. Unapotumia jina kama hilo, alitakiwa ajipange nyimbo iendane na mvumo wa wa eneo lenyewe.....kama ya yule msouth afrika inayoishi mpaka leo.

Ali umetukera sana mashabiki.
 
Dah me nimeielewa mkuu naigonga sana tokea nimei dowload jana.
 
Sio umetukela sema amekukela

Tofautisha wingi na umoja hayo ni maoni yako au ujumbe wako sio wetu/ wangu


We kama unamuelewa huyo konde bac kuwa nae
 
Back
Top Bottom