Alikiba unapaswa kuomba RADHI Wakristo

Kutumia neno "Nyie ni wakristo", ni Disrespect na ni kitendo cha kumaanisha kuwa Dini ya wakristo ndio ya wafanya uovu, au ya watu wasiofaa, au ya watu wa ovyo. Kwamba Wakristo sio watu wa kuheshimu Mazishi.
Sijaelewa, kwani kuchukua video wakati wa mazishi ni uovu?
Mbona kuna baadhi ya waislam huonesha hayo matukio?
Huenda kiba aliuliza kutokana na taratibu zilizozoeleka za dini yake; yenye masharti mengi!
Nadhani Kauli yake haipaswi kuchukuliwa kwa ukubwa huo ulioeleza!
 
Mbona Ameuliza swali zuri? Ni sawa na uende umevaa sare kwenye mazishi ya kiislam au upange foleni ya kuaga maiti ni lazima wakushangae na wakuulize we ni mkristo?

Ukijibu ndiyo watakaa kimya watajua ni utamaduni wenu na ukijibu hapana bas utaambiwa taratibu za kiislam maiti haagwi wala katika mazishi haitakiwi kuvaa sare.

Hivyohivyo camera katika mazishi ya kiislam hairuhusiwi, ila kwa wakristo ni kawaida kuchukua video za kumbukumbu
 
Wakristo huwa hawana muda wa kuhangaika na "watu wasio haki"...

Kama wewe ni Mkristo elewa maneno "watu wasio haki"...
Wewe una haki gani? Na hao wasio haki hawana haki gani? Acha kuandika ujinga ujinga kama vile akili zako umeziweka kwenye friji kwa muda.
 
Fuatlia alikuwa ana maanisha nn kwanza ,tambua Ally kiba sio mtu dini kama unavyofikria.
Sikiliza hiyo Kauli vizuri alafu ulete hapa hoja kuwa hakulenga kuidharau Dini ya wakristo, labda kama kiswahili kinakusumbua... Dini ni nyingi sana kwa nini alenge Dini ya wakristo kwamba ndio wanatabia mbaya misibani... Mbona hakuuliza nyie ni kabila gani... Kwa maana hiyo ni kwamba yeye kwenye akili yake kaamini kuwa wakristo ndio wapiga picha misibani
 
😂😂Kwani taarifa hata wewe umejuaje kama Qur an imechomwa?

Tangu ni mdogo nasikiq hizo taarifa za Qur an kuchomwa yaana hata mtaani kwetu yupp kijana alichoma Qur an na tunaishi nae...Mungu atailindi dini yake milele .

Angalia tunavyopingwa vita na mataifa makubwa leo hii si pangekuwa hamna dini ila ukweli unabaki moyoni.
 
Sasa kama Dini yake ndio inakataza Kuchukua Video, kwa nini aulize kwamba ni wakristo kwani nani alisema Ukristo ndio unaruhusu kuchukua video msibani... Kwani angeuliza nyie ni wa Dini gani kosa lake lingekuwa wapi, kwa nini alenge wakristo hapo ndipo swali langu wakati dini Tanzania ni nyingi
 
HII AWAMU YA SITA WAKRISTO MNALALAMIKA SANA
Faiza akikomenti MNALALAMIKA
Mohamed said akileta Uzi MNALALAMIKA
Alikiba akisema tu MNALALAMIKA
Salim Kikeke kafuga ndevu MNALALAMIKA
Mama ameteua mawaziri juzi WAKRISTO wapo wengi MNALALAMIKA
Bandari apewe muwekezaji MNALALAMIKA..

Nyie hamna subira na uvumilivu ...
 
Mbona kama ni mpuuzi fulani hivi aliyelewa sifa? Ukiwa staa ondoa mipaka ya dini yako maana utakuwa na mashabiki wa dini mbalimbali acha kutoa maneno ya kuudhi dhidi ya dini nyingine kwa kuwa huko pia una mashabiki. Kwanza hata kuonesha kujinasibisha zaidi na dini yako wakati una mashabiki wengi na wasio na dini ni ujuha. Labda wale specific artist kama waiba qaswida na injili wale wana mashabiki wa huko kwenye uinjili na ukaswida, hata hao wanaweza kuwa na mashabiki wasio wa dini yao. Mastaa waheshimu dini zote za mashabiki wao
 
Huna akili wewe.
 
Wewe nae hua unakurupuka tu na chuki zako za udini,unadhani hujulikani humu? Umeielewa kauli ya Kiba? Au unafuata mkumbo tu kama kawaida yako?
 
Umesahau yule kijana alichana Quran, Magufuli akamfukuza kazi... Na baadhi ya waislamu mitandaoni wakawa wanataka kumuua... Wewe hujui Imani ni nini na ina nguvu gani... Al-shabab kila siku wanaua huko na kutaja Allah, wewe huna imani, wenzako wanaua huko kisa tu fulani sio muislam... Ndio maana Nchi za wakristo utakuta waislamu... Hila hapo Zanzibar tu kufungua kanisa ni ishu, Ukifungua kanisa Iran, Iraq, Afghanistan na nchi nyingine za kiislamu unaweza uliwa kabisa
 
Kama ambavyo qur-an haijasema waislam wanafuga majini lakin watu wamekua wakisema ni dini ya majini hivyo hivyo kauli ya alikiba kuwa wakristo wanarekodi watu wakiwa wanazika ni kutokana na tunayoyaona misibani kwenu
 
Aliuliza kwa sababi si desturi ya Waislamu Kurekodi wala kupiga picha katika msiba hasa Kwenye makabuli...

Heshima katima maziko ni kitu kinachohitajika sana katioa hadi ya hali ya juu sana katika uislamu ndo maana hata muislamu yoyote akipita barabarani na akaona kuna watu wanabeba Jeneza kuelekea kuzika hata kama hamjui mtu anayeenda kuzikwa lazma asimame ili abebe jeneza....
Kauliza kwa sbabu kilichofanyika si utaratibu wa dini ya kiislamu...
Na kingine Tanzania hakunaga Mpagani its Either Ni mkristo ama Muislamu asiyetaka kufata dini yake Period....
 
Acha kuongea vitu usivyovijua,hua mnaropoka hovyo tu,Iraq yapo makanisa,Iran wapo christians,Lebanon wapo wakristo,Syria,Misri kote huko wapo wakristo na Makanisa yapo.
 
Mleta mada unaonekana umepigika kimaisha kinoma,ndio maana unajiona ni victim na kutafuta visababu vya kulalamika ili japo ujifariji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…