"From Ukonga to ikulu"
Hiyo kauli kwa namna moja inaweza kuonekana kama kashfa, lakini pia kwa namna nyingine ni reality.
Ni la kebehi. Ni unafik ule ule uliotumika kumsingizia kuwa alilamba asali. Ule ule uliotumika kudai kuwa kuna hela za Abduli alipelekewa Lissu.
Mbowe alienda kweli Ikulu baada ya kutoka Ukonga. Akatoa tamko pamoja na Rais ambapo akazungumzia umuhimu wa Haki. Akatoa taarifa kwa chama chake. Chama chake kikachagua watu wa kuanza mazungumzo kuhusu maridhiano. Makamu Mwenyekiti wa sasa alikuwa Mjumbe. Chama chake kilipoona hamna kinacho endelea wakajitoa.
Aliitisha maandamano ya kupinga yanayoendelea nchini, na hao mashujaa wenu pamoja na wanachama na wananchi wengine hawakujitokeza kumuunga mkono.
Makamu Mwenyekiti wake aliposhambuliwa Mbeya alikimbia mara moja kuwa nae. Akakamatwa na kurudishwa Dar.
Makamu Mwenyekiti wake alimuunga wazi wazi Mwanachama mmoja muandamizi aliyekuwa anamtupia shutuma kibao za ovyo ovyo bila ushahidi wowote.
Makamu Mwenyekiti wake alikataa hadharani kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ambacho Mwenyekiti alikiita. Alipoulizwa alisema ana mambo ya maana zaidi.
Makamu Mwenyekiti alikataa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao chama chake kilisema kitahudhuria.
Yote haya, bado mnashangaa kwa nini Mbowe ameuachia uongozi wa sasa uendeshe chama kwa namna wanayotaka. Hajapinga lolote walilofanya hadharani au kuwashutumu kwa lolote lile kama ambavyo walimfanyia wakati wa uongozi wake.
So, sishangai kama wewe umeamua kuichukulia kwa upande wa kashfa, na maneno mengine uliyoongezea.
Ni kashfa maana hayakuwa na haja kuyatamka. Mbowe hayuko kizimbani.
Lakini naamini pia hutamshangaa yule atakayeichukulia hiyo kauli pale juu kama reality, kwasababu ule ndio ukweli uliojitokeza baada ya Mbowe kuachiwa toka gerezani.
Hakuna anaepinga kuwa Mbowe alienda Ikulu. Kinachopingwa ni kukataa ukweli kuwa mazungumzo ya maridhiano yaliyotokana na yeye kwenda Ikulu ndio yalitoa nafasi kwa wakina Lissu kurudi nchini, Chadema ( na vyama vingine) kuweza kufanya mikutano ya hadhara bila kificho. Kesi za maghumashi zilizokuwa zikiwakabili wanachama na wafuasi wengi wa Chadema kufutwa.
Leo kiongozi aliyewezesha yote hayo mnamuita msaliti, pandikizi la CCM n.k.
Lissu aliposema maneno yale alijua anachofanya. Mnyika na Heche walipoyarudia, walikuwa wanajua wanachofanya. Nia yao haikuwa njema kwa Mbowe.
Hebu sasa wote tutoke nje ya box tujiulize swali, je; Mbowe baada ya kutoka ikulu, aliendelea kuwa Mbowe yule kamanda mwenye misimamo au alikuja kupoa?
Nimekueleza kwa kirefu mambo mengi aliyofanya. Hata wakina Lissu wanakiri kuwa No Reforms No Elections ilitokana na uongozi wake.
Tukiwa bado nje ya hilo box, niambie kitu gani ambacho Chadema ya sasa imefanya zaidi ya Chadema ya wakati ule? Mbowe na wenzake walichangiwa milioni 300 ndani ya siku mbili. Huu uongozi wa wapambanaji mpaka sasa wanahangaika kupata milioni 300 na ushee kwa ajili ya Mkutano Mkuu wao. Wakati wa Mbowe tulikuwa tunasikia kila siku jinsi Chadema walivyokuwa wakipambana. Hao wapambanaji wote wameenda wapi?
Kwa upande wangu Mbowe alikuja kupoa sana, akawa wa baridi, mtu asiyeeleweka misimamo yake, na ndicho kitu kilichopelekea akapoteza ushawishi wake aliokuwa nao kwa wengi kwa muda mrefu.
Hapana. Watanzania mnataka dezo na hamkuwa tayari kusimama nae. Nafasi ilipojitokeza ya kumtosa, mkamtosa.
Nilisikitika sana kumsikia Lissu akiuliza kwa nini watu hawakuwa wengi Mahakamani. Kumbe ushujaa wa kumuunga mkono ni humu mtandaoni. Na kumbe sio Mbowe peke yake asiyeenda Mahakamani.
Amandla...