Aliko Dangote asema kupata mtoto wa kiume sio kipaumbele chake

Tajiri namba moja barani Afrika,Aliko Dangote amesema kupata mtoto wa kiume sio kipaumbele chake.
Dangote alisema hayo wakati wa mahujiano na kituo cha televisheni cha Arise News cha nchini Nigeria.

Mtangazaji wa kipindi hicho alimuuliza Dangote kama ana mpango wowote kuhusu kupata mtoto wa kiume kwa sababu kwa utamaduni wa huko Kano anapotokea Dangote,mtoto wa kiume ndiye mrithi na muendelezaji wa jina la familia.

Dangote alijibu kuwa kupata mtoto wa kiume sio kipaumbele chake na pia Mungu ndiye anaeamua akupe mtoto wa jinsia ipi. Pia alisema wakati mwingine unaweza kuomba upate mtoto wa kiume lakini yeye ndio akawa chanzo cha kudondosha chini jina la familia.

Vilevile Dangote alimalizia kwa kusema,haamini kama watoto wa kiume wangeendesha kampuni zake kwa ufanisi zaidi kuliko mabinti zake wanavyofanya sasa.

Dangote amejaliwa kupata watoto watatu wakike ambao ni Halima,Fatima na Marya na wote tayari wanashikilia nafasi za juu za uongozi kwenye kampuni za baba yao.

Chanzo: Tuko News
Hapo ukute kuna mtoto sio wake ila alishikishwa tu na mkewe halafu mke ametunza Siri!
 
Sema wa

Sema watoto wa tajiri wamegoma aisee.
 
Ana mtoto wa kiume wa kuasili. Ila inasemekana hajaingizwa kwenye biashara za familia.

Hoja kuu ni uwezo si jinsia. Sio kila mtoto anakuwa unavyotaka awe, mwingine anaweza kutaka maisha ya kawaida na akajitenga kabisa na biashara za familia. Mabinti wameonesha uwezo.
 
Ndio ana mtoto wake wa kiume wa kuasili anaitwa Abdulrahman kama sijakosea,lakini kwenye biashara za familia sijaona jina lake .
 
Narudia tena asijikoshe, mwanaume yeyote rijali atataka kupata mtoto wa kiume katika watoto wake atakaozaa, siongelei nyie mashoga na watoto wa single mothers naongelea real men. Yeye kakosa mtoto wa kiume basi atulie asijioshe na kusema sio kipaumbele chake.
 
Hata mimi ninamuunga mkono. Mtoto ni mtoto tu. Ukifanikiwa kupata mtoto mshukuru Mungu. Akikujalia watoto wenye akili na afya njema mshukuru zaidi na zaidi. Full stop. Zingine ni mbwembwe tu.

Mimi nina watoto wa jinsia zote, na wote wana thamani inayolingana machoni pangu. Namaanisha wote ni watoto wangu.
 
Moto hauzai moto huyu jamaa na mihela yote hana kijana na ukweli ni kwamba wanawake ukimuachia ukwasi kama ule ataolewa mali zile zinaenda upande huo wa mumewe ...na pia mtu kama Raila na jina lake alivyojenga angekua na kijana ana akili kidogo angepitia upepo wa Raila akawa Kiongozi mkubwa kama Tshekedi alivyotumia upepo wa Baba yake tu kupata Urais.....

Jiulizeni hata hapa Tanganyika Nyerere angekua na mtoto au mjukuu anaejielewa angeenda mbali sana....Sasa tumebakia na majizi yanatumaliza kwa kupokezana;;;;
 
Narudia tena asijikoshe, mwanaume yeyote rijali atataka kupata mtoto wa kiume katika watoto wake atakaozaa, siongelei nyie mashoga na watoto wa single mothers naongelea real men. Yeye kakosa mtoto wa kiume basi atulie asijioshe na kusema sio kipaumbele chake.
Amekosaje mkuu amekwambia anatafuta? Angekuwa anatafuta ungekuta ana watoto 10 wakike huyo ndiye mtu anatafuta jinsia fulani lakini mtu ana watoto wawili au watatu huwezi kusema anatafuta jinsia fulani. Halafu maana ya urijali ni tofauti na jinsia ya mtoto utakaye mpata. Jinsia ya mtoto haitokani na mwanaume peke yake bali itategemea pia mzunguko wa mwanamke, hali ya uke wake, na mazingira ya ukeni. Tatizo hamuendi shele mnakuja kusumbua huku mtandaoni
 
Back
Top Bottom