Alikubamiza miezi nane gerezani, leo mmekuwa marafiki wa kufa na kuzikana

Alikubamiza miezi nane gerezani, leo mmekuwa marafiki wa kufa na kuzikana

We kenge mbona huulizi kwanini mke wa Lissu hakuwahi kumtembelea mume wake gerezani wala kuhudhuria kesi mahakamani. Mbowe hawezi kwenda kumtembelea mshamba km Lissu, alimhangaikia kuokoa maisha yake badala yale Lissu anakuja kumtukana mtu km Mbowe? Lissu ni punda asiye na fadhili, Mbowe alikosea sana kumwachia chama, hata hivyo atakichukua chama chake
Sawa nini kenge, Muulize mana yako kama ukenge siutimizi mpaka ukaonekana duniani
 
Kwa mahakama za maagizo ulitegemea wasimkute na kesi ya kujibu? Ukitaka kujua ni mahakama ya maagizo, wanaanza kukwepesha mashahidi muhimu.
Ngoja tuone hili picha la kihindi
 
Mashtaka ya uongo kivip Babu wamemkuta ana kesi ya kujibu, ameanza kujitetea na mashahidi wanaendelea kumtetea na mbaya zaidi mahakama imewaita Wana usalama, kesi inasikilizwa open Kila mtu anaona kimasiala wanaweza kumnyoa mwenyekiti
Seems hujaenda shule au ni uchawa umeshakuwa part of your "genetic" make up
 
Mnaopenda gutter politics lazma mtaumiza mioyo yenu tu bure. Mh.Mbowe anajua maana halisi ya uongozi,upinzani na siasa kuliko wengi asa upande wa upinzani. Kinacho kosekana kwa sasa ndani ya CHADEMA hamna mtu mwenye hulka ya hivyo. Pamoja na yote Mh.Mbowe akuwai kuwataka wananchi na wafuasi wa CHADEMA waichome nchi...UKWELI NI KUA LISSU atoshi kwenye siasa zenye ustaarabu na utaifa..Kinachowagharim ndiyo hicho
So ulitaka Chadema iendelee kuongozwa na huyo dalali au siyo!
 
Ndugu ,you have nailed it... Mbowe ni mwanasiasa halisi sio mwanaharakati kwa aslimia ata 20% .Waliochukua chama kwasasa wao ni harakati,payuka,tukana,beza nk.. CHADEMA kwasasa aiwezi kufanya operation yenye maana kama enzi za Mbowe-OPERATION SANGARA
Kama haiweza fanya wewe inakuuma nini?
 
Ni la kebehi. Ni unafik ule ule uliotumika kumsingizia kuwa alilamba asali. Ule ule uliotumika kudai kuwa kuna hela za Abduli alipelekewa Lissu.
Mbowe alienda kweli Ikulu baada ya kutoka Ukonga. Akatoa tamko pamoja na Rais ambapo akazungumzia umuhimu wa Haki. Akatoa taarifa kwa chama chake. Chama chake kikachagua watu wa kuanza mazungumzo kuhusu maridhiano. Makamu Mwenyekiti wa sasa alikuwa Mjumbe. Chama chake kilipoona hamna kinacho endelea wakajitoa.

Aliitisha maandamano ya kupinga yanayoendelea nchini, na hao mashujaa wenu pamoja na wanachama na wananchi wengine hawakujitokeza kumuunga mkono.

Makamu Mwenyekiti wake aliposhambuliwa Mbeya alikimbia mara moja kuwa nae. Akakamatwa na kurudishwa Dar.

Makamu Mwenyekiti wake alimuunga wazi wazi Mwanachama mmoja muandamizi aliyekuwa anamtupia shutuma kibao za ovyo ovyo bila ushahidi wowote.

Makamu Mwenyekiti wake alikataa hadharani kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ambacho Mwenyekiti alikiita. Alipoulizwa alisema ana mambo ya maana zaidi.

Makamu Mwenyekiti alikataa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao chama chake kilisema kitahudhuria.

Yote haya, bado mnashangaa kwa nini Mbowe ameuachia uongozi wa sasa uendeshe chama kwa namna wanayotaka. Hajapinga lolote walilofanya hadharani au kuwashutumu kwa lolote lile kama ambavyo walimfanyia wakati wa uongozi wake.

Ni kashfa maana hayakuwa na haja kuyatamka. Mbowe hayuko kizimbani.

Hakuna anaepinga kuwa Mbowe alienda Ikulu. Kinachopingwa ni kukataa ukweli kuwa mazungumzo ya maridhiano yaliyotokana na yeye kwenda Ikulu ndio yalitoa nafasi kwa wakina Lissu kurudi nchini, Chadema ( na vyama vingine) kuweza kufanya mikutano ya hadhara bila kificho. Kesi za maghumashi zilizokuwa zikiwakabili wanachama na wafuasi wengi wa Chadema kufutwa.
Leo kiongozi aliyewezesha yote hayo mnamuita msaliti, pandikizi la CCM n.k.
Lissu aliposema maneno yale alijua anachofanya. Mnyika na Heche walipoyarudia, walikuwa wanajua wanachofanya. Nia yao haikuwa njema kwa Mbowe.

Nimekueleza kwa kirefu mambo mengi aliyofanya. Hata wakina Lissu wanakiri kuwa No Reforms No Elections ilitokana na uongozi wake.

Tukiwa bado nje ya hilo box, niambie kitu gani ambacho Chadema ya sasa imefanya zaidi ya Chadema ya wakati ule? Mbowe na wenzake walichangiwa milioni 300 ndani ya siku mbili. Huu uongozi wa wapambanaji mpaka sasa wanahangaika kupata milioni 300 na ushee kwa ajili ya Mkutano Mkuu wao. Wakati wa Mbowe tulikuwa tunasikia kila siku jinsi Chadema walivyokuwa wakipambana. Hao wapambanaji wote wameenda wapi?

Hapana. Watanzania mnataka dezo na hamkuwa tayari kusimama nae. Nafasi ilipojitokeza ya kumtosa, mkamtosa.

Nilisikitika sana kumsikia Lissu akiuliza kwa nini watu hawakuwa wengi Mahakamani. Kumbe ushujaa wa kumuunga mkono ni humu mtandaoni. Na kumbe sio Mbowe peke yake asiyeenda Mahakamani.

Amandla...
Umepofushwa na uchawa wako kwa Mbowe au ni ujinga wako binafsi.
 
Ndugu ,you have nailed it... Mbowe ni mwanasiasa halisi sio mwanaharakati kwa aslimia ata 20% .Waliochukua chama kwasasa wao ni harakati,payuka,tukana,beza nk.. CHADEMA kwasasa aiwezi kufanya operation yenye maana kama enzi za Mbowe-OPERATION SANGARA

..popote penye utawala unaotumia dhuluma, mabavu, na ukatili, lazima pataibuka wanaharakati.

..Na msimlaumu Mbowe kwani amejitahidi, na amefanya alichoweza.

..Mbowe asingekuwepo, huenda Chadema ingekuwa chama cha wanaharakati mapema zaidi.

..Tatizo sio Mbowe. Tatizo sio wanaharakati. Tatizo ni Ccm na mbinu zao za kidhalimu.
 
..popote penye utawala unaotumia dhuluma, mabavu, na ukatili, lazima pataibuka wanaharakati.

..Na msimlaumu Mbowe kwani amejitahidi, na amefanya alichoweza.

..Mbowe asingekuwepo, huenda Chadema ingekuwa chama cha wanaharakati mapema zaidi.

..Tatizo sio Mbowe. Tatizo sio wanaharakati. Tatizo ni Ccm na mbinu zao za kidhalimu.
Mimi nadhani tatizo ni wanaharakati maana mwanaharakati yeye kila kitu ni kibaya ..Vipi kuna mwaharakati anaesema tufanyie hiki harakati kwakua kimekua kizuri?
 
So ulitaka Chadema iendelee kuongozwa na huyo dalali au siyo!
Tupe faida na mafakio ya CHADEMA chini ya Lissu na chini ya Mbowe kama sio majanga tu. Mbowe akuwai kutwambia wafuasi wachadema kua tuchome nchi yetu sisi wenyewe
 
Huenda ushabiki ama ujinga umekutawala, Mbowe alipewa kesi ya ugaidi na shutuma zake ilikuwa ni kulipua vituo vya mafuta na kufanya uasi mwingi. Huenda wakati wa kesi ile ulikuwa hujajiunga na hizi siasa za majitaka. Mmekuwa mkishabikia siasa za hila kiasi kwamba mkifanya utetezi mnajikuta mnaji Contradict tu.
Mihemko na jazba aviwezi kua suluhu tofauti na kujivua nguo kamanda. Mbowe pamoja na kua na kesi ya ugaidi nk akuwai kusimama mbele ya chombo cha habari na kutuambiwa wafuasi na wanachama wa CHADEMA tuichome nchi yetu sisi wenyewe.
 
Kinachofanya ccm kuwakamata viongozi wa chadema kuwateka na kuwaua na wengine kuwafunga ni nini ? Ccm kihoja haina uwezo wa kushindana na chadema bila ya hizo figisu za kutumia vyombo vya dola na mahakama. Ndio maana nia yao ni kuiua chadema na sio kwamba waliopo hawana uwezo wakuongoza chama. Hata Mbowe hakuwa pekeyake kwenye uongozi alipokamatwa huyo huyo Lissu alitumia kila njia Mbowe aachiwe bila masharti kwani kesi ilikuwa ni ya kisiasa na alikuwa anaongea hadharani. Ni wapi Mbowe amefanya hayo?

Kiufupi ni kwamba Mbowe na ccm kiujumla na waliokuwa wanamuunga mkono wamechukia Lissu kuwa mwenyekiti wa Chadema ndio hayo yanayomtokea sasa, miezi miwili mbele baada ya uchaguzi akakamatwa ili anyamaze na sio kwa uharakati. Mbona kila siku wanamtaka wamwachilie halafu ahame nchini?
Hakuna anechukia Lissu kua mwenyekiti bali kinachochukiwa ni kauli za kuligawa taifa na kutaka watanzania wachome nchi yao wenyewe wakati yeye familia yake hipo ughaibuni salama.
 
Hakuna anechukia Lissu kua mwenyekiti bali kinachochukiwa ni kauli za kuligawa taifa na kutaka watanzania wachome nchi yao wenyewe wakati yeye familia yake hipo ughaibuni salama.

Hamna mahali alitamka watanzania wachome nchi yao, hilo limedhibitika kwa mashahidi wa juzi mahakamani. Hakuna mahali alitaka kugawa taifa, all he ever wanted ni tume huru, sio tume ya rais yenye makada ndani yake halaf utegemee uchaguzi huo uwe huru
 
Tupe faida na mafakio ya CHADEMA chini ya Lissu na chini ya Mbowe kama sio majanga tu. Mbowe akuwai kutwambia wafuasi wachadema kua tuchome nchi yetu sisi wenyewe
Aliyepewa kesi ya ugaidi kuwa anataka kuchoma vituo vyq mafuta ni nani? Au unajifanya mjinga makusudi. Nani alikuambia uchome nchi yako? Hivi hujioni ulivyo mjinga, mtu mzima kabisa unasema eti niliambiwa nikachome nchi yangu,huwezi kuwa sawa bro
 
Ninyi labda ndio mmemjua mbowe leo huyu ni CCM pure 100% akiona hela mbele yake mate yanajaa mdomoni
 
Wewe mwenyewe ulikuwa unatujazia server humu kumkampenia huyo jamaa aendelee kuongoza chama!!!

Leo humwelewi au ndiyo bendera kufuata upepo!
 
Back
Top Bottom