Kuna jambo ambalo hamtaki kuelewa. Samia hajawahi kuwa karibu na Mbowe hivyo alipowekwa ndani na serikali yake hakushangaa. Na haikuwa mara ya kwanza. Lissu alikuwa mtu wake wa karibu sana na walipitia mengi pamoja. Hakutegemea kuwa Lissu atamgeuka na kusema na/au kuruhusu watu wamchafue jinsi walivyomchafua. Ni lazima ilimuuma kuliko alivyowekwa ndani DPP.
Na mbaya zaidi bado Lissu na wapambe wanaendeleza uchafuzi ule. Kwenda kwake Ikulu baada ya kutoka gerezani kumegeuzwa kuwa ishara ya usaliti. Kama wanavyosema " from Ukonga to Ikulu". Nadhani wanaamini watam shame ili awaangukie.
Anachofanya Mbowe ni kuwaonyesha kuwa yeye ni mtu huru atafanya anachoona yeye sahihi. Sio kama wale ambao nao wameanza kuweka rasta kwa sababu kiongozi wao ameweka rasta.
Mnajipotezea muda kumuandama Mbowe. Ameisha move on. Kama kweli mnaamini amewasaliti kwa muda mrefu, dawa ni kumfukuza kwenye chama. Kama ambavyo CCM walivyomfukuza msaliti wao.
Amandla...