Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Huwa ni kipaumbele cha watu wajinga na wajima
Tajiri namba moja barani Afrika,Aliko Dangote amesema kupata mtoto wa kiume sio kipaumbele chake.
Dangote alisema hayo wakati wa mahujiano na kituo cha televisheni cha Arise News cha nchini Nigeria.
Mtangazaji wa kipindi hicho alimuuliza Dangote kama ana mpango wowote kuhusu kupata mtoto wa kiume kwa sababu kwa utamaduni wa huko Kano anapotokea Dangote,mtoto wa kiume ndiye mrithi na muendelezaji wa jina la familia.
Dangote alijibu kuwa kupata mtoto wa kiume sio kipaumbele chake na pia Mungu ndiye anaeamua akupe mtoto wa jinsia ipi. Pia alisema wakati mwingine unaweza kuomba upate mtoto wa kiume lakini yeye ndio akawa chanzo cha kudondosha chini jina la familia.
Vilevile Dangote alimalizia kwa kusema,haamini kama watoto wa kiume wangeendesha kampuni zake kwa ufanisi zaidi kuliko mabinti zake wanavyofanya sasa.
Dangote amejaliwa kupata watoto watatu wakike ambao ni Halima,Fatima na Marya na wote tayari wanashikilia nafasi za juu za uongozi kwenye kampuni za baba yao.
Chanzo: Tuko NewsSahihi
Hakuna Hilo,inategemeaAache uongo, mtoto wa kiume ni ndoto ya kila mwanaume, Mungu hakupi vyote so asijikoshe.
Sio ndoto ya kila mwanaumeAache uongo, mtoto wa kiume ni ndoto ya kila mwanaume, Mungu hakupi vyote so asijikoshe.
Ndoto ya mwanaume mwenye akili ni kupata mtoto na sio mtoto wa jinsia fulani.Aache uongo, mtoto wa kiume ni ndoto ya kila mwanaume, Mungu hakupi vyote so asijikoshe.
Kwahiyo Mungu alimnyima mtoto wa kiume?Aache uongo, mtoto wa kiume ni ndoto ya kila mwanaume, Mungu hakupi vyote so asijikoshe.
"Ila kwa mwanaume ni ngumu maana hakuna wa kum manipulate"Kwa hiyo umeona utafute mechi na wanaume?
Mimi naona ni mtazamo wake tu. Kila mtu ana namna a nayaona mambo.
Wanawake msipo ongozwa vyema huwa mnaishia kuwa manipulated kirahisi. Ukute kawalea vizuri tu. Ila kwa mwanaume ni ngumu maana hakuna wa kum manipulate japokuwa akiendekeza sketi pia lazima kimlambe tu na yeye.
Kikubwa hapo sio jinsia bali ni namna alivyo wa shape watoto wake, waweze kuhandle kampuni zake
Kipaumbele cha kila mwanamme? Wewe ndio uache uongoAache uongo, mtoto wa kiume ni ndoto ya kila mwanaume, Mungu hakupi vyote so asijikoshe.
"Ila kwa mwanaume ni ngumu maana hakuna wa kum manipulate"
Mindset ya ajabu sana hii, mbona wanaume wengi tu wakiachiwa makampuni makubwa wanaishia showoff, pombe tu na kuhonga mali michepuko.
Tuache mfumo dume, ona kwa watoto wa kiume wa marehemu Hanspoppe, Msuya, Mengi, lwakatare n.k mbona wote wamevuruga mali hadi zingine kutapeliwa na wajanja?
japokuwa akiendekeza sketi pia lazima kimlambe tu na yeye.
Kikubwa hapo sio jinsia bali ni namna alivyo wa shape watoto wake, waweze kuhandle kampuni zake
Kwa dunia ya Sasa ni rahisi mwanamke kufanya biashara na ikaenda mbele kuliko wa kiume kiufupi mtoto ya kiume ya Sasa hivi ni ya hovyo."Ila kwa mwanaume ni ngumu maana hakuna wa kum manipulate"
Mindset ya ajabu sana hii, mbona wanaume wengi tu wakiachiwa makampuni makubwa wanaishia showoff, pombe tu na kuhonga mali michepuko.
Tuache mfumo dume, ona kwa watoto wa kiume wa marehemu Hanspoppe, Msuya, Mengi, lwakatare n.k mbona wote wamevuruga mali hadi zingine kutapeliwa na wajanja?
Kuna wanaume hawataki watoto kabisa, si wa kike wala kiume.Aache uongo, mtoto wa kiume ni ndoto ya kila mwanaume, Mungu hakupi vyote so asijikoshe.
Ndio Maana kupata katiba Mpya ni Kazi Kwa aina hiyo ya Watu.Sio ndoto ya kila mwanaume
Nchi hii inachangamoto moto nyingi, Moja wapo ni kuwa na Quality Human Capital, Imagine huyo Jamaa Leo 2026 anafikiria hivyo.Kuna wanaume hawataki watoto kabisa, si wa kike wala kiume.
Kuna janii zimeshajiondoa kwenye ubaguzi wa jinsia na unyanyapaa wa kuona mtoto wa kike ni kama nusu mtoto. Kitu ambacho unafanya hapa.
Usifikiri unavyoona kijijini kwenu huko dunia nzima ndiyo iko hivyo.